MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
1. Salim Ahmed Salim - ni mwanadiplomasia mkongwe wa kimataifa aliyewahi kupata nyadhifa mbalimbali kubwa ikiwemo ile ya ukatibu mkuu wa Umoja wa Afrika.
2. Filbert Bayi - ni mwanariadha maarufu au pengine mwanamichezo maarufu zaidi na aliyewahi kuliletea taifa heshima kubwa kuliko wanamichezo wote wa kizazi cha zamani na sasa. Alivunja rekodi ya dunia katika mbio za 1500m huko Jamaica mwanzoni mwa miaka ya 70. Pia ni mwanajeshi mstaafu.
3. Zitto Kabwe - huyu ni mwanasiasa aliyevunja mwiko wwa siasa za nchi hii kuonekana ni kwa ajili ya wazee tu au watu wenye umri mkubwa pale alipofanikiwa kuingia bungeni mwaka 2005 akiwa na umri wa chini ya miaka 30. Baada ya yeye tumeshuhudia vijana wengi wakihamasika na kuleta changamoto kubwa kwenye siasa. Hoja zake zilizowahi kuitetemesha serikali ni jambo jingine linalomfanya awepo kwenye hii orodha tukufu.
4. Diamond Platinumz - kwa sasa ndiye mfalme wa muziki hapa nchini na hana mpinzani yeyote hadi pale Mungu atakapofanya maamuzi mengine ya kutuletea mbadala wake. Tuzo zake ni kitu kinachomtofautisha na wanamuziki wenzake.
5. Jecha Salim Jecha - abarikiwe sana huyu baba kwa kuepusha machafuko huko Zanzibar baada ya kutumia cheo chake cha uenyekiti wa ZEC vizuri kwa kufuta matokeo ambayo mmojawapo wa wagombea alishajitangaza mshindi. Jamii isingenielewa endapo jina lake lisingetokea kwenye orodha hii.
6. Mbwana Samatta - ni mchezaji bora kwa kizazi chake na mwenye jitihada binafsi na nidhamu. huenda akawa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza ligi kuu ya Ufaransa. Mungu amtangulie.
7. Zuwena Mohamed "Shilole" - ni mwanamuziki na mwigizaji nguli zaidi kwa sasa hapa nchini. Anautendea haki muziki wa Tanzania kwa kufanya makubwa. Ikumbukwe huyu mwanadada kabla ya kuwa mwanamuziki alikuwa miongoni mwa wasanii walioiinua sana tasnia ya uigizaji kwa kutoa kazi zenye viwango vya kimataifa. Show zake za USA na Ubelgiji hazitakaa zisahaulike nafsini mwa mashabiki zake waliohudhuria. Orodha hii tukufu isingeweza kukosa jina la malkia huyu wa Bongo flavor
8. Edward Lowassa - ni mwanasiasa mkongwe anaekubalika sana na wananchi. Kwenye orodha hii kaingia kwa sifa mbili kuu alizonazo; uvumilivu & kusamehe.. huyu mzee ni mvumilivu sana baada ya kuvumilia maneno yote mabaya yaliyomwandama kufuatia kashfa ya RICHMOND iliyosababisha ajiuzulu cheo chake cha uwaziri mkuu. uvumilivu mwingine ni baada ya jina lake kukatwa kwenye uteuzi wa mgombea urais wa CCM na pia kushindwa uchaguzi mkuu wa urais. Kusanehe ni sifa nyingine kubwa aliyonayo.
9. Bakhressa - ni mfanyabiashara mkubwa Tanzania anaegusa maisha ya watu ya kila siku kupitia bidhaa zake kama juice, unga, mandazi, maziwa nk. Pia ana sifa ya utoaji (Philanthropist)
10. Nape Nnauye - ni mwanasiasa anaejielewa sana pia msemaji wa chama cha mapinduzi. Kauli zake za busara zimesaidia sana kukijenga chama chetu pendwa na kuchangia ushindi wa Rais Magufuli. Kauli zake nyingi zimekuwa mwiba mkali wenye sumu kwa wapinzani.