JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Watu 193 wakiwamo watumishi wa afya waliochangamana na wagonjwa wa ugonjwa wa Marburg katika Mkoa wa Kagera wamewekwa karantini kwa ajili ya kufatiliwa maendeleo yao ya kiafya.
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya jitihada zinazoendelea kufanywa na serikali kudhibiti ugonjwa huo, Mganga Mkuu wa serikali hapa nchini Prof. Tumaini Nagu amesema kuwa wanaendelea kufuatilia watu waliochangamana na wagonjwa hao na kwamba kati ya watu hao ambao wamepatikana na kuwekwa karantini, 89 ni watumishi wa afya na 104 ni kutoka kwenye jamii.
Machi 16,2023, Serikali ilitangaza kuzuka kwa ugonjwa huo katika kata za Maruku na Kanyangereko katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba, ambao mpaka sasa umesababisha vifo vya watu watano.
Dalili za ugonjwa huo ni homa kali, kuumwa kichwa, maumivu ya misuri, mwili kuishiwa nguvu, kuharisha, kutapika na kutokwa na damu sehemu za wazi za mwili, hivyo wananchi wametakiwa pindi watakapoona mtu mwenye dalili za namna hiyo wawahi katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Chanzo: EA Radio