Watu ambao hugombania usafiri wa umma kama wakazi wa Mbagala huishi maisha marefu?

Watu ambao hugombania usafiri wa umma kama wakazi wa Mbagala huishi maisha marefu?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa kwenye gazeti la Washington Post umesema watu ambao hugombania usafiri wana nafasi kubwa ya kuishi maisha marefu na kuepukana na baadhi ya saratani.

Kwa Dar es salaam, wakazi wa mbagala wanajulikana kwa kugombania gari na kupambana kupata nafasi ama kiti cha kukaa kwenye gari.

Hatimae Mbagala mmekumbukwa.
---
MBAGALA RESIDENTS TO LIVE LONGER?

A new study quoted by The Washington Post shows that people who regularly rushed up stairs or hurried to catch a bus were about 30% less likely to die of many types of cancer than people who dawdled

Does this mean that residents of the Mbagala suburb in Tanzania's commercial hub Dar es Salaam, who have become legendary for hustling super hard just to get a seat on a bus, will likely avoid cancer?
 
Ni kweli, swali jepesi tu, kipindi Cha COVID 19 uliwahi kusikia kondakta yeyote wa daladala aliyekufa au kulazwa kwa corona!?, Au raia wa uswahilini kufa hovyohovyo!?, Au mfano mwingine kuku wa kienyeji na wale wanaofugwa Ili wauzwe ndani ya wiki 3 nani mwenye nafasi zaidi ya kukwaa magonjwa hatarishi ya kidunia!?, Logically watu wanaoishi maisha ya kubangaiza wanajikuta wanafanya mazoezi hata bila kuambiwa waende gym, raia wa mbagala kugombania gari asubuhi na jioni au kukosa seat na kusimama kutoka kawe, kariakoo, buguruni, temeke hadi mbagala masaa mawili daily ni zoezi tosha. Hakuna anayependa shida ila wakati mwingine shida zinasaidia watu kuwa ngangari automatically. Mfano wa mwisho watu weusi kutoka bara la Africa tukienda ulaya na US tunaaminiwa sana kwenye nguvu kazi sababu tunaonekana sote tumetoka mbagala na ukweli ni kwamba hata wanaotokea masaki n.k wakifika nchi za wazungu bado wanaonekana wapambanaji ukilinganisha na wazungu. Kesi za cancer na magonjwa kama kisukari, pressure n.k kwa watu wa uswahilini sio nyingi kama hawa wa familia bora.
 
Maisha katika hali ya kawaida,Mara kupata Mara kukosa,Mara uwaze utakula nini, Mara uchemshe ubongo kwa kina,Mara udaiwe kodi ya chumba na hujui utapataje, hii type hujikuta kwenye mazoezi makali ya kimwili na kiakili,hakuna muda wa kurundika Mafuta kwenye miili yao!,"HUISHI MAISHA MARAFU MMO!"
For 24hrs×365days, yupo Gym!😁😁😁
 
Kuna faida gani ya kuishi maisha marefu kama mtu unakaa mbagala..?🤔
 
Ni kweli, swali jepesi tu, kipindi Cha COVID 19 uliwahi kusikia kondakta yeyote wa daladala aliyekufa au kulazwa kwa corona!?, Au raia wa uswahilini kufa hovyohovyo!?,
Kuna methali inasema, "when a beggar die, no star falls" (sijui kama kikristo kimenyooka) but point ni kwamba, hata kama wangekufa mia Moja Kwa siku, hakuna chombo Chochote Cha habari kingeripoti
 
A new study quoted by The Washington Post shows that people who regularly rushed up stairs or hurried to catch a bus were about 30% less likely to die of many types of cancer than people who dawdled
CCM watajivunia Kwa mafanikio haya!
 
SEMA ILE NI AIBU HIVI UMEKOSEKANA KWELI UTARATIBU WA WATU HATA KUPANGA MSTARI VITUONI KUWEZA KUINGIA KWA USTAARABU? KUNA MUDA TUNAONEKANA WAJINGA KWA MAMBO YA KIPUUZI KAMA KUGOMBEA GARI KARNE HII
 
Kuna methali inasema, "when a beggar die, no star falls" (sijui kama kikristo kimenyooka) but point ni kwamba, hata kama wangekufa mia Moja Kwa siku, hakuna chombo Chochote Cha habari kingeripoti
Hii ni uongo!
 
Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa kwenye gazeti la Washington Post umesema watu ambao hugombania usafiri wana nafasi kubwa ya kuishi maisha marefu na kuepukana na baadhi ya saratani.

Kwa Dar es salaam, wakazi wa mbagala wanajulikana kwa kugombania gari na kupambana kupata nafasi ama kiti cha kukaa kwenye gari.

Hatimae Mbagala mmekumbukwa.
---
MBAGALA RESIDENTS TO LIVE LONGER?

A new study quoted by The Washington Post shows that people who regularly rushed up stairs or hurried to catch a bus were about 30% less likely to die of many types of cancer than people who dawdled

Does this mean that residents of the Mbagala suburb in Tanzania's commercial hub Dar es Salaam, who have become legendary for hustling super hard just to get a seat on a bus, will likely avoid cancer?
Kama huna gari hapa mjini aisee utateseka sana, umaskini sio sifa njema.
 
Back
Top Bottom