JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Takwimu za Umoja wa Mataifa (UN) zimeeleza vifo hivyo vinatokana na changamoto za kiafya au ulemavu unaohusiana na masuala ya uzazi.
Changamoto hizo za kiafya pia zimechangia vifo vya Watoto 170,000 wenye umri wa mwezi mmoja 1 hadi miaka mitano kwa mwaka.
============
An estimated 240,000 newborns die within 4 weeks of birth every year due to birth defects and lack of access to quality care services.
WHO has details on how to help prevent, detect and treat congenital anomalies
Source: UN
=========
Akielezea kuhusu "Congenital disorders", Daktari Mkunga Elisha Makarabo kutoka UMATI Nchini Tanzania anasema, hizo ni changamoto / Ulemavu ambao anazaliwa nao mtoto.
Inaweza kutokea wakati Mtoto anaumbika ndani ya mfuko wa uzazi na akazaliwa na ulemavu flani ambao ukauona direct au anaweza zaliwa na ulemavu ambao usiugundue wakati huo na ukaja kugundulika baada ya kipindi au miaka kadhaa.
Kiufupi ni tatizo au ulemavu anaozaliwa nao mtu au mtoto, mara nyingi inaweza sababishwa na baadhi ya dawa ambazo anatumia mama mjamzito ambazo si salama kwa kipindi husika au ikatokea tu.
Mfano wa changamoto hizo;
- Kichwa kikubwa
- Midomo sungura
- Mgongo wazi
- Mtindio wa ubongo
- Club foot/ Talipes equinovarus
- Digital figures n.k