#COVID19 Watu 29 wameshakufa kwa wimbi la 3 la Coronavirus. Wagonjwa wafikia 858 Tanzania nzima

Waliotajwa humu tu wanazidi 29. Nao wa mtaani ndio wawe 29 tu?
 
Waziri ameeleza kuwa licha ya Serikali kuendelea kusisitiza watu kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo bado wapo wanaozembea.

Ameshasahau kwamba naye alihusika katika kuchochea watu waone C-19 ni kama mafua tu, full kuzindua seasons za nyungu na kunywa hadharani zile 'togwa' za NiMR
 
Hivi data huyu mama sijajua amezopata wapi ? Diwani aliyefariki Leo Kule Kilimanjaro,Moshi manispaa , lecturer wa chuo kikuu Moshi, mtumishi kibo pharmacy Moshi, na weñgine wengi umepewa data hizi? Kilio ni kikubwa angalia data unazozitoa zitakuletea matatizo
 
S
😂😂😂😂😂😂😂😂😂Watanzania mna mambo
e
Serikali ndio wanafanya mzaa kwa afya ya watu wake,kama wamebadilisha mbinu ya tuliyotumia kwenye wimbi la Kwanza na lipili,wakaamua kufuata ya kisasa zaidi, kwanini wasifuate kanuni za kisasa?wapige watu lock down,akuna magulio,akuna mtu kusafiri akuna Mtu kutoka Moshi/kilimanjaro kuja dar-as-salaam, wapige marufuku watu kwenda viwanjani,na kufanya mikutano,makanisa misikiti vyote vifungwe, biashara zote zifungwe,waige wazungu wanavyo fanya,awaoni Rwanda na Uganda pamoja na Kenya wanavyo fanya?wao kila siku maneno lakini atua hawachukui, ccm wanafanya mikutano kila siku, mbona awajapiga marufuku kufanya mikutano yao? serikali ndio inabidi waweke mashariti ya corona,nasi wananchi tutuate.Mwaka jana walipoamashisha nyungu watu wote tulipiga nyungu, mpaka Muhimbili kulijengwa nyungu.
 
Afadhali sasa Utawala uliopo sio ule wa kuzika kichwa mchangani kama Mbuni
 
Kumbe vifo vichache Sana kulinganisha na vifo vya malaria na Mama wajawazito.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sumu aliyoipanda mwendazake juu ya korona bado ipo, mpaka kuwatoka watu itakuwa imetumaliza
 
Mhh
Mhh mbona inarisha kwakweli, umakini unahitajika sasa, nadhani ni mda muafaka kuzuia mikusanyiko kama masokoni kama kariakoo, kwenye masala sala na usafiri wote wa uma tupunguze misongamano, vinginevyo hali itakua mbaya zaidi
 
Uongo uongo tu kusudi watu wachanjwe

Kama wamekula pesa za wahisani kwa kisingizio cha corona wajiandae kuzitapika sisi watanzania hatuko tayari kuchanjwa na hao 29 ni uongo mtupu wa kutisha watu.
Sema siko tayari sio hatuko tayari na nani?
 
Hamasa ya mwendazake ya kupuuzia athari za UVIKO 19 naifananisha sana na ile ya Kinjeketile wakati ule wa Vita vya Maji Maji dhidi ya athari za risasi za moto za mkoloni Mjerumani.

Kweli historia hujirudia; "from Colonial era to Corona era".
 
Sitakuja kumwelewa wala kuelewa maelekezo ya huyu waziri kuhusu corona kamwe labda niwe kilaza

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Huyu bibi anatakiwa afukuzwe na kushitakiwa yeye na Ndugai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…