Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikikia watu 23 kwa tuhuma za makosa ya uchochezi, kupanga njama za kufanya vurugu pamoja na uhalifu mwingine katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sabasaba.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 8 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa amesema watuhumiwa hao walikamatwa kati ya Julai 5 na Julai 7, 2026 kupitia operesheni na doria zinazoendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.
DCP Mutafungwa amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili kubaini undani wa tuhuma zinazowakabili na kwamba taratibu zote za kisheria zinaendelea kufuatwa.
"Jeshi la Polisi linaendelea na taratibu za kisheria, ikiwemo mahojiano ya kina na taratibu zitakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linapenda kuwatoa hofu wananchi wote kuwa hali ya usalama ni shwari," amesema.