Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa Jeshi la Polisi linawashikilia watu 52 kwa kufanya mkusanyiko usio halali jijini humo.
Amesema leo Juni 29 huko maeneo ya Kibo Ubungo Dar es Salaam, jeshi hilo limewakamata watu hao waliokuwa wakisali kanisa la Kiinjili la Afrika Mashariki (KKAM) na baada ya ibada watu hao walitoka na kufanya mkusanyiko huo.
Hata hivyo, picha za video zimeonyesha polisi wa kutuliza ghasia wakipambana na waumini wa kanisa la Glory Of Christ (Ufufuo na Uzima) eneo la Kibo Ubungo, ambao baadaye walihamia kanisa la KKAM.
Waumini hao wamekuwa wakisali pembeni ya barabara eneo hilo tangu kanisa hilo lilipofungwa Juni 2, 2025.