Watu milioni 60 kinachotushinda ku-solve tatizo la mafuta ya kula ni nini?

Watu milioni 60 kinachotushinda ku-solve tatizo la mafuta ya kula ni nini?

Mr Chromium

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2020
Posts
2,761
Reaction score
3,835
Nchi ina ardhi yenye rutuba?
Rasilimali watu?
wasomi?
Zao la arizeti linakubali?
Mawese yanakubali?
Nazi zinakubali?
Karanga zinakubali?
Ufuta nao unakubali?
Haya n mafuta ya mimea bas kama hayo tumeshindwa yako wap mafuta ya samaki,wanyama nk

Ukiacha hilo kwene sukar ivo ivo.
Hii nchi nayo, basi hata tuigilizie wenzetu

IMG_0179.jpg

IMG_0179.jpg
 
Nadhani sio sahihi kuongea kwa mtazamo wa watu mil 60.

80/20 rule inatutaka kuwa watu wachache wanaweza kufanya jambo ambalo linaweza kusaidia wengi.

Ndio maana tukawa na viongozi wanaotupa dira. Tuwe na Dira ya kutatua changamoto za kitaifa za kwa kudumu. Bado nchi yetu uelewa wetu uko chini sana ili tupige hatua, kama Singapore tunahitaji Brilliant Dictator na team yake yenye nia njema na taifa. Kitu kama Klemlin yenye maono ya kitaifa. Aliyepita alijitahidi ila alikuwa hana watu wanaoaminiana kufikia lengo. Na nia ilionekana kuwa kubwa kuliko uwezo wa kutatua changamoto zetu.

Bado tunahitaji a Better version ya JPM, Mama Yetu wanafanya vzr, ila baada yake arudi tena mbabe mwingine lakini awe bora kuliko aliyepita.
 
tuna subiri CCM itoke madarakani na katiba mpya ilete mafuta ya kula
 
Uelewe, "Ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi"

Siasa chafu na uongozi mbovu ndio vimetufikisha hapa.
siasa chafu na uongozi mbovu ndio zinawapa ulaji wageni wenye mashamba makubwa na mahoteli ya pesa nyingi pamoja na makampuni makubwa ya huduma mbalimbali...

ktk taifa la ujerumani kuna sheria moja nzuri sana, wana kwambia ukiingia barabara kuu hakikisha gari yako nzima na ina mafuta ya kutosha... ukipata tatizo lolote na kupelekea kusimamisha gari, iwe kuishiwa mafuta au vyovyote, utakutwa na adhabu...

sharia hizi hazifai kwetu... masikini wanatakiwa kuishi kimasikini na wawe na mawazo ya kimasikini... ili wapate mtu wa kumpa lawama
 
Kuna watu wanna 10% zao kwa hao mapapa wa kuleta mafuta na hao wa sukari kwahio ili kuweza hio vita fanya chini kwa chini usijitokeze pablic
 
Nadhani sio sahihi kuongea kwa mtazamo wa watu mil 60.

80/20 rule inatutaka kuwa watu wachache wanaweza kufanya jambo ambalo linaweza kusaidia wengi.

Ndio maana tukawa na viongozi wanaotupa dira. Tuwe na Dira ya kutatua changamoto za kitaifa za kwa kudumu. Bado nchi yetu uelewa wetu uko chini sana ili tupige hatua, kama Singapore tunahitaji Brilliant Dictator na team yake yenye nia njema na taifa. Kitu kama Klemlin yenye maono ya kitaifa. Aliyepita alijitahidi ila alikuwa hana watu wanaoaminiana kufikia lengo. Na nia ilionekana kuwa kubwa kuliko uwezo wa kutatua changamoto zetu.

Bado tunahitaji a Better version ya JPM, Mama Yetu wanafanya vzr, ila baada yake arudi tena mbabe mwingine lakini awe bora kuliko aliyepita.
Kwa viongozi hawa hawa wenye akili ndogo ama unaongelea wapi?
 
Tuanze kulima,Mimi mwaka huu naenda kulima Kongwa alizeti eka 20,nitatumia mbegu hybrid,nitakamua na kuuza mwenyewe.

Bila mkakati wa serikali Nchi bado haiwezi kujitosheleza
 
Sasa kama uagizaji wa Mafuta ya kula kutoka nje, na uzalishaji wa mafuta ndani ya nchi, unafanywa na wenzetu wenye asili ya kiasia, bila hata Serikali kuwaingilia, unategemea bei weli zipungue hapo? Tena ni makampuni machache yenye huo U-Monopoly. Tutaendelea tu kuumia, tena sana. Labda wazawa wenyewe tuje na viwanda vyetu; kama kweli tutaweza.
 
Kilimo cha kufa na kupona hakiwezi kutuokoa. Hata ukiangalia kilimo cha chakula Tanzania, bado ni kilimo primitive sana. Iwe na mahindi, mchele au ndizi; bado ni kilimo cha kujitosheleza kwa chakula, na kuuza kinachobaki; sio cha biashara. Tafuta mtu anayefanya hizo biashara, utashangaa. Kazi ya kutafuta mpunga au mahindi ni ngumu sana. Unakuta mkulima mmoja ana magunia 8, mwingine 10; vurugu tupu. Hata ndizi ni hivyo hivyo, mkulima mmoja anatoa mikungu 4 mwingine 2, mpaka mfanyabiashara ajaze lori la mikungu 400 ni kazi sana.

Sasa unategemea wakulima wa aina hiyo wataweza kufanya kilimo cha mafuta ambayo hata kula hawawezi! Mkulima ana shamba la eka 10, apande mawese halafu atakula nini?

Wenzetu wameweza kufanya commercial farming, na wana back up kubwa sana ya serikali, kupitia ruzuku mbalimbali na guarantee ya bei. Tatizo hapa tukijaribu hizo mambo, utatokea upigaji sio wa dunia hii.
 
Back
Top Bottom