Wapalestina wasiopungua 20 wameripotiwa kupoteza maisha siku ya Julai 16,2025, katika kituo cha kugawa misaada cha Gaza Humanitarian Foundation (GHF) kilichopo Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, huku kukiwa na maelezo yanayopingana kuhusu chanzo cha msongamano huo wa umati
GHF, shirika linaloungwa mkono na Marekani na Israel, limedai kuwa msukosuko huo ulichochewa na watu wenye silaha wanaodaiwa kuhusishwa na Hamas, ambapo watu 19 walikanyagwa hadi kufa na mmoja kuchomwa kisu
"Tuna ushahidi wa kuamini kuwa kulikuwa na watu waliopandikizwa katika umati wakiwa na silaha na wakihusishwa na Hamas waliotibua hali kwa makusudi," ilisema GHF katika taarifa yake
Hata hivyo, Wizara ya Afya ya Gaza imetoa maelezo tofauti, ikisema kuwa raia 21 walipoteza maisha, wengi wao kwa kukosa hewa baada ya gesi ya machozi kurushwa, hatua iliyosababisha hofu na kukanyagana kwa umati wa watu waliokuwa wakisaka msaada
"Wananchi 21 wameuawa, wakiwemo 15 waliokufa kwa kukosa hewa kutokana na gesi ya machozi iliyorushwa kwa watu waliokuwa na njaa," ilisema taarifa ya Wizara hiyo, ikielezea tukio hilo kama “mtego wa mauti” katika kituo cha misaada ya Marekani
Shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limesema kuwa ndani ya wiki sita zilizopita, limeorodhesha vifo vya watu wasiopungua 875 karibu na maeneo ya misaada Gaza, vingi vikitokea karibu na vituo vya GHF. Idadi kubwa ya vifo hivyo imetokana na risasi, huku raia wa eneo hilo wakilaumu jeshi la Israel kwa mashambulizi hayo.
Jeshi la Israel limekiri kuwa raia wa Kipalestina wamejeruhiwa au kuuawa karibu na vituo vya misaada, na kuongeza kuwa limebadilisha maelekezo ya kiusalama
====
At least 20 Palestinians were killed on Wednesday at an aid distribution site run by the Gaza Humanitarian Foundation (GHF), in what the U.S.-backed group said was a crowd surge instigated by armed agitators
The Gaza health ministry disputed this explanation, saying tear gas was fired at the crowd, causing panic and a subsequent stampede
The GHF, which is supported by Israel, said 19 people were trampled and one fatally stabbed during the crush at one of its centers in Khan Younis in southern Gaza
"We have credible reason to believe that elements within the crowd – armed and affiliated with Hamas – deliberately fomented the unrest," GHF said in a statement
There has been no immediate comment from Hamas.
Palestinian health officials told Reuters 21 people had died of suffocation at the site. One medic said lots of people had been crammed into a small space and had been crushed
A Gaza health ministry statement said: "Twenty-one citizens were killed, including 15 who died of suffocation as a result of tear gas fired at the starving people and the subsequent stampede at the American aid distribution center (death traps), south of Khan Yunis, since dawn today"
On Tuesday, the U.N. rights office in Geneva said it had recorded at least 875 killings within the past six weeks in the vicinity of aid sites and food convoys in Gaza - the majority of them close to GHF distribution points
Most of those deaths were caused by gunfire that locals have blamed on the Israeli military. The military has acknowledged that Palestinian civilians were harmed near aid distribution centers, saying that Israeli forces had been issued new instructions with "lessons learned"
View attachment 3408044
Source: CGTN