SoC02 Watoto wenye ulemavu na elimu maalumu

SoC02 Watoto wenye ulemavu na elimu maalumu

Stories of Change - 2022 Competition

Kenyanya

New Member
Joined
Aug 23, 2022
Posts
3
Reaction score
1
Wengi tunawafahamu na kuwapita njiani, ni ndugu zetu ila hatuwajali, niwanetu ila tunawaficha, tunawafungia, hatuwapi elimu. Wengine hukufuru na kusema watasoma nini ili wawe nani? wengine pia huwatumia kama vitega uchumi katika miji na majiji katika umri mdogo. Ila wao husema nimipango ya mungu ila kwanini walimwengu watufanyie hivi?. Tunataka kusoma katika mazingira bora kama wanafunzi wengine. Swali ni kwamba jamii haina uelewa juu ya watu au watoto wenye ulemavu au tumeamua kumwachia mungu baada yakuwapitisha kwenye mateso na mwisho kusema " amefariki muache apumzike kateseka sana, huo ni mkosi au laana".

Wacha Mwalimu Tinshu nijikite kuwahabarisha Maputo ya watoto au wanafunzi wenye ulemavu katika kupata haki yao ya Elimu. Je wafahamu watoto wenye ulemavu wanaweza pata elimu nakutimiza ndoto zao na familia zao?. Iko hivi kupitia elimu maalum wanafunzi hawa wanaweza kunufaika.

Elimu maalum ni utaratibu wa ufundishaji wa wanafunzi wenye uhitaji maalumu katika njia nzuri kulingana na mahitaji yao. Njia au mbinu nzuri ni pamoja na matumizi ya lugha alama, na video kwa wanafunzi wasiosikia, matumizi ya nukta nundu na vitabu vya sauti kwa wanafunzi wasioona na mpango binafsi, picha, vitu halisi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa akili. Muingoni mwa makundi ya wanafunzi wanaohitaji Elimu maalumu ni walemavu wa akili, usonji, walemavu wa macho na walemavu wa usikivu (wasiosikia).

Baada yakumaliza shahada ya elimu maalum niliamua kwenda kujitolea shule ya msingi Ludete (Geita), yenye kitengo cha elimu maalum ( wasiosikia, wenye huoni hafifu, usonji na ulemavu wa akili) lengo likiwa kufanyia kazi taaluma yangu ili niongeze ujuzi vilevile kukidhi haja yangu yakua sehemu ya kuleta tabasamu na matumaini kwa watoto wenye ulemavu na familia zao.

Siku ya kwanza kazini mtoto mwenye usonji (Big) alipotea. Mama la mama ambaye ni mkuu wa kitengo cha elimu maalum akasema "Tinshu tukamtafute" huku akikimbia kuwauliza walimu waliokuwa nje nao wakajibu "tatizo mnadeal na ndagu za watu". Niliumia sana kusikia hivo hasa kutoka kwa mwalimu mwenzetu, ndipo tukaingia mitaa ya Katoro kwa muda wa masaa mawili tukawa tumempata kwa msaada wa wanafunzi na wazazi wake.

Suala la imani potofu kama ushirikina ni kubwa sana. Kuanzia kwa walimu, wazazi na jamii kwa ujumla. Hii ni changamoto kubwa kwa elimu maalum, kuanzia katika ubainishaji wa mtoto majumbani kwao. Watoto hufungiwa kama wanyama ndani, mtoto kupelekwa Kwa waganga nakuchajwa na kufanyiwa matambiko kukatishwa masomo sababu kapelekwa kwa mganga. Hali hii imepelekea vifo na udumavu Kwa watoto hawa . Vilevile kuja shule akiwa amevaa ilizi.

