Watu 4 wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani

Watu 4 wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani

Watu wanne wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Agosti 19, 2024 wamefiksihwa mahakamani na kusomewa mashktaka mawili.

Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Kanda Dodoma na kusomewa mashtaka ya kubaka kwa kikundi (gang rape) na kumwingilia kinyume na maumbile binti ambaye hakutajwa jina lake mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania mkoani Dodoma, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mashtaka Makao Makuu, Renatus Mkude amesema vijana hao wamekana mashtaka hayo na kutokana na unyeti wa shauri hilo wataendelea kuwa mahabusu.

Watuhumiwa hao waliofikishwa mahakamani ni MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo, Amin Lord Lema, Nickson Idala Jackson na C.1693 Playgod Edwin Mushi

Kwa mujibu wa taarifa ya Renatus Mkude, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka amesema kesi hiyo itasikilizwa kwa siku tano kuanzia leo Agosti 19 hadi Agosti 23 siku ya Ijumaa.

Pia soma:

1. Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa na wanaume watatu

2. Watuhumiwa wa mande ya Ubakaji na ulawiti waliotumwa na afande wakamatwa
Duuu chadema mshasahaulishwa kipigo alichopewa sugu?
 
Kwanini hawataji jina wasije kutuletea mwingine wa kufanana naye kwenye ushahidi ili wavuruge kesi
Mbona ni jambo la kawaida tu kwenye sheria!! Hasa kwenye kesi za udharirishaji, ili kutunza utu wa mhusika!
 
Upo sahihi msomi mwenzangu.

Na ugumu upo kwenye kupeleka original device iliyotumika kurekodi tukio! Yaani ile simu ya kwanza kurekodi:

N.b case imekaa vibaya sana upande wa hawa madogo.

Ninadhani imekaa vibaya upande wa Jamuhuri kwa sababu ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha ushahidi wa video na picha.
 
Duuh... wewe jamaa kwa hizi spana unaonekana unaweza hata kuwa wakili mtetezi wa wale magaidi yaliyofungwa kule Guantanamo Bay na mkashinda kesi.
😄 Kesi ya ugaidi hata ukimpa mwanafunzi wa mwaka wa pili fani ya sheria anaimudu.

Neno gaidi halijawahi kueleweka na ndiyo maana watuhumiwa wanaishia kuwekwa mahabusu tu maana mahakamani pagumu kuwapata na hatia.
 
UShahidi wa video ni mgumu sana aisee,yaani kumfunga mtu ni kipengele ndio maana hata yule afande rama wa zenji alitoboa kwa sababu vipengele ni vingi sana.

Na ninadhani kwenye jicho la sheria hawa jamaa huwenda wakatoboa

Umenikumbusha Afande Rama. Nilitarajia angeachiliwa maana electronic evidence kama ndiyo ushahidi pekee ni ngumu sana kumfunga mtu.

Bado Mahakama zina sita kuukubali maana ni ushahidi manipulative yaani unaweza kuchezewa kirahisi.
 
Huyo nyundo avue jezi yetu.
Askari mfupi ukute wazazi wake ni mabosi halafu wenyewe wanaharibu haribu tu.
 
Kuna muda nikiliangalia hili suala jinsi wabongo walivyolichukulia kwa hisia kali, natamani mahakama itoe hukumu ambayo iko kinyume kabisa na matarajio yao... halafu nione reaction yao itakuwaje, nataka nione je, kwa hizi hasira zao wataingia mabarabarani kwa ajili ya kudai justice kwa huyo binti kweli kama wanavyowafanya wanawake wa India kwa yule daktari aliyebakwa? Au hasira zao zitaishia kwenye kucomment tu huku mitandaoni halafu baada ya hapo watasahau.

NB: hata mimi nimechukizwa sana na hili tukio hasa nikiangalia hawa wahusika kada waliopo inanichukiza zaidi.

Niamini mimi. Hawa jamaa wataachiwa!
 
Afande naye adakwe maana kama ni ushahidi wa maneno na video naye anahusika maana demu alikiri mwenyewe kuwa afande alikula kotekote ikiwemo kuzibua mtaro,
 
Ninadhani imekaa vibaya upande wa Jamuhuri kwa sababu ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha ushahidi wa video na picha.
Video na picha ni moja ya ushahidi, lakini kuna mashahidi wengine akiwemo victim mwenyewe.
 
Video na picha ni moja ya ushahidi, lakini kuna mashahidi wengine akiwemo victim mwenyewe.
Hii kesi imekaa kisengesenge sana wanasheria wenyewe wa Serikali wengi viazi sana ukianzia na yule Mkuu kwa hio kuwafunga hawa manyapara ni mtiti
 
Afande naye adakwe maana kama ni ushahidi wa maneno na video naye anahusika maana demu alikiri mwenyewe kuwa afande alikula kotekote ikiwemo kuzibua mtaro,
Mnavokazania afande mnawapa nafasi hao jamaa bila kujua lazima wataachiwa huru
 
Afande nani mboni mnavuruga Mada?
Hawa ndio wanavuruga mada baada ya kudili na mibakaji ambayo imeonekana wanakalia kudili na afande sababu ni chuki binafsi hivi Kwa akili yao mtu ana cheo kikubwa halafu hajaonekana kwenye video utamfunga Kwa bongo hii aisee wabongo akili 2
 
😄 Kesi ya ugaidi hata ukimpa mwanafunzi wa mwaka wa pili fani ya sheria anaimudu.

Neno gaidi halijawahi kueleweka na ndiyo maana watuhumiwa wanaishia kuwekwa mahabusu tu maana mahakamani pagumu kuwapata na hatia.
Unaona sasa? Hapa tu tayari umeshanionesha Advertise kwamba kesi ya ugaid8 inaweza ikaishia hapo hapo tu kwenye mkanganyiko wa maana ya neno gaidi.... nyie watu bwana
 
Niamini mimi. Hawa jamaa wataachiwa!
Kwa mbali hata mimi naona hilo likitokea, japo sidhani kama wataachiwa katika mazingira rahisi rahisi, lazima watasoteshwa huko rumande kama mwaka mzima, halafu ndio wataachiwa kimya kimya wakati huo wabongo wameshasahau....

Watanzania wako emotional sana, jana nimekaskia kadada flani hivi redioni kwenye kipindi cha diva kanaongea huku kanatoa machozi kakimtaka mama samia asimamie hii kesi hili eti hukumu yao itolewe kihadhara.
 
Ni kweli inaumiza lakini siyo sahihi mkuu wa nchi kuingilia kazi ya Mahakama.
 
Ni kweli inaumiza lakini siyo sahihi mkuu wa nchi kuingilia kazi ya Mahakama.
Ulishawahi kujiuliza ni kwanin wabongo huwa yakitokea mambo mazito kama haya wanakuwa na kimuhe muhe cha kumtaka raisi aingilie kati na yeye ndio atoe maamuzi ilihali vyombo husika vya kushughulika nayo vipo?
 
Back
Top Bottom