Watoza ushuru wa enzi za Biblia

Watoza ushuru wa enzi za Biblia

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Kuna sehemu Yohana aliwahubiria watoza ushuru. Walimuuliza. "Sisi ni watoza ushuru. Unatushauri tufanye nini?" Yohana aliwajibu, "Msitoze zaidi ya kiasi kilichowekwa."

Zamani kulikuwa kuna kitu kinaitwa tax farms(mashamba ya kodi). Tajiri anaifuata serikali ya Roma na kuomba tenda ya kukusanya kodi kwenye eneo fulani.

Serikali inamwambia lipa kiasi kadhaa cash halafu utakusanya kodi labda kwa mwaka, miaka miwili nk. Lakini serikali inakuwa na muongozo wa jinsi kodi inavyopaswa kuwa.

Huyu tajiri akishalipa anaingia hilo eneo na jeshi lake la watoza ushuru kufanya kazi. Walikuwa makatili sana.

Inabidi watoze kadri wawezavyo ili kupata faida. Mara nyingi walitoza hata kiasi kilichozidi kilichopo kwenye muongozo. Wengi ambao walishindwa kulipa kodi waliuzwa utumwani.

Ndiyo kisa cha Yohana kuwaambia wasitoze zaidi ya kiasi kilichowekwa.
 
Na sisi watoza ushuru wa kizazi hiki cha sasa unatushauri tufanye nini ili tusiikose mbingu?
 
Na sisi Graduate unatushauri tufanyeje ili tuupate mkate wetu wa kila siku.
 
Funga kazi alikuwa ni yule jamaa mfupi kama nyundo 'Zakayo mtoza ushuru'

Watu wafupi sijui shida iko wapi! Ni Wakorofi sana.
 
Back
Top Bottom