Watu milioni 60 ni idadi kubwa kwa soko la ndani la bidhaa zinazohitajika kila siku mfano maziwa, mayai, matunda na mbogamboga

Watu milioni 60 ni idadi kubwa kwa soko la ndani la bidhaa zinazohitajika kila siku mfano maziwa, mayai, matunda na mbogamboga

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Huku kwetu Kwamtogole mayai na maziwa ni vyakula vya mgonjwa. Hata wale wenye magonjwa sugu wanaamini wakinywa maziwa yanapunguza nguvu ya dawa. Maziwa yananunuliwa haraka inapobainika mtu amekunywa sumu.

Matunda ni starehe hasa kwa kipato cha wengi. Baba akifanikiwa kupata robo au nusu kilo ya sukari na maandazi anakua amemaliza asubuhi. Mchana kilo ya unga ikipatikana basi kama familia ni kubwa itapata na nusu kilo ya maharage. Matunda ni majaliwa.

Bahati nzuri mboga za majani zinalika sana, hii ni kutokana na unafuu wake kulinganisha na samaki na nyama. Hii imepelekea kuwa na soko kubwa la mboga za majani. Kuna watu wanaendesha familia kwa kuuza mboga za majani. Hata wenye usafiri mzuri wanatoa mboga za majani Iringa jioni na zinauzwa Dar es Salaam na Dodoma asubuhi.

Kama watu wangeongeza matumizi ya maziwa na mayai na hata matunda uzalishaji ungeongezeka na hata middle men wangerahisisha upatikanaji kutoka kwa wazalishaji mpaka kwa walaji. Wauzaji wengine wa maziwa wanaweka maji ili kuongeza faida. Kama wazalishaji wakiongezrka hawa wauzaji wa maziwa yenye maji watakosa soko.
 
Mayai, matunda, maziwa ni anasa.

Mboga za majani ndo mboga kamili kwa familia za kawaida za Ki Tanzania

Laiti Mheshimiwa angeyaona maisha ya wa Tanzania wa kawaida wasavyosulubika pengine angesema neno. After educating vijana no employment tupo nao wanatutegemea, what a life.

Sensa ni muhimu ila kwa watu wenye njaa hao wauliza maswali watakuwa na wakati mgumu.
 
Na itakuwa hivyo ikiwa tuu serikali itahakikisha inawapa purchasing power..

Pia behavior consumer lazima ibadilike maana hapa Tanzania mtu hata akipata hela kidogo anawaza kujenga..

Nimesikia Raia Samia akisema sasa wanabadili utaratibu wa kukuza Uchumi,utoke Chini kwenda juu na sio juu kuja chini ambayo haileti tija Sana.
 
Umesahau bongo watu wanakula kuku kila siku..hasa vichwa vya kuku..miguu na utumbo.

Bila kusahau mihogo..hivi ndio vyakula pendwa na vinavyolika sana miongoni mwa wananchi wa bongo Dsm.

#MaendeleoHayanaChama
 
Siyo kwamba watu hawafahamu umuhimu wa maziwa na mayai katika miili yetu Bali ugumu wa maisha unasababisha watu waipende mboga ya majani na hasa chainizi.

Uwezo wa viongozi wetu kupambana na changamoto zinazoikumba nchi na wananchi umekuwa mdogo Sana,imefika mahala ili uwe kiongozi Ni lazima upitie kwenye UCHAWA.
 
Majuzi Mhe rais akiwa ziarani Iringa nilisikia waziri Ummy akisema watoto wenye udumavu kutokana na lishe duni ni 47% yaani karibia nusu ya watoto.. Na hii yote inatokana na lishe duni..
 
Kila mtu akila pears moja kwa siku msimu wa ma pears, yale ma pears ya Lushoto hayatatosha na itabidi miti mingi ipandwe kukidhi soko.
 
Majuzi Mhe rais akiwa ziarani Iringa nilisikia waziri Ummy akisema watoto wenye udumavu kutokana na lishe duni ni 47% yaani karibia nusu ya watoto.. Na hii yote inatokana na lishe duni..
Hii 47% ni kwa Tanzania nzima au kwa Iringa tu?
 
Milioni 60 wakati watu wenye nguvu ya manunuzi sina hakika kama wanafika milioni 10 ukijumuisha na wale wa kuunga unga
 
Milioni 60 wakati watu wenye nguvu ya manunuzi sina hakika kama wanafika milioni 10 ukijumuisha na wale wa kuunga unga
Bongo msosi wenyewe hasa kwa vijana ambao unemployment ni wa kuunga unga na vijana wanachukua idadi kubwa pia ya population ya watu
Umepita kwa mwana umekula ugali na utumbo wa kuku
Jion geto unapasha kiporo cha wali na chai hakuna cha balance diet hapo

Kesho asubuhi unaamka asubuhi kusaka vibarua
 
Milioni 60 wakati watu wenye nguvu ya manunuzi sina hakika kama wanafika milioni 10 ukijumuisha na wale wa kuunga unga
Kama hawa milioni 10 wakinunua litre moja ya maziwa kila siku ina maana ni litre milioni 10 kwa siku.
 
CCM haina maono Wala dira kitu pekee wanacho weza fanya hata kuondoa uhai wa watu ni wao kutumia njia yoyote kubaki madaraka.

Prof Mussa kasha wahi sema "60% ya viongozi waliopo serikalini Wana uwezo mdogo" mfano mosi ni mkuu wa kampuni mwenyewe ana deal na vitu ambavyo hata mtoto wa darasa la Saba anashangaa ni aibu mkuu wa kampuni kulalamika kwamba waandishi hawapigi picha vizuri za kuonesha watu kwenye mikutano yake.
 
Umesahau bongo watu wanakula kuku kila siku..hasa vichwa vya kuku..miguu na utumbo.

Bila kusahau mihogo..hivi ndio vyakula pendwa na vinavyolika sana miongoni mwa wananchi wa bongo Dsm.

#MaendeleoHayanaChama
Hivi tukae tujivunie kuwa tuna taifa linalokula vichwa na utumbo wa kuku kweli!
 
Mada nzuri kweli kama ingefanyiwa utafiti wa kutosha! Hata kwa hali iliyopo unavuna mazao mkoa mfano pears au machungwa au una mbuzi wengi wa kuuza lakini mwananchi hajui soko liko wapi! Una mayai yako unatakiwa ujue soko liko Mbeya au Dodoma na ukipeleka ukute wateja wa kutosha uuze ugeuze.
Nilitegemea vijana wa Tehama wangejipatia kazi kwa kubuni program nyepesi za kuonyesha sehemu ipi izalishe nini na ukishazalisha ukauze wapi. Hii iwe ni shughuli ya kila siku na hata aina ya usafiri waeleze: treni, basi, lori, ndege au meli.
 
Kwa kweli, "hili nalo mkalifanyie kazi"_SSH
 
Back
Top Bottom