Watu mnaoomba Miungu ni heri huo muda muwekeze kwenye vitu vya msingi!

Forgotten

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,518
Reaction score
10,839
"Pray for Palestine" "Pray for Ukraine" "Pray for Congo" "Pray for Kariakoo"

Hizi zimekuwa nyimbo kila mahali utakapopita mtandaoni imekuwa ni kawaida ya wanaoamini kuna Mungu wakijifariji kwa kuandika maneno au kuomba wakiamini kuna mtu wa ajabu yupo mahali anasikiliza maombi yao na kuna maajabu yatatokea.

Hii ni mifano mizuri kuwa wanaoomba Mungu wanapoteza muda na nguvu zao kwenye kitu ambacho hakipo, hakijawahi kuwepo na hakitawahi kuwepo kamwe.

Tangu watu wameanza kuomba hiyo Miungu isiyokuwa na ushahidi wa kuwepo zaidi ya hadithi za Abunuwasi, Dunia hii siyo magonjwa, njaa, vita, wala mabalaa yamewahi kuisha. Kama hiyo Miungu ingekuwepo kusingekuwa na haya yote in the first place.

Watu wanaoomba wanaamini wakifanya hivyo wanaweza kuushawishi ulimwengu kuwa upande wao. Wanadhani wao kuwa karibu na Mungu (their imaginary friend) wanakuwa watu wakipekee sana hivyo wanastahili kuwa first priority kwa kila wanachokiomba. Ndiyo maana wengine wanalia, wanafunga na kuomba ili tu wasikilizwe wao kwanza badala ya wengine.

"God's plan" "God's plan for me" hivi huyo Mungu kama tayari ana mpango na wewe kwanini sasa inabidi umuombe tena, yeye si atimize kulingana na mpango alionao juu yako?

Kuna Miungu zaidi ya 3,000 lakini kila mtu anaamini wa kwake ndiyo wa kweli. 😂
 
Wafia dini hawawez kukuelewa watasema unahitaji neema😂 mi Huwa nawambiaga tu kwamba mungu wa wakristo atawachoma waislam wote moto Kwa kuwa hawamkiri na kumpokea yesu kama mwokoz wa maisha Yao pia MUNGU wa waislam atawachoma wakristo wote moto pia mana imeàndikwa uislam ndio dini ya haki na kweli ya mwenyez mungu, yoyote aliye nje ya uislam yu katka hasara kubwa. Kwa kutumia mistari hyo ya dini hzo kuu mbili lakini wapi watu Bado hayaelew kwamba dini na MUNGU ni propaganda
 
Mkuu usiseme hivyo siku parapanda ikilia utalia na kusaga meno
 
"Pray for Palestine" "Pray for Ukraine" "Pray for Congo" "Pray for Kariakoo"

Hizi zimekuwa nyimbo kila mahali utakapopita mtandaoni imekuwa ni kawaida ya wanaoamini kuna Mungu wakijifariji kwa kuandika maneno au kuomba wakiamini kuna mtu wa ajabu yupo mahali anasikiliza maombi yao na kuna maajabu yatatokea.

Hii ni mifano mizuri kuwa wanaoomba Mungu wanapoteza muda na nguvu zao kwenye kitu ambacho hakipo, hakijawahi kuwepo na hakitawahi kuwepo kamwe.

Tangu watu wameanza kuomba hