SI KWELI Watoto wachanga hawahisi joto

SI KWELI Watoto wachanga hawahisi joto

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Imezoeleka kuona watoto wachanga wakiwa wamefunikwa manguo mengi sana, hii sio shida iwapo hali ya hewa inaruhusu yaani ya ubaridi au ya kawaida.

IIa kunaweza kuwa na hali ya joto kali watu wazima mnatamani kukaa kwenye feni ila mtoto mchanga bado kafunikwa mablanketi na kavishwa sweta, ukihoji unajibiwa watoto wachanga hawahisi joto.

Wapo wanaotetea hoja hii kwa madai tumboni kulikuwa na joto hivyo mtoto hawezi hisi joto bali huhisi baridi muda wote.

Je, hii ni kweli?

1717662771071.png
 
Tunachokijua
Watoto wachanga ni binadamu wadogo ambao wametoka kuzaliwa na mara nyingi wanakuwa na umri chini ya mwaka mmoja. Shirika la Afya Duniani (WHO) linafafanua mtoto mchanga, kama mtoto aliye chini ya siku 28. Kwa upande wao Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Marekani (CDC) vinadokeza kuwa hatua za mtoto mchanga zinaanzia kuzaliwa hadi kufikia umri wa mwaka mmoja.

Kumekuwa na hoja ya kijamii ikidai kuwa watoto wa changa hawapati hisia ya joto hata kama kukiwa na joto kali. Hali hii imesababisha wazazi wengi kuwavunika nguo nzito wakati wote bila kujali hali ya hewa iliyopo.

Upi ukweli kuhusu dhana hii?
JamiiCheck imefuatilia vyanzo mbalimbali kutoka kwa Wataalamu wa Afya ambao wote wamekanusha ukweli wa dhana hiyo na kubainisha kuwa mtoto mchanga kama walivyo watu wazima pia huweza kuhisi baridi na joto.

Mathalani, Daktari na Mkufunzi wa Afya kutoka KCMC, Norman Jonas amekanusha hoja ya mtoto kutohisi hali ya joto kwa kuelza kuwa, mtoto kama walivyo binadamu wengine wanasikia hali ya baridi na joto. Akifafanua kwa ufupi hoja hii Norman Jonas anasema:

Hiyo ni dhana tu, hakuna ukweli wowote Kisayansi, Mtoto anasikia baridi na anasikia joto kama ilivyo mtu mwingine yeyote.
Ndio maana mtoto anaweza kutetema kwa kusikia baridi na kama joto litazidi anaweza kupata magonjwa yanayotokana na joto pia
Me mtot wangu feni ikizimika tu anaamka kwa joto
 
Back
Top Bottom