Ester505
JF-Expert Member
- Jul 14, 2020
- 793
- 1,049
Wametaka wenyewe kukopa.eti kila siku elfu moja.ukizidisha Mara 365 (mwaka)unapata 365000,haya jumlisha na kianzio ulichotoa Ina maana inafika hata laki 5.Jamani hawa watu wanajiita Watu Credit wanaodhamini mikopo mbalimbali ya simu za mikononi, tunaomba Serikali iingilie kati. Wananchi wanaibiwa sana na kuonewa kiuchumi.
Mtu anakopeshwa simu ya Tsh 300,000/= sokoni, analazimika kulipia zaidi ya milioni kwa mwaka, na usipolipia simu yao wanafunga tena wanajibu kwa jeuri sana.
Simu ya laki 3, riba yao haiongeleki. Serikali watusaidie. Ukiwaambia gharama halisi za simu sokoni, wanasema wao hawauzi simu. Tunaibiwa
Mara Mia ninunue kiswaswadu kuliko uzuzu huu