Watu milioni 14 wako hatarini baada ya Trump kukata misaada - ripoti

Watu milioni 14 wako hatarini baada ya Trump kukata misaada - ripoti

Hadi vichaa wamechukua fomu kugombea ubunge....hiyo pesa wanatoa wapi? Ngoja tubanwe ili tujue kujibana pia
 
Ashikilie hapo hapo sisi uchumi wetu mkubwa na mama kagawa mikangafu ya kutosha ili tudondoke na chanjo ya tetenasi hatuna..!! 😹😹
 
Kimbuka Kuna wasiojiweza wanahitaji msaada mkuu binadamu hatulingani!

Cc Smart911
Naelewa hilo mkuu lakini yule sio rais wa Africa, yule ni rais wa USA. Ieleweke hivo. Wewe huoni viongozi wa Africa wanavyo ishi maisha ya anasa? How msafara wao unakua na magari zaidi ya 60 for what? Tujifunze kubana matumizi, tunaweza kuwalea watu wetu sisi wenyewe bila kutegemea mataifa mengine. Tunayo sababu hata 1 ya kua na wabunge 400? Tunayo sababu ya kua na mikoa yote hi tulionayo? We have a lot to do, maisha ni uchaguzi
 
Kwani lazima marekani si urusi,China,Korea kaskazini mnasema wako vizuri zaidi wataziba magepu.
 
Hatua ya Donald Trump kupunguza kiwango kikubwa cha ufadhili wa Marekani kuelekea misaada ya kibinadamu ya kigeni inaweza kusababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 14 ifikapo mwaka 2030, kulingana na utafiti uliochapishwa katika jarida la matibabu la The Lancet.
Theluthi moja ya wale walio katika hatari ya kukabiliwa na vifo vya mapema ni watoto, utafiti umebaini.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema mwezi Machi kwamba utawala wa Rais Trump ulifuta zaidi ya asilimia 80 ya programu zote katika Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani, USAID.
"Kwa nchi nyingi za kipato cha chini na wastani, mshtuko unaosababishwa unaweza kulinganishwa kwa kiwango na janga la kimataifa au mzozo mkubwa wa silaha," Davide Rasella, ambaye aliandika ripoti ya Lancet, alisema katika taarifa.
Kusishwa ghafla kwa ufadhili huo "kunatishia kurudisha nyuma''- hatua zilizopigwa miongo miwili iliyopota katika juhudi za kuimarisha afya miongoni mwa watu walio katika hatari," aliongeza Rasella, mtafiti katika Taasisi ya Barcelona ya Afya Ulimwenguni.
Ripoti hiyo inakuja wakati makumi ya viongozi wa dunia wanakutana katika mji wa Seville nchini Uhispania wiki hii kwa mkutano wa misaada unaoongozwa na Umoja wa Mataifa.
Watafiti hao wa walichambua data kutoka mataifa 133, kukadiria kuwa ufadhili wa USAID ulikuwa umezuia vifo milioni 91 katika nchi zinazoendelea kati ya 2001 na 2021.
Nchi za Kiafrika inabidi zijipange sasa, hatuwezi kuwa tegenezi kila siku kwa vitu ambavyo sis wenyewe tunaweza kuyamudu wenyewe. This is the time.
 
Uyu mzee mbinafsi sana
Trump alichaguliwa na wamarekani kwa ajili ya Marekani kama ambavyo Xi ni kwa ajli ya China, etc. Vitokeapo vimaokoto ni hisani tu sio lazima.
 
Back
Top Bottom