Watoto wa shule wanapata shida sana, kuwe na maazimio ya kitaifa

Watoto wa shule wanapata shida sana, kuwe na maazimio ya kitaifa

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Baada ya kusikia watoto waliofariki kwa kuzama mtoni, nikakumbuka takwimu zinazoonesha idadi ya watoto wanaovuka maji kufika shule, idadi ya watoto wanaovuka maeneo yenye wanyama hatarishi kufika shule. Serikali inajua kuhusu hilo, kwa kuwa takwimu hizi nazitoa kwao.

Basi nikaingia niangalie data za watoto hao, nikakumbana na data nyingine ambazo nikalazimika kuzichungulia. Aisee 23.1 ya watoto wa shule nchini, wanajilea wenyewe. 19.3 wanalelewa na bibi zao. Wanaolelewa na mama zao ni wengi kuliko wanaolelewa na baba zao.

Naendelea kuchimba hizi data nije na story nzuri, lakini kwa hali hii nathubutu kusema hali kwa watoto ni mbaya. Ikumbukwe kuwa kwenye taarifa za kuhusu shule na utoro wapo watoto wengi wanaoacha shule kwa kuwa ni walezi wa familia zao.

Fikiria risk anayokumbana nayo mtoto anayelelewa na mezi ambaye hana kipato, ambao ni 0.5% fikiria wanaolelewa na bibi na babu.

Hali hii inahitaji mkakati wa kitaifa ili kuokoa maisha ya watoto na kutengeneza taifa lenye good human Capital.
 
Back
Top Bottom