#COVID19 Watu 29 wameshakufa kwa wimbi la 3 la Coronavirus. Wagonjwa wafikia 858 Tanzania nzima

#COVID19 Watu 29 wameshakufa kwa wimbi la 3 la Coronavirus. Wagonjwa wafikia 858 Tanzania nzima

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima amesema hadi sasa jumla ya watu 29 wamefariki kutokana na wimbi la tatu la Covid-19 huku jana pekee kukiwa na wagonjwa wapya 176.

Idadi hiyo inafikisha Tanzania kuwa na jumla ya wagonjwa 858 wa Covid-19.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dk Dorothy amesema takwimu hizo ni alizopata jana hivyo upo uwezekano vifo zaidi vikawa vimetokea.

Waziri ameeleza kuwa licha ya Serikali kuendelea kusisitiza watu kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo bado wapo wanaozembea.

“Itoshe kuwaambia kuwa ugonjwa upo na watu wanakufa, tusingependa kupeana hizi taarifa za vifo tuchukue tahadhari, kila mmoja wetu ajiulize unapofanya mambo kinyume na kuchukuta tahadhari unalenga kumtesa nani,” amesema Dk Gwajima.

Waziri huyo pia alitupa lawama kwa viongozi wa Serikali ambao hawashiriki kwenye vita vya kupambana na ugonjwa huo.

“Nawakumbusha watu hawa wasiotaka kwenda mstari wa mbele wasichukulie mzaha Uviko 19, ugonjwa huu upo tusijiachie kwa sababu wimbi la kwanza na la pili lilipita,”.

Mwananchi
 
Hii Corona naona inachukuliwa kwa mzaha na wengi, sijui tatizo ni nini, nionavyo wabongo bila kuugua hawaamini kama huu ugonjwa upo, na huko hospitalini oxygen hakuna yakutosha.

Itachukua muda sana Corona kuondoka Tanzania, hizi kauli za Waziri wengi wanaziona kama matamko tu ya kisiasa, naamini ipo siku watu watazitafuta chanjo wenyewe, only a matter of time.
 
mzee alisha mislead watu. na wakaamini.. sasa ku reverse hiyo effect ni ngumu
 
😢😢😢
images.jpeg
 
Madaktari na manesi wapimwe kila wiki wanaweza kuusambaza ugonjwa kutoka kwa wagonjwa kwenda kwa wagonjwa wa magonjwa mengine.
Sio wakingwe kwa kuvaa mavazi maalumu (PPE) wakiwa kazini? Ndio maana siku hizi ukienda hospitali na changamoto ya kupumua wote wanatimka mbio na kukuacha na ndugu zako!
 
Uzembe wa viongozi ndiyo unasababisha yote haya,siasa zikiingia kwenye Mambo mazito hamweleki,punda haendi bila fimbo serikali toeni takwimu kila iitwapo Leo inaweza ikawashitua wananchi.
 
Hii Corona naona inachukuliwa kwa mzaha na wengi, sijui tatizo ni nini, nionavyo wabongo bila kuugua hawaamini kama huu ugonjwa upo, na huko hospitalini oxygen hakuna yakutosha.

Itachukua muda sana Corona kuondoka Tanzania, hizi kauli za Waziri wengi wanaziona kama matamko tu ya kisiasa, naamini ipo siku watu watazitafuta chanjo wenyewe, only a matter of time.

ni ngumu sana covid kua tishio kiasi icho, ukiachana na wale wenye matatizo ya afya kwa ujumla huenda covid ingekua treated kama mafua japokua kwa mbele kuna vifo vya mafua
 
Waziri huyo pia alitupa lawama kwa viongozi wa Serikali ambao hawashiriki kwenye vita vya kupambana na ugonjwa huo.

“Nawakumbusha watu hawa wasiotaka kwenda mstari wa mbele wasichukulie mzaha Uviko 19, ugonjwa huu upo tusijiachie kwa sababu wimbi la kwanza na la pili lilipita,”.

Mwananchi
Kweli Kabisa Gwajima wa Awamu ya Tano alilita mzaha sana kwenye huu ugonjwa wa Uviko..., nina uhakika sasa hivi anajishangaa !!!,

Atleast huyu Gwajima 2.0 yupo Serious (I wonder what changed...)
 
ni ngumu sana covid kua tishio kiasi icho, ukiachana na wale wenye matatizo ya afya kwa ujumla huenda covid ingekua treated kama mafua japokua kwa mbele kuna vifo vya mafua
Umeandika utumbo gani hapa, kwako mafua sio tatizo lakini unakiri yanaweza sababisha vifo mbele ya safari? hayo mafua yanayomnyima mtu oxygen yapo huko kijijini kwenu sio?
 
Zile pesa za tozo tunakubali kukatwa zikanunue mitungi ya gesi tusaidie wa Tanzania wenzetu, lakini sio kujenga magofu....
 
Uongo uongo tu kusudi watu wachanjwe

Kama wamekula pesa za wahisani kwa kisingizio cha corona wajiandae kuzitapika sisi watanzania hatuko tayari kuchanjwa na hao 29 ni uongo mtupu wa kutisha watu.
Mkuu huu ugonjwa upo, mtaani kwangu nimezika wazee kama wa 3...
 
Back
Top Bottom