Upungufu wa miondombinu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu. Hasa madarasa na vyoo, Mama la mama anasema wakati wananzisha kitengo walipigwa marufuku kutumia darasa lenye sakafu kwa watoto wenye ulemavu ilehali watoto wenye akili timamu wanasomea kwenye vumbi. Baada ya jitihada kubwa walipewa hilo darasa moja lakini halitoshi kulingana na idadi ya wanafunzi na aina tofauti za ulemavu. Mfano katika darasa letu kuna wanafunzi wasiosikia, ni ngumu kujifunza lugha alama maana huwasiliana na kucheza darasani na watoto wenye ulemavu wa akili hivo hutengeneza alama zao.

Kadri Siku zinavyokwenda Tishu nilizidi kuzoea mazingira nakua sehemu ya mabadiliko.

Utoaji wa elimu Kwa walimu, wazazi na jamii juu ya ulemavu hasa wa akili ilikua sehemu ya maisha yangu. Tulitoa elimu kwenye vikao vya shule sababu ilifikia hatua walimu wanazuia baadhi ya wazazi wasilete watoto idarani kua hawana ulemavu na wataambukizwa. Elimu hii pia ilifika hadi nyumba kwa nyumba hasa kwa wazazi wenye watoto walemavu waliosajiliwa shuleni na wasiosajiliwa kila siku ya ijumaa. Hali hii ilipelekea ongezeko la ubainishaji na usajili wa watoto wenye ulemavu.

Vilevile ujenzi wa madarasa mawili ulianza kwa juhudi ya mkuu wa shule "Baba na uongozi wa wilaya hatimae jengo likapauliwa. Ukweli ni kwamba tumekwama katika ujenzi huo , nitumie fursa hii kuomba wanajamii na wadau wa elimu mtusaidie kumalizia hili jengo. Ili watoto wapate sehemu nzuri ya kusomea kulingama na aina zao za ulemavu, vilevile miondombinu mizuri ya vyoo.

Kikubwa zaidi niufundishaji wa watoto hawa, tunao watoto wenye ulemavu wa akili na usonji tunawafundisha stadi za mawasiliano, stadi za viungo, stadi za afya na kusoma kuhesabu na kuandika. Watoto wasiosikia wapo wa darasa la kwanza na la pili. Tunaouhitaji wa dhana na vifaa vya kufundishia hasa vyakidijitali kama printer. Hii itasaidia kutoa picha za vitu vyenye uhalisa kwajili ya kujifunzia.

Suala la Afya kwa watoto hawa ni jambo la msingi. Nitumie jukwaa hili kuomba upatikanaji wa bima za afya 47 kwa watoto hawa.

Nishukuru serikali kwa kutenga fungu la chakula kwa watoto hawa. Kiukweli kimekua kichocheo kikubwa cha ustawi wa kitengo cha elimu maalum. Si unajua tena panapokua na wali mambo hua mazuri. Kuanzia kwenye maudhulio hadi jitihada za ujifunzaji zimefanya kitengo kushamiri.

Ni mimi na wewe wakuwasemea watoto hawa, kuwasaidia, kuwatetea na kutengeneza mazingira mazuri wapate elimu bora.

Ni miakamiwili sasa maisha yangu yakujitolea yamekua yakujifunza zaidi hasa baada ya mama la mama kutoka semina mbalimbali zinazoandaliwa na serikali na huzitafsiri kwa kutoa ujuzi huo kwa watoto na jamii kwa ujumla.

Wakati unakwenda Mama la mama nikama mwenye masikitiko, najalibu kumuuliza kinacho msibu. " Tinshu naamishwa nakua mkuu wa shule, maisha yangu ni elimu maalumu". Kiukweli napigwa na butwaa inakuwaje hivi ila ndo uhalisia jembe letu linaondoka hatutakua nae muhula ujao baada ya Sensa. Uhaba wa walimu utakuwepo na kitengo kitakupo.

Wasalaam;
Mwil.TINSHU.
 
Upvote 2
Habari yako ndugu, Kenyanya.

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, nipate mawazo yako au mapendekezo juu ya nakala ihusuyo


Ahsante!!
Asante sana
 
Back
Top Bottom