Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
WATU HUJA KWAKO KIMKAKATI,MVUTO WAKO KIMUONEKANO NI ZIADA TU.
Wenye upeo mkubwa wa kuona mbali hili si jambo geni wanaelewa kabisa kuwa mvuto ni kitu cha ziada tena pengine kikawa na nafasi ndogo kwenye kufanya watu waje kwako ila mwenye upeo mdogo atajisifia mvuto wake kuwa ni sukari yenye mvuto
Mtu anapokuja kwako awe mwenza kimapenzi ama rafiki kuna mikakati kaona kabisa akiwa kwako itakuwa rahisi yeye kufanikisha hivyo haji kizembe la sivyo labda awe mtu asiye na malengo yoyote yaani awe mtu ambaye hajui anataka nini kwenye hii Dunia.
Unaweza kuona anakupenda sana kwa tafasiri zako za nje ila huo upendo ataonyesha kwingine ikiwa tu akiona kwako humpi urahisi wa kufanikisha mikakati yake na akiondoka utabaki unalia kila siku ila yeye tayari kisha sahau yuko zake na huko anatimiziwa mikakati yake.
Ishi na watu kwa akili kubwa usijiachie sana ukaingia kwenye mfumo wa kutumikishwa na wanaharakati ukihisi ni upendo kumbe wapo kwako KIMKAKATI na yawezekana wakaondoka ikiwa watatimiza lengo au wataona umejanjaruka.
Wanaweza kukugeuza ajira kwa kutumia mgongo wa upendo na bahati mbaya kwako inakuwa hasara.
Ishi na watu ila usiache kuendeleza malengo yako kwa kuwafanyia wao tu na ukiona viashiria vyote kuwa umefanywa HARAKATI usisite kuchukua maamuzi magumu maana hapo jua upo UNATUMIWA TU KISHA UTELEKEZWE .
TANBIHI: Ikiwa anakuja KIMKAKATI ambapo wote mnanufaika huyo ni mzuri kwa mfano kama mtu kaona una kitu ambapo mkiungana naye akileta kitu chake mtafanya makubwa basi hiyo ni mikakati mizuri.
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako