Watu Hubadilika: Waache Waandike Upya Kurasa za Maisha yao

Watu Hubadilika: Waache Waandike Upya Kurasa za Maisha yao

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
“Jamaa ni Profesa? Wapi bwana. Tulisoma naye. Shule alipata three.”
“Mchungaji? Kweli watu wana utani na Mungu. Tuulize sisi tuliocheza nae.”
“Jamaa kawa waziri? Kabebwa hakuna kitu pale. Shuleni alizungusha.”
“Unamwamini huyu jamaa? Mwaka juzi alimtapeli jana yangu.”
“Kaolewa? Namjua. Shuleni alifukuzwa kwa kupata mimba.”

Tunawazuia [sana] watu kubadilika.
Hatuamini mtu anaweza kukutana na mazingira yakamlazimisha kuwa mtu mwingine. Hatumruhusu mtu tunayemjua kuhariri kitabu cha maisha yake. Hatumpi amani ya kuusahau unyonge wake bila usumbufu wa kukumbushwa asiyopenda kuyakumbuka. Tunang’ang’ania historia mbaya tunazozijua kuhusu watu. Tunawanyanyasa na kuwasengenya watu, saa nyingine, kwa kurasa za maisha zilizochochea badiliko tusilojijua. Hata afanye nini bado tunamkumbusha mtu kurasa asizopenda kuzisoma kwa sauti.

Usiamini unawajua sana watu.
Nyakati hupita. Nyakati hubadilika.
Watu hukutana na mengi.
Watu hukua. Watu hujifunza kwa makosa yao.
Watu hufikishwa mahala pa kubadilika.
Hata wasipokuletea taarifa.
Hata wasipojitetea kwako.
Watu huweza kuandika upya kurasa za maisha yao. Kila unapokutana na mtu unayemfahamu usiamini unamjua sana. Muda na matukio hubadisha watu.

Usisubiri mtu asiyependa historia yake mbaya akuondoe kwenye maisha yake. Usisubiri mtu ‘anayehariri kitabu cha maisha yake’ atafute amani kwa kujitenga na wewe. Usisubiri mtu aache kazi ofisini kwako kama mkakati wa kujipa nafasi nyingine ya kurekebisha makosa aliyoyafanya akiwa hapo. Tuwape watu nafasi ya kubadilika kwa sababu ni kweli watu hubadilika na hawatoi taarifa.
 
Ni kweli ila siku zote runatakiwa kujua kuwa kwa namna yoyote utakayoamua kuishi unatengeneza historia, ukiachana na mambo ambayo yapo nje ya uwezo wetu kama hayo ya kupata three ni vema mtu utajitahidi kuishi kwa nidhamu maana historia huwa haifutiki..itakufuata mpaka kaburini bila kujali wakati unakufa ulikuwaje.
 
Back
Top Bottom