Dr Msaka Habari
Member
- Apr 9, 2022
- 66
- 32
Hayo yamezungumzwa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Shirika hilo Thabisani Ncube, katika Mkutano wa pili wa Kimataifa wa Ubora wa Elimu ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).
Alisema kuwa shirikisho linajukumu la kuhakikisha jamii inajua kusoma na kuandika hivyo wanatoa udhamini na mahitaji mengine muhimu kwa watoto hao.
"Tuna programu ya kutoa mafunzo kwa walimu waliopo Makazini kwa kuwajengea uwezo wa kutosha ili watoe elimu bora kwa wanafunzi" alisema Ncube.
Hata hivyo alisema mbali na udhamini huo wanatoa chakula kwa wanafunzi Mashuleni ili kuwasaidia kufatilia vyema masomo na kuhakikisha wanapata ufaulu wa juu.
Eidha aliongeza kuwa kuna shule sita eneo la Umasaini nako pia wanatoa huduma ya chakula kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Meneja wa Mafunzo kwa walimu Noah Kamanda alisema kuwa wanaprogramu ya mafunzo kwa Viongozi wa shule nayo wanatoa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji.