Watu 367 wamefariki kwa ajali barabarani Oktoba hadi Desemba 2022

Watu 367 wamefariki kwa ajali barabarani Oktoba hadi Desemba 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Fuatilia yanayojiri Bungeni leo Februari 6, 2023 kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 10, Kikao cha 5



VITAMBULISHO VYA NIDA NI ASILIMIA 68 TU
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Vita Rashid Kawawa akisoma Taarifa ya kamati kwa kipindi cha Februari 2022 hadi 2023, amesema:

“Uchambuzi wa kamati kuhusu upatikanaji wa vitambisho vya Taifa hadi kufikia 0ktoba 2022, imebaini Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ilisajili vitambulisho 23,630,813 hadi kufikia Novemba 2022 ikiwa ni sawa na 68% ya lengo la watu 34,080,610 waliokusudiwa kusajiliwa.

“Pamoja na jitihada zinazoendelea idadi ya vitambulisho vinavyozalishwa ni ndogo kuliko mahitaji halisi.”



Ripoti: Watu 367 wamefariki kwa ajali barabarani Oktoba-Desemba 2022
Kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2022 matuko ya ajali za barabarani yaliyosababisha vifo ni 281 ikiwa ni ongeko la makosa 8 sawa na 2.9% ya takwimu kama hizo kwa Mwaka 2021.

Ajali za Mwaka 2022 zimesababisha vifo vya watu 382 wakati Mwaka waliokufa walikuwa ni 367 kwa kipindi kama hicho kwa Mwaka 2021, hivyo kuna ongezeko la watu 15 sawa na 4.1%

Uchambuzi wa kamati umebaini kuwa ajali nyingi zinasababishwa na uhaba wa vitendea kazi kama vile taa za barabarani, speed radar touch, camera na vipima ulevi, baadhi ya wanasiasa kuingilia utekelezaji wa sheria barabarani, ubovu wa barabara, hulka za binadamu kuamini ajali hazizuiliki, madereva wengi wasio na sifa za udereva.
 
Ni mwendawazimu peke yake ndiye anaweza kufuatilia Bunge hili haramu la CCM

 
Haya

Wamjibu Tundu Lisu amesema hakuna Mbunge wa Kuchaguliwa humo Bungeni
 
Back
Top Bottom