Watoto wenu wote wanapitia hatua hii?

Chemwali

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2011
Posts
397
Reaction score
178
loh jamani naomba msaada wenu,my son ana miaka 3...ndo ameanza shule january..yaani before i never experience kuandikwa andikwa ndani but nw imekuwa hectic...nimeshamgombeza hadi kumchapa na kwa kuwa akili yake inaelewa hata nikimwambia nilikwambiaje anajibu niandike kwenye book tu....but baada ya muda atajisahau ataenda achukue pencil,pen au colour aanze kuchora ukuta kwa kuimitate like teacher,au kochi,au karpet chini au meza yaani ni chochote kilicho mbele yake...nanunua notes books,paper,na hizi ubao za plastic zenye automatic ufutio but wapiiii atataka kule kule...wengine mlifanyaje?au ni jambo la kusubiri tu huo msimu upite?
 
Chemwali nakupa ushauri tu wa bure, acha hicho kipindi kipite maana utamuumiza bure kwa viboko na haita saidia chochote huo ndio umri wake. Hata mie chumba changu kilikuwa kimeandikwa utadhani ndio chumba cha mafunzo ya chekechea kilikuwa na kila aina ya michoro (ilifika wakati akikosa pencil au chaki anatumia wanja au lipstick kuandika) lakini ilifika wakati alicha mwenyewe kuandika kwenye ukuta. sasa hivi nina kazi ya kununua madaftari mapya kila siku.
 
Ni kawaida yao hata ukichapa hataacha.Kipindi hicho kitapita tu.
 
Hakyani ili tulazimu kupiga rangi almost the whole house...Nafikiri hii hali kila mtoto aipitie...
 
pole... nilifikia kubadilisha aina ya viti kwa kuchorwa na watoto katika kipindi cha umri huo, sasa wametulia... Acha kipindi kipite...!
 
Wa kwangu makochi yamekuwa kituko, hadi mashuka ni wino mtupu
 
mashuka ndo uwiiii ukiona tu yuko chumbani piga alarm kichwani kwamba utamkuta kwenye shuka hahaa mh
 
nimechekaaaaaaa..... nawapenda watoto lolz. Wanaleta furaha sana ndani ya nyumba.
 
Wanapenda sana kuchora ukuta wanafananisha waalim wao wanavyoandika ubao!
 
binafsi nahisi huyo mtoto wako hana watoto wengine karibu wa kumkeep bize, na hii inamfanya awe anajikeep bize pekee yake hivyo hata ukimkanya mwili wake unataka hivyo anajisahau tu baada ya muda. nakushauri uwe unamchanganya na watoto wenzake ili asumbuane nao hii itampelekea awe anachoka na akija kwako atakuwa na njaa na usingizi tu hivyo akila hatakusumbua tena ataishia kulala
 
Ni kawaida ya watoto wa umri huo, hata wa kwangu amemaliza nyumba kwa kuchora. Anyway nina kazi ya kuweka rangi nyumba nzima. Lakini sikuwahi kumchapa hata siku moja, wala sitomchapa. Tukumbuke na sisi tulitokea huko huko.
 
ni kipindi tu kinapita, atacha mwenyewe huna haja ya kumwadhibu mtoto anajifunza.
 
mkuu Chemwali, na mimi wangu umri huohuo nae kaanza january shule,
yaani kila kona ya ukuta, kabati na hadi kwenye friji ameandika.
lakini ni msimu tu utapita usimchape.
 
Last edited by a moderator:
Wangu mimi alikuwa anachora hadi vitandani utakuta kitanda kimechorwa mashuka ndo usiseme hadi milango yote ikafikia muda akaacha mwenyewe muache tu wakati ukifika ataacha
 
Tuombe Mungu waendelee kupenda kujifunza hata baada ya chekechea.
 
Mdogo wangu aliamua kuweka label kika mlango nyumbani. Chooni, jikoni etc.
Wataalamu wanashauri ununue flip chart ubandike ukutani. Sehemu moja unaweza kuweka sebleni, jikoni na chumbani kwake. Kubaliana nae kuwa hapo tu ndo atakapoandika na sio sehemu nyingine yoyote. Jaribu kumuelewa...yuko excited amegundua kitu kipya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…