Watoto!!

Watoto!!

View attachment 25640View attachment 25639View attachment 25638

"... wewe kaka acha tu! huyo ni mkorofi sana hivi ukimfungulia kamba hapa anazunguka mitaa yote ya mji wa Tanga na hapo alipo ana majeraha ya kupigwa na kuchanjwa na nyembe kutokana na ukorofi wake hivi tumeaona njia pekee ni kumfunga kamba na kumchunga kama ng'ombe akiwa malishoni japo na usiku akilala tuna mfunga kamba pale anapolala" alisema mwanamke huyo anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 23 na 25

Hata hivyo anasema mbali ya kufungwa kamba pia kwa upande wa chakula wamekuwa wakimwekea katika sahani yake maalum na kula akiwa amefungwa kamba huku kwa wiki ama mwezi huoogeshwa mara moja.

Alisema kuwa sababu za kufungwa na kutengwa na familia ni kutokana na tatizo hilo la utindio wa ubongo linalomkabili na kupelekea hali ambayo ndani ya familia yao wamekuwa wakiona kama ni aibu kwa kijana huyo kutembea mitaani na tatizo hilo.

Pia alikili kuwa kijana huyo amekuwa na uwezo mkubwa wa kutambua japo hajapata bahatika kupelekwa shule na kuwa sehemu kubwa hata kutamka baadhi ya maneno ameanza kujifunza baada ya kuanzishwa kwa utaratibu wa kumfunga kamba nje ya nyumba hiyo na hivyo kubahatika kujifunza kuongea kwa kusikika kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakipita eneo hilo.

“Ujue awali tulikuwa tukimfungia ndani pasipo kutoka nje na jua ameanza kuliona sasa ndani ya miaka mitano hii ila awali hakuwa anatoka nje kabisa na kila huduma alikuwa akipewa ndani na siku zote alikuwa ni mtu wa kushinda ndani amefungwa .....kakangu wewe usimwone hivi huyo hapa ukijaribu kumfungulia kamba atazunguka mitaa yote kuingia katika nyumba za watu na kufanya vurugu hadi wenyewe wanampiga na kumchana na viwembe ....kwa usalama wake na kutuepushia aibu tumeona ni vema kumfunga kama ng’ombe wa maziwa hapa katika kamba”

Hata hivyo alisema kuwa kijana huyo amekuwa akifungwa kama na mama yao mzazi kwa maagizo ya baba yao na kuwa zimekwisha fanyika jitihada mbali mbali za kujaribu kumtibu katika hospitali ya mkoa wa Tanga kiasi cha kijana huyo kuanza kupona ila wazazi wake walimkatisha dozi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha kwa maana ya kuwa na nauli ya daladala ya kwenda Hospitali mara kwa mara.

“Hapa unapomwona Hasani ni kama amepona kwani hakuwa hivi alikuwa ni zezeta kabisa ila sasa hivi kutokana na kutibiwa ameanza kupona na kuwa na uelewa hata wa kutambua jambo...”

Habari na Picha na Mdau Francis Godwin
 
View attachment 25640View attachment 25639View attachment 25638

"... wewe kaka acha tu! huyo ni mkorofi sana hivi ukimfungulia kamba hapa anazunguka mitaa yote ya mji wa Tanga na hapo alipo ana majeraha ya kupigwa na kuchanjwa na nyembe kutokana na ukorofi wake hivi tumeaona njia pekee ni kumfunga kamba na kumchunga kama ng'ombe akiwa malishoni japo na usiku akilala tuna mfunga kamba pale anapolala" alisema mwanamke huyo anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 23 na 25

Hata hivyo anasema mbali ya kufungwa kamba pia kwa upande wa chakula wamekuwa wakimwekea katika sahani yake maalum na kula akiwa amefungwa kamba huku kwa wiki ama mwezi huoogeshwa mara moja.

Alisema kuwa sababu za kufungwa na kutengwa na familia ni kutokana na tatizo hilo la utindio wa ubongo linalomkabili na kupelekea hali ambayo ndani ya familia yao wamekuwa wakiona kama ni aibu kwa kijana huyo kutembea mitaani na tatizo hilo.

Pia alikili kuwa kijana huyo amekuwa na uwezo mkubwa wa kutambua japo hajapata bahatika kupelekwa shule na kuwa sehemu kubwa hata kutamka baadhi ya maneno ameanza kujifunza baada ya kuanzishwa kwa utaratibu wa kumfunga kamba nje ya nyumba hiyo na hivyo kubahatika kujifunza kuongea kwa kusikika kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakipita eneo hilo.

"Ujue awali tulikuwa tukimfungia ndani pasipo kutoka nje na jua ameanza kuliona sasa ndani ya miaka mitano hii ila awali hakuwa anatoka nje kabisa na kila huduma alikuwa akipewa ndani na siku zote alikuwa ni mtu wa kushinda ndani amefungwa .....kakangu wewe usimwone hivi huyo hapa ukijaribu kumfungulia kamba atazunguka mitaa yote kuingia katika nyumba za watu na kufanya vurugu hadi wenyewe wanampiga na kumchana na viwembe ....kwa usalama wake na kutuepushia aibu tumeona ni vema kumfunga kama ng'ombe wa maziwa hapa katika kamba"

Hata hivyo alisema kuwa kijana huyo amekuwa akifungwa kama na mama yao mzazi kwa maagizo ya baba yao na kuwa zimekwisha fanyika jitihada mbali mbali za kujaribu kumtibu katika hospitali ya mkoa wa Tanga kiasi cha kijana huyo kuanza kupona ila wazazi wake walimkatisha dozi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha kwa maana ya kuwa na nauli ya daladala ya kwenda Hospitali mara kwa mara.

"Hapa unapomwona Hasani ni kama amepona kwani hakuwa hivi alikuwa ni zezeta kabisa ila sasa hivi kutokana na kutibiwa ameanza kupona na kuwa na uelewa hata wa kutambua jambo..."

Habari na Picha na Mdau Francis Godwin

Hata kama huu ni unyanyasaji kabisa bora asumbue au wampeleke milembe
 
Dah EMT mbona unawasha moto hivyo??
Inasikitisha sana.....
 
Na wale wamama wanaounguza mikono watoto wakiiba je? watu wamekosa utu kabisa. napenda watoto na sipendi kabisa mtu anaenyanyasa watoto
 
Na wale wamama wanaounguza mikono watoto wakiiba je? watu wamekosa utu kabisa. napenda watoto na sipendi kabisa mtu anaenyanyasa watoto

Mashetani wadogoo tu hao!!!
 
Watoto ni zawadi na watoto ni tunu. Watoto ndio mwendelezo wa kizazi kilichopo. Ndio warithi wa kila tunachokifanya au tunachokifanya. Ni wao ambao watarithi wema wetu au uovu wetu. Hivyo maisha ya mtu mzima wa sasa ni lazima yaongozwe kwa kiasi kikubwa na matamanio ya kuwarithisha watoto yaliyio mema na siyo mabovu.

Hivyo, dhamira zinatuita kutunza mazingira, kuwalinda, na kuwasimamia ili waweze kukua katika mazingira ambamo watatambua upendo na siyo chuki, furaha na siyo karaha, huruma na siyo kisasi n.k

Kuna msemo wa Kiswahili kwamba "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo". Msemo huu unabeba saikolojia ya malezi ya mwafrika ya kwamba ukitaka mtoto wako awe mtu mzuri mbeleni ni lazima umlee vizuri; ukitaka mtoto wako awe asiyejali watu mlee pasipo kujali n.k Msemo huu unaendana na saikolojia ya wazungu ambao wao husema kuwa "the abused becomes an abuser". Mtu ambaye alinyanyaswa utotoni, na yeye atajikuta ananyanyasa.

Mtoto ambaye anashuhudia wazazi wake wakigombana kila kukicha na ambaye hashuhudii heshima kati ya wazazi naye atakapokuwa mtu mzima atajikuta anarudia vitendo vile vile vya wazazi wake. Ndio maana utaona kijana wa kiume ambaye ni abusive kwa mke wake ana uwezekano mkubwa kwamba aidha hakuwa na mfano mzuri wa baba au alishuhudia wakati wa utoto baba yake akimnyanyasa mke wake.

Lakini ukiondoa kwenye mambo hayo mtoto anatakiwa akue katika mazingira bora ya kihisia (conducive emotional environment). Huwezi kumlea mtoto bila ya kumbembeleza, kumkumbatia, kumpa pole akiumia au kumuonesha unamjali. Hii si sawa na kumdekeza mtoto; tunaposema mazingira bora ya kihisia maana yake ni pamoja na kumfanya ajisikie ana utu bila ya kumfanya ajisikie ni yeye peke yake ana utu. Hivyo, hata unapomgombeza unatakiwa umgombeze kutoka katika upendo na siyo kutoka katika hasira.

Ndio maana inashauriwa mara nyingi kwamba usimgombeze mtoto wake wakati ukiwa na hasira kwa sababu utasema vitu ambavyo vitaacha majeraha ya kudumu ndani ya hisia na moyo wa mtoto huyo.

Kwa mfano: "We mtoto malaya mkubwa"!
"Mtoto mwizi wewe"
"Najuta kukuzaa"
"Ndio maana uko x,y"

Maneno haya yanaumba. Yanamfanya mtoto awe vile ambavyo mzazi anasema. Kama wewe unamuona mtoto wake ni "malaya" au "mwizi" watu wengine wamuonaje? HIvyo, jambo jingine ni kuonesha uchaguzi mzuri wa maneno unayomuambia mtoto wako.

Lakini nje ya hayo, mtoto anatakiwa ajue mipaka ya maisha. Watoto ambao wanalelewa pasipo kuwekewa mipaka nao hujikuta wanafikiria dunia nzima inazunguka katika nyumba yao na wao ndio kiini cha dunia hiyo. Hivyo, mzazi mzuri siyo yule tu anayempa mtoto wake kila kitu anachotaka bali pia anayejua kuwa kuna vitu ambavyo mtoto wake hatopata hata kama vipo ndani ya uwezo wa mzazi. Kwa mfano, si mzazi ambaye hawezi kumkatalia mtoto wake kitu anamtengenezea mazingira ya kuamini kuwa chochote anachotaka ni lazima apewe au apate. Matokeo yake mtoto huyo akiwa mtu mzima anaweza kutumia mbinu mbalimbali kwa sababu anaamini vyote vilivyopo ni haki yake. Mtoto atakuwa ni mbinafsi kuliko shetani mwenyewe.

Kumbe malezi ya mtoto yanahitaji uwiano mzuri wa nidhamu na mapenzi, kumuonesha jinsi dunia ni zaidi ya familia yake na kumfundisha kujali watu na kujiheshimu yeye mwenyewe. Yote yanawezekana endapo wazazi wenyewe wataonesha malezi bora kwa watoto.

Nje ya hapo, wazazi wanaweza kujikuta wanafanya vitu viovu kabisa dhidi ya watoto wao. Hata hivyo, tatizo bado linabakia kuwa siyo wazazi wote nao walipata malezi mazuri. Kama mwenye mtoto (mama au baba) hakuwahi kupatiwa malezi mazuri au malezi bora ataweza vipi kutoa malezi bora kwa mtoto wake?

Jiulize:
Ni wazazi wangapi huwafukuza watoto "wasiwasumbue" wakati watoto wanataka kucheza na mzazi huyo?
NI wazazi wangapi huwaachia watoto wao mikononi mwa mahouse girl kiasi kwamba watoto wanatengeneza bond "na dada" kuliko na wazazi - ukitaka kupima hili angalia mtoto akilia ni kwa nani anakimbilia kwenda kubembelezwa?
Ni watoto wangapi wakisikia baba karudi nyumbani hukimbia chumbani kwao hadi "waitwe"?
Ni watoto wangapi, baba akiingia ndani tu nyumba nzima inakuwa kimya?
Ni watoto wangapi wakiitwa "sebuleni" huanza kufiria na kutetemeka wakifikiria makosa yao ya siku nzima?

Ukiona unapata majibu yenye mashaka ni lazima ujiulize je una malezi mazuri kwa watoto wako?
 
Asante MMK kwa uchambuzi mzuri!Some limetufikia walengwa!
 
Asante MMK kwa uchambuzi mzuri!Some limetufikia walengwa!

ila naona ni mrefu sana; ningeupunguza kidogo maana wengine wana matatizo ya kusoma maelezo marefu na wengine tuna matatizo ya kuandika kwa ufupi!
 
ila naona ni mrefu sana; ningeupunguza kidogo maana wengine wana matatizo ya kusoma maelezo marefu na wengine tuna matatizo ya kuandika kwa ufupi!

Watu wanaogopa kusoma ila wanataka kujifunza!
 
Back
Top Bottom