Watoto wafariki kwa kula mihogo yenye sumu

Watoto wafariki kwa kula mihogo yenye sumu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Watoto wanne wa familia moja wamefariki dunia nchini Tanzania, baada ya kula mihogo inayodaiwa kuwa ilikuwa na sumu.

DW imezungumza na Dr. Sadick Sizya kuhusu madhara ya kiafya yanayoweza kusababishwa na mihogo mibichi ama michanga.
 
Attachments

Mwezi wa 9 nilikwama ktk nchi jirani ambapo nilipeleka mzigo vijijini huko, gari ilinasa ktk kijiji kimoja nilikaa hapo siku karibia nne kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha huko.

Nikaishiwa chakula chote, akapita mzee mmoja anauza mihogo mikubwa kweli kweli na kwa kuwa nilikuwa nna njaa basi nikanunua ya buku kwa pesa ya kwao, dah ilikuwa ni michungu sipata kuona, nikaghair nikahisi hii ndio ile niliyokuwa nasikiaga inaweza ikawa ni sumu.

Ckuitupa nikaiweka pembeni lakin kadri njaa ilivyozidi usiku niliishughulikia tu hivyo hivyo nikasema kama ni sumu basi mm nafia huku nchi ya watu.

Nashukuru kwa kweli iliuvusha ule usiku na kesho yake nikafanikiwa kutoka lile eneo. Lakini ki ukweli ni vigumu sana kujua muhogo upi ni salama na upi si salama mpaka uwe unaijua
IMG_20191010_122937.jpg
 
Mihogo yenye sumu inapatikana sana maeneo ya kahama miti yake inakuwa mikubwa kiasi kwamba ukiwa unachuma kisamvu chake itakulazimu upande juu jina limenitoka kidogo ila kwa mwenye ufahamu wa jina atusaidie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwezi wa 9 nilikwama ktk nchi jirani ambapo nilipeleka mzigo vijijini huko, gari ilinasa ktk kijiji kimoja nilikaa hapo siku karibia nne kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha huko. Nikaishiwa chakula chote, akapita mzee mmoja anauza mihogo mikubwa kweli kweli na kwa kuwa nilikuwa nna njaa basi nikanunua ya buku kwa pesa ya kwao, dah ilikuwa ni michungu sipata kuona, nikaghair nikahisi hii ndio ile niliyokuwa nasikiaga inaweza ikawa ni sumu. Ckuitupa nikaiweka pembeni lakin kadri njaa ilivyozidi usiku niliishughulikia tu hivyo hivyo nikasema kama ni sumu basi mm nafia huku nchi ya watu. Nashukuru kwa kweli iliuvusha ule usiku na kesho yake nikafanikiwa kutoka lile eneo. Lakini ki ukweli ni vigumu sana kujua muhogo upi ni salama na upi si salama mpaka uwe unaijuaView attachment 1290483
Mkuu naomba ajira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ardhi ya Burundi hii mkuu, ulilipa noti imeandikwa AMAFARANGA IGIHUMBI-IBIKOGWA, UBUMWE, N' AMAJAMBERE.

karibu tena Gitega kwetu!
Mwezi wa 9 nilikwama ktk nchi jirani ambapo nilipeleka mzigo vijijini huko, gari ilinasa ktk kijiji kimoja nilikaa hapo siku karibia nne kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha huko. Nikaishiwa chakula chote, akapita mzee mmoja anauza mihogo mikubwa kweli kweli na kwa kuwa nilikuwa nna njaa basi nikanunua ya buku kwa pesa ya kwao, dah ilikuwa ni michungu sipata kuona, nikaghair nikahisi hii ndio ile niliyokuwa nasikiaga inaweza ikawa ni sumu. Ckuitupa nikaiweka pembeni lakin kadri njaa ilivyozidi usiku niliishughulikia tu hivyo hivyo nikasema kama ni sumu basi mm nafia huku nchi ya watu. Nashukuru kwa kweli iliuvusha ule usiku na kesho yake nikafanikiwa kutoka lile eneo. Lakini ki ukweli ni vigumu sana kujua muhogo upi ni salama na upi si salama mpaka uwe unaijuaView attachment 1290483

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mihogo michungu itatumiwa kwa ajili ya unga wa ugali baada ya kuondoa sumu kwa njia ya kuvundika kwa siku kama tano hivi, hiyo teknolojia ipo vijijini miaka kibao na sisi wengine tumekuzwa na ugali wa mhogo
 
Watoto wanne wa familia moja wamefariki dunia nchini Tanzania, baada ya kula mihogo inayodaiwa kuwa ilikuwa na sumu.

DW imezungumza na Dr. Sadick Sizya kuhusu madhara ya kiafya yanayoweza kusababishwa na mihogo mibichi ama michanga.

Hii stori inasikitisha sana. Actually hawa watoto wamekula hiyo mihogo michungu baada ya kuwa wamekosa alternative, hawakuwa na chakula kingine.

Ni watoto yatima wanalelewa na mama mjane. Mimi nimeshangaa kuwa Nchi hatuna njaa, inakuwaje watu wanakufa kwa kukosa chakula na tunao huko viongozi wa serikali za mitaa na ngazi zingine za chini zinazofuata baada ya mtaa, zinazoweza kuwa na taarifa za kila kaya kwa urahisi? Ningekuwa Mkuu wa Wilaya huko, kuna watu ningewapeleka mahakamani na ningejitahidi kuhakikisha kuwa hawashindi hii kesi! Inakuwaje watu wanakufa kwa kukosa chakula wakati hatuna njaa? Na hata kama tungekuwa na njaa, bado huwa siyo rahisi sana watu kufa kwa njaa. Kunaweza kukawa na viongozi wa ngazi za chini huko ambao wana roho mbaya, hawajali wanachi. Inaumiza sana
 
Back
Top Bottom