Kilimo cha kufa na kupona hakiwezi kutuokoa. Hata ukiangalia kilimo cha chakula Tanzania, bado ni kilimo primitive sana. Iwe na mahindi, mchele au ndizi; bado ni kilimo cha kujitosheleza kwa chakula, na kuuza kinachobaki; sio cha biashara. Tafuta mtu anayefanya hizo biashara, utashangaa. Kazi ya kutafuta mpunga au mahindi ni ngumu sana. Unakuta mkulima mmoja ana magunia 8, mwingine 10; vurugu tupu. Hata ndizi ni hivyo hivyo, mkulima mmoja anatoa mikungu 4 mwingine 2, mpaka mfanyabiashara ajaze lori la mikungu 400 ni kazi sana.
Sasa unategemea wakulima wa aina hiyo wataweza kufanya kilimo cha mafuta ambayo hata kula hawawezi! Mkulima ana shamba la eka 10, apande mawese halafu atakula nini?
Wenzetu wameweza kufanya commercial farming, na wana back up kubwa sana ya serikali, kupitia ruzuku mbalimbali na guarantee ya bei. Tatizo hapa tukijaribu hizo mambo, utatokea upigaji sio wa dunia hii.