Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Huku kwetu Kwamtogole mayai na maziwa ni vyakula vya mgonjwa. Hata wale wenye magonjwa sugu wanaamini wakinywa maziwa yanapunguza nguvu ya dawa. Maziwa yananunuliwa haraka inapobainika mtu amekunywa sumu.
Matunda ni starehe hasa kwa kipato cha wengi. Baba akifanikiwa kupata robo au nusu kilo ya sukari na maandazi anakua amemaliza asubuhi. Mchana kilo ya unga ikipatikana basi kama familia ni kubwa itapata na nusu kilo ya maharage. Matunda ni majaliwa.
Bahati nzuri mboga za majani zinalika sana, hii ni kutokana na unafuu wake kulinganisha na samaki na nyama. Hii imepelekea kuwa na soko kubwa la mboga za majani. Kuna watu wanaendesha familia kwa kuuza mboga za majani. Hata wenye usafiri mzuri wanatoa mboga za majani Iringa jioni na zinauzwa Dar es Salaam na Dodoma asubuhi.
Kama watu wangeongeza matumizi ya maziwa na mayai na hata matunda uzalishaji ungeongezeka na hata middle men wangerahisisha upatikanaji kutoka kwa wazalishaji mpaka kwa walaji. Wauzaji wengine wa maziwa wanaweka maji ili kuongeza faida. Kama wazalishaji wakiongezrka hawa wauzaji wa maziwa yenye maji watakosa soko.