Watu milioni mbili duniani wanaishi na Ugonjwa wa Fistula

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Rashid Mfaume amesema ugonjwa wa fistula ya uzazi bado ni tatizo nchini na kwamba zaidi ya watu milioni mbili duniani wanaishi na ugonjwa huo.

Amesema hayo kuelekea Siku ya Fistula Duniania Mei 23, ambapo mbali na idadi hiyo pia kuna visa takribani laki moja vilivyoripotiwa duniani kuwa na ugonjwa huo.

Dk. Mfaume aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza ya Fistula. Maadhimisho hayo yalifanyika Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam, kwamba ali kuwa mgeni rasmi alkimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala.

Kutokana na tatizo hilo, Dk. Mfaume alisema elimu inapaswa kuendelea kutolewa na kwamba ugonjwa huo umekuwa ukiwatesa watu ambao wamekuwa wakichelewa kupata matibabu.

Aliipongeza Hospitali ya CCBRT kwa kutoa matibabu bure kwa wagonjwa wa fistula ikiwamo kuwapatia chakula na nauli za kuwatoa mikoani na kuwaleta katika hospitali yao ili wapate matibabu.

Mkurugenzi Mtendaji wa CCBRT, Brenda Msangi, alisema ugonjwa wa fistula unatibika, hivyo jamii inapokuwa na wagonjwa hao wawapeleke hospitalini kupata matibabu.

Alisema kesho Tanzania itaungana na huungana na nchi zingine duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza fistula ya uzazi.

“Huu ni mwaka wa 10 tangu tulipoanza kuungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku hii mwaka 2013," alisema.

Msangi alisema kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni: "Tokomeza Fistula, Wekeza, Imarisha Huduma za Afya na Wezesha Jamii'.

Aliongeza kuwa kaulimbiu hiyo inamaanisha kuwekeza na kuimarisha huduma za afya.

Amesema huwahudumia watu enye ulemavu, mabinti wanaopata mimba za utotoni, lengo ni kuzuia fistula mpya pamoja na kuondoa vifo vya mama na mtoto.

Ameongeza kuwa tangu mwaka 2003 walipoanzisha kampeni kupambana na fistula, zaidi ya wanawake 17,500 wamepatiwa matibabu.


Chanzo: Nipashe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…