Camilo Cienfuegos
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 19,380
- 68,484
Leo nimekumbuka utawala wa awamu ya tano chini ya Jemedari hayati John Pombe Magufuli.
Nakuletea watu mashuhuri (Viongozi) waliopendwa sana na hayati Magufuli katika utawala wake.
Orodha hii haiwahusishi viongozi wakuu ambao ni aliyekuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika na Jaji Mkuu.
Orodha hiyo ni kama ifuatavyo;
10. Ngusa Dismas Samike
Huyu alikuwa Mnikulu wa Ikulu. Ni mtu wa nyumbani kwao, Ngusa Samike alikuwa miongoni mwa watu wa karibu sana wa Magufuli na alikubalika sana kwa utendaji wake wa kazi. Alikuwa low key sana.
9. Doto James Mgosha
Huyu ni mpwa wa hayati Magufuli. Alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha. Kwa maana nyingine huyu ndiye alikuwa Mlipaji Mkuu wa Serikali. Alihudumu kwenye wadhifa huo mpaka pale Rais Magufuli alipofariki.
Hakuwa mtu wa show off ila ni miongoni mwa watu walioaminiwa sana na hayati Magufuli.
8. Mrisho Mashaka Gambo
Katika awamu ya tano huyu jamaa aliinuliwa kutoka Ukuu wa Wilaya mpaka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kama haitoshi mwaka 2020 akateuliwa na CC ya CCM chini ya Rais Magufuli kugombea ubunge wa Arusha Mjini. Alipendwa na akaaminika na hayati Magufuli.
Bahati mbaya hakujua kuchanga karata zake vizuri baada ya kifo cha Magufuli. Kwasasa yupo nje ya mfumo.
7. Diwani Athumani Msuya
Huyu ni kutoka kule kwa jamaa zetu. Ni katika awamu ya 5 tuliona namna ambavyo jamaa alikuwa bosi katika taasisi nyeti za nchi.
Alikuwa bosi wa TAKUKURU na baadae TISS. Hiyo ni ishara tosha kuwa aliaminika na kupendwa.
6. Medard Matogolo Kalemani
Mtoto wa nyumbani, mrithi wa jimbo la Chato mpaka Waziri wa Nishati, akawa kiongozi mwandamizi katika Serikali ya awamu ya 5.
Kitaaluma akiwa ni mwanasheria msomi ila akapewa Wizara ya Nishati kuanzia mwaka 2017. Ni katika zama zake biashara ya jenereta ilikufa kifo cha mende kwani umeme ulikuwa unapatikana vizuri.
Hakuwahi kutumbuliwa wala kuhamishwa wizara katika utawala wa awamu ya 5.
5. Paul Christian Makonda
Kila mmoja anajua namna Makonda alivyokuwa anakubalika na hayati Magufuli.
Pengine alitajwa kama Mkuu wa Mkoa aliyekuwa na ushawishi na mamlaka kubwa kuliko wenzake.
Alikingiwa kifua licha ya maneno mengi sana kutoka kwa wakosoaji wake kuhusiana na elimu yake.
Aliaminika mpaka pale alipojaribu kugombea ubunge wa Kigamboni ndipo alipotemwa serikalini.
4. Jenerali Venance Salvatory Mabeyo
Moja ya teuzi bora kabisa zilizowahi kufanywa na hayati Magufuli enzi za uhai wake akiwa Rais basi ni kumteua Mabeyo kuwa CDF.
Mnyenyekevu, jasiri, shupavu kabisa na pengine uimara wake utakumbukwaa zaidi wakati wa msiba wa Magufuli namna alivyosimamia katiba ifuatwe.
3. Meja Jenerali Charles Mbuge
Miongoni mwa nyota zilizong’ara awamu ya tano basi huwezi kusahau kutaja jina la Meja Jenerali Mbuge.
Kutoka kwenye ujenzi wa ukuta wa mererani mpaka ujenzi wa Ikulu ya Dodoma.
Alipanda vyeo kwa haraka sana ndani ya muda mfupi, hali iliyowafanya wakubwa huko jeshi i kuhofia nafasi zao.
Kutoka Kanali mpaka Mejaa Jenerali ndani ya muda mfupi sana.
Wengi walishuku Meja Jenerali Mbuge alikuwa anaandaliwa kuwa Mkuu wa Majeshi.
Bahati mbaya haikuwa hivyo mara baada ya kifo cha ghafla cha hayati Magufuli.
2. Injinia Patrick Aron Mfugale
Huyu alikuwa ni bosi pale TANROADS.
Komredi wa siku nyingi sana wa hayati Magufuli tangu akiwa Waziri kabla ya Urais.
Magufuli alisifiwa kwa ujenzi wa barabara alipokuwa Waziri wa Ujenzi ila nyuma yake alikuwepo Mfugale. Walishibana sana.
Huyu alikuwa “untouchable” hata pale umri wa kustaafu ulipofika bado aliongezewa muda wa kuhudumu serikalini mpaka mauti yalipomkuta.
Kivuko cha magari cha juu pale TAZARA kimepewa jina kwa heshima yake.
Vilevile jengo la kupokelea abiria katika uwanja wa ndege wa Chato limepewa jina kwa heshima yake.
1. Injinia John William Kijazi
Alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi katika Serikali ya awamu ya 5.
Rafiki mtiifu kabisa wa hayati John Pombe Magufuli tangu walipokuwa Wizara ya Ujenzi. Magufuli akiwa Waziri, Kijazi akiwa Katibu Mkuu.
Hata Magufuli alipokuwa anahamishwa wizara alikuwa anaomba kwa Rais wahamishwe wote.
Magufuli, Kijazi na Mfugale waliunda utatu mtakatifu Wizara ya Ujenzi mpaka kwenye Urais wa Magufuli.
Na hata vifo vyao wote watatu vilitokea mwaka 2021.
Kijazi anatajwa kama kiongozi shupavu aliyekuwa na mamlaka ya kusikilizwa na kuzingatiwa na Rais Magufuli.
Iliwahi kusemwa sehemu, ni John Kijazi akiwa Katibu Mkuu Kiongozi, alimuombea msamaha Kassim Majaliwa, asitimuliwe kwenye Uwaziri Mkuu baada ya Wabunge wengi wa kusini kuongoza mgomo wa Korosho hali ilyosababisha Magufuli kutishia kuwapiga shangazi zake Majaliwa.
Kifo cha ghafla cha John Kijazi kilimnyong’onyesha sana JPM na yeye hakuchukua mwezi akaja kufariki.
Kivuko cha juu cha magari Ubungo kimepewa jina kwa heshima yake.