Watoto Wenu Muwalee Wenyewe

Watoto Wenu Muwalee Wenyewe

Mimi Ni Mtu Wa Mungu

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2021
Posts
679
Reaction score
1,295
Siku hizi mnawaachia walimu kazi ya malezi yaani nyie mmejichomoa kabisa eti mpo busy 'kutafuta maisha'

Walimu kazi yao ni kuwafundisha herufi na silabi kwa msingi wa kujua kuandika
1+1, 2+2 kwa msingi wa hesabu

Walimu kumfunda mwanao heshima na tabia njema kwa ujumla sio kazi yao ni ya kwenu
Ni miaka michache mwalimu na mwanafunzi watakuwa pamoja lakini ni miaka yote mzazi na mwanao mtakuwa pamoja

Na kwa hili mwalimu hana hasara hata mwanao akiwa nunda/shoga mwenye hasara ni wewe.

ASUBUHI NJEMA
 
Mwalimu atalea vipi watoto mia 8 huku ana stress ya umasikini.
Mkiambiwa wachangieni walimu hata buku buku mnapiga kelele.
Kama tunaweza wachangia pesa mitume na manabii wa uongo wakaishi kifahari kwann tusiwachangie walimu waishi vizuri kutulelea watoto?
Kila mzazi akitoa elf moja kila mwezi KWA ajili ya posho ya walimu walimu hawatowaza mikopo au deiwaka Ili waishi watawaza kufundisha tu na sio kingine.
 
Kila mtu alee mwanae, walimu nao wana majukumu ya kulea watoto wao.
Kumekuwa na kesi nyingi za kuwashughulikia walimu negatively na kuhatarisha ajira zao, hivyo ninawasihi walimu wafundishe ipasavyo ila suala la nidhimu na maadili wazazi wahusike.

Leo hii mwalimu akimchapa mwanafunzi bahati mbaya akadhurika zahama anayokutana nayo si ya mchezo, hivyo kila mtu alee mwanae asitegemee msaada wa mwalimu pekee.
 
Serikali ipige marufuku kambi na mabweni uchwara hasa kwa watoto wadogo.

Katika hili kusiwepo na kisingizio chochote.

Mzazi kaa na mwanao mlee mfundishe tabia njema na maadili mema mwenyewe.

Akifikisha 18 angalau anakuwa ameshajua mbivu na mbichi.
ndio maana yangu mkuu ahsante
 
Siku hizi mnawaachia walimu kazi ya malezi yaani nyie mmejichomoa kabisa eti mpo busy 'kutafuta maisha'

Walimu kazi yao ni kuwafundisha herufi na silabi kwa msingi wa kujua kuandika
1+1, 2+2 kwa msingi wa hesabu

Walimu kumfunda mwanao heshima na tabia njema kwa ujumla sio kazi yao ni ya kwenu
Ni miaka michache mwalimu na mwanafunzi watakuwa pamoja lakini ni miaka yote mzazi na mwanao mtakuwa pamoja

Na kwa hili mwalimu hana hasara hata mwanao akiwa nunda/shoga mwenye hasara ni wewe.

ASUBUHI NJEMA
Ahsante sana mkuu
 
Back
Top Bottom