Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mashirika ya misaada kadhaa ya Umoja wa Mataifa yamesema watu wapatao 160,000 wamo hatarini kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula nchini Yemen.
Ripoti ya mashirika hayo juu ya hali hiyo ya kutisha imetolewa kabla ya mkutano wa wafadhili utakaofanyika hapo kesho. Umoja wa Mataifa umetayarisha mkutano huo kwa ajili ya kuchangisha fedha.
Ripoti ya asasi za Umoja wa Mataifa inatanabahisha juu ya hali mbaya inayoikabili Yemen ambayo imekuwamo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2014 baada ya waasi wa kihouthi wanaoungwa mkono na Iran kuutwaa mji mkuu wa Yemen, Sanaa na sehemu kubwa ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Mfungamano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia uliingia vitani kupambana na waasi hao mnamo mwaka 2015 ili kuisaidia serikali inayotambuliwa kimataifa.