Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Miongoni mwetu kuna wenzetu ambao kutokana na malezi, wanapokuja kupata umaarufu na fedha, wanakuwa kama nusu vichaa au vichaa kamili. Wanapopata umaarufu kidogo au wanapofuma fedha kutokana na juhudi zao au hata kwa wizi na rushwa, wanafumua kile ambacho kilikuwa kimefichwa kwenye malezi yao.
Kuna idadi ya kutosha ya wenzetu ambao kutokana na fedha walizonazo, badala ya kuwa mfano wa binadamu bora na binadamu wa msaada, wanageuka kuwa wadhalilishaji na wapenda sifa, ambao huhangaika huku na huko kutafuta kununua umaarufu rahisi. Huingia kwenye baa hii na ile na kuonyesha kwamba wao ni kina nani, huwanyang'anya wanyonge wake zao, huwafungulia adui zao wasio na kitu kesi za kughushi na hutafuta kila njia ili watajwe na vyombo vya habari bila sababu.
Ni kitu gani huwakabili watu wa aina hii ambao baadhi yetu ni marafiki au jamaa zetu? Hawa ni watu ambao walipata mkengeuko mkubwa wakati wa malezi yao. Ni watu ambao, kwanza wametoka kwenye familia duni au za mzazi mmoja (hasa mwanamke). Lakini ni watu ambao walipokuwa wadogo walionyeshwa kwa kila njia kwamba hakuna wanachokijua na hawawezi chochote.
Unaweza kukuta ni watu ambao walipokuwa wadogo walikuwa wakishukwa na kamasi muda wote na pengine hata kusoma walishindwa. Ni watu ambao utoto wao ulijaa shida, masimango na kejeli nyingi za udhaifu na mashaka ya kutomudu chochote.
Kama tujuavyo malezi yetu na mazingira tuliyokulia hutuathiri sana tuwapo wakubwa. Mawazo yetu ya kina hunakili kila jambo ambalo sisi tumeliona ni muhimu, ambapo jambo hilo huja kutumiwa ukubwani hata kama sisi hatujui. Kwa kuambiwa kwamba, sisi ni watoto wajinga, watoto tusiojua kitu na ambao hatutakuja kuweza kitu maishani, tunakuwa tumejengewa hasira dhidi yetu wenyewe. Tunapokuja kuwa wakubwa na kama tukipata mafanikio tunaweza kuwa kwenye hali au tabia za aina mbili. Tunaweza kuwa ni watu tusiojiamini au kuamini kwamba uwezo tulionao hautadumu.
Muda mwingi tunaweza kuutumia kwa kuhofia kupoteza na kurudi mahali pagumu ambapo patadhihirisha kwamba ni kweli hatujui kitu, kama tulivyofanywa kuamini tukiwa watoto. Tunakuwa ni watu wa mashaka wakati wote na hata mahusiano yetu na wapenzi wetu au wake zetu yanakuwa yamezingirwa na mashaka makubwa.
Ni vigumu kumwambia mtu mwenye mkengeuko huo kwamba, ana athari za kimalezi na akakubali kwa sababu, kwake yeye haoni tatizo lake. Anachokiona yeye ni kutenda yale ambayo anaamini ni haki kuyatenda kwa sababu dunia haimfahamu alivyo. Kwake dunia anayojaribu kuionyesha alivyo ni ile ya utotoni, ingawa mwenyewe hajui.
Ni kwa sababu kama hizi ambapo wazazi tunaambiwa kwamba, badala ya kuwavunja moyo watoto wetu wanapoonyesha udhaifu fulani, tuwape moyo sana. Tunapowaonya na kuwaambia kwamba, ni mabwege, wajinga na kuwaita majina yote mabaya tunayoyafahamu, tunakuwa tunawatengenezea mazingira ya kuja kujihami wakipata fedha ukubwani au umaarufu fulani. Kujihami huku siku zote ni kwa hasara zao.