Watoto wakisoma shule za St. Kayumba wanakua strong sana kichwani na wanakua na hekima msikilize Jesca Magufuli

Watoto wakisoma shule za St. Kayumba wanakua strong sana kichwani na wanakua na hekima msikilize Jesca Magufuli

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
9,397
Reaction score
12,415
Elimu siyo tu madarasa ya kifahari, bali ni msingi wa maadili, busara, na hekima. Watoto wa viongozi wanaosoma shule za kawaida kama St. Kayumba hukutana na changamoto nyingi zinazowajenga kiakili na kimaisha. Hawa watoto hujifunza kuwa na nidhamu, kuwaheshimu watu wa kila hali, na kuthamini kila hatua ya mafanikio yao.

Musikilize Jesca Magufuli. Maneno yake, msimamo wake, na hekima yake vinaonyesha wazi kuwa elimu ya msingi yenye maadili na kujifunza miongoni mwa jamii mbalimbali humjenga kiongozi wa kweli.

Usiogope kumpeleka mtoto wako shule ya kawaida. Pengine ndipo hekima yake na ujasiri wake vitakapozaliwa. Maisha hayahitaji tu maarifa darasani, yanahitaji pia tabia, heshima, na busara vitu ambavyo shule za kawaida mara nyingi huvipatia nafasi ya pekee.
 
Darasa Moja wanafunzi 100 ndio kuwa Strong?

Mwaka mzima baadhi ya masomo unafundishwa topic moja ndio kuwa Strong?

Waalimu kutukana na kuchapa wanafunzi kama wendawazimu Ndio kuwa strong?

Watoto kushinda njaa shuleni ndio kuwa strong?

Umaskini sio sifa njema.

Ogopa shule ambayo wanasiasa au wenye vipato hawazipendi
 
Hamna kitu hapo ashukuru baba yake aliwatengenezea njia ya kufanikiwa .

Kwakuwa wenzake waliopata four ya 30 ndoto ziliishia hapo za kusoma.

Pia watoto wa Magufuli wamesoma kayumba primary maana Jeremiah kasoma feza na huyo Jesca Kamalizia form four st Marry je hizo ni st kayumba?

ni uongo, jesca hajamaliza form st marys, weka ushahidi kamaliza form 4 st marys mwaka gani ?
 
Darasa Moja wanafunzi 100 ndio kuwa Strong?

Mwaka mzima baadhi ya masomo unafundishwa topic moja ndio kuwa Strong?

Waalimu kutukana na kuchapa wanafunzi kama wendawazimu Ndio kuwa strong?

Watoto kushinda njaa shuleni ndio kuwa strong?

Umaskini sio sifa njema.

Ogopa shule ambayo wanasiasa au wenye vipato hawazipendi
Kibongo bongo huwa tunapenda kupata stories za mtu alie fanikiwa kwa tabu mno , ukileta stories za kuendeleza pesa za familia unaonekana kiazi tu , ingia kwenye peg za mo dewji uone anavyochukuliwa poa 🤔
 
Hamna kitu hapo ashukuru baba yake aliwatengenezea njia ya kufanikiwa .

Kwakuwa wenzake waliopata four ya 30 ndoto ziliishia hapo za kusoma.

Pia watoto wa Magufuli wamesoma kayumba primary maana Jeremiah kasoma feza na huyo Jesca Kamalizia form four st Marry je hizo ni st kayumba?

magufuli hajawai kutoa hela zake kusomesha shule expensive kama feza, huyo ni mtoto wa nje ya ndoa amesomeshwa na mama yake, single mother huwa wanapenda kujitutumua, ila baada ya magufuli kuwa rais, serikali ndio ikampeleka feza maana ukiwa rais serikali inabeba majukumu yako ya ada za wanao kama benefit za urais. kwa ufupi mtoto huyo amesomeshwa feza na serikali ya Tanzania, sawa sawa na kikwete alivyosomeshewa watoto wake Feza na serikali
 
magufuli hajawai kutoa hela zake kusomesha shule expensive kama feza, huyo ni mtoto wa nje ya ndoa amesomeshwa na mama yake, single mother huwa wanapenda kujitutumua, ila baada ya magufuli kuwa rais serikal ndio ikampeleka feza maana ukiwa rais serikali inabeba majukumu yako ya ada za wanao kama benefit za urais
Haya ndo mambo mnaweza kuwashika watu masikio
 
Hizo ni fikra za Kimaskini.
Kwamba uteseke ndipo utoboe
Na huu upumbavu ndo walikuwa nao wazazi wetu.

Wanasema kila mtoto atazaliwa na bakuri yake.

Usipowapa hela wanasema utakosa baraka na ukiwasaidia wanasema utbarikiwa na wengin watakutishia kukupa laana.

Tunabidi tusirudie haya makosa kuamini MTU anabidi kuteseka ndo atoboe au anabidi kufanikiwa kwa bahati
 
Back
Top Bottom