Watu mliopo serikalini ifikie hatua muwahurumie walipa kodi

Watu mliopo serikalini ifikie hatua muwahurumie walipa kodi

Joshua Mbezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
1,994
Reaction score
4,446
Kijiografia nchi yetu ni kubwa sana na ukubwa huu unapelekea kuongezeka kwa gharama za maisha hasa kwa watumishi wa Umma

Ofisi ya Rais Utumishi mnachofanya sio kizuri ni kuongeza gharama zisizo kuwa na maana kabisa kwa wananchi wote tunajua mtumishi yupo kwa ajiri ya kuwahudumia watanzania wote lakini hili suala inabidi liangaliwe upya

Hivi Inakuwaje umtoe mtu Kagera kule Kyerwa umpangie kituo Cha kazi huko Tandahimba Mtwara ? Au mwingne unamtoa Dar es Salaam kule Mabwepande umpeleke kyerwa kule Murongo kabisa kule mpakani mwa Tanzania na Uganda? Mwingne unamtoa Tarakea Kilamanjaro unampeleka Tunduma kule mpakani na Zambia

Halafu unamwekea masharti ya kwamba haruhusiwi kuhama kituo Cha kazi Hadi amalize miaka minne hii yote inaenda kuongeza gharama kwa wananchi kwenye malipo ya nauri kwa mtumishi husika ikitokea mtumishi husika akiwa na familia ya watoto wanne na mke hela anayolipwa kwa ajili ya nauli inatosha kabisa kumlipa mtumishi mpya kwa miezi miwili. Sasa piga hesabu wapo watumishi wangapi nchini wenye changamoto kama hii?

Kwahiyo tunajikuta tunapoteza hela nyingi kwenye vitu vya kawaida kabisa

Nafikiri serikali ije Mpango mkakati wa kwamba watu wafanye kazi kwenye Kanda zao mfano mtu wa Kanda ya Nyanda za juu kusini anaweza kufanya kazi kwenye mikoa ya iringa, njombe,mbeya, songwe, nk

Kanda ya ziwa mtu afanye kazi kwenye mikoa ya Kagera, geita ,mwanza, shinyanga, simiyu na Mara .

Hii itasaidia kupunguza gharama nyingi zinazotumika katika ulipaji wa hela ya nauri kwa watumishi lakini pia itapunguza changamoto ya kuhama hama hovyo kwasababu watu watakuwa karibu na familia zao na itaimalisha taasisi ya familia kwasababu wanandoa watakuwa karibu zaidi hivyo itasaidia katka kuboresha malezi ya watoto wao.
 
Wewe wamekupangia wapi mkuu?
Me nilipangiwa mwanza wilaya ya ukerewe halafu ndani huko ikara wanakuita,halafu mshahara wenyewe TGS nikarefuse post....
huu mwaka wa 8 toka nikatae ajira za kikandamizi bora nibaki NONDE-SUA nilime mpunga au ufuta tu.
 
Nafikiri serikali ije Mpango mkakati wa kwamba watu wafanye kazi kwenye Kanda zao mfano mtu wa Kanda ya Nyanda za juu kusini anaweza kufanya kazi kwenye mikoa ya iringa, njombe,mbeya, songwe, nk
Huu mkakati wako hauna Tija! Moja ya hoja za mwalimu kutuchaganya hivyo ilikuwa kuimarisha uzalendo miongoni mwa raia. Sasa wewe ufanye kazi ulikozaliwa si ndio mwanzo wa kuanzisha ukabila hapo
 
Huu mkakati wako hauna Tija! Moja ya hoja za mwalimu kutuchaganya hivyo ilikuwa kuimarisha uzalendo miongoni mwa raia. Sasa wewe ufanye kazi ulikozaliwa si ndio mwanzo wa kuanzisha ukabila hapo
Sijasema ufanye kazi ulikozaliwa rudia kusoma post

Sawa
 
Wewe wamekupangia wapi mkuu?
Me nilipangiwa mwanza wilaya ya ukerewe halafu ndani huko ikara wanakuita,halafu mshahara wenyewe TGS nikarefuse post....
huu mwaka wa 8 toka nikatae ajira za kikandamizi bora nibaki NONDE-SUA nilime mpunga au ufuta tu.
Sio Mimi Mkuu aliyepelekwa huko n mchepuko wangu katolewa geita kapangwa huko sijuh panaitwa simanjiro manyara
 
Back
Top Bottom