Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Watoto wawili wa familia moja, Ester Hillary na Eliana Hillary, ambao walikuwa wanafunzi wa shule za msingi na wakazi wa Mtaa wa Ikindwa, Kata ya Mapambano, Manispaa ya Tabora, wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia Septemba 13, huku mtoto mmoja akinusurika kifo.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mama wa watoto hao aliwafungia ndani na kuelekea kwenye ibada ya asubuhi. Aliporudi alikuta nyumba ikiwa imejaa moshi mzito, na watoto wakiwa hawajazimia kabisa bali wakipumua kwa shida.
Soma Pia: Watoto watatu familia moja wafariki kwa moto
Majirani wameeleza kuwa waliwahisha watoto hao hospitalini, lakini licha ya jitihada za madaktari, walifariki dunia wakiwa bado wanapatiwa matibabu. Chanzo cha moto huo kinahusishwa na mmoja wa watoto, ambaye inadaiwa alikuwa na tabia ya mara kwa mara ya kuchezea kiberiti.