RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Watu 12 wameuawa na wengine wanne wamejeruhiwa baada ya watu wanaohisiwa kuwa wa kikundi cha Alshabaab kuvamia nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Bisharo usiku wa kuamkia leo.
Polisi na wanajeshi kwa sasa wanaendelea na msako mkali ili kuwatia nguvuni wahusika.
Taarifa zinasema milipuko mitano ilisikika kabla ya ufyatulianaji wa risasi kutokea.
Eneo lililoshambuliwa huishi sana watu kutoka nje ya mji huo na ambao sio wa jamii ya Wasomali.
Mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika taifa jirani la Somalia.
Chanzo: BBC
Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.
Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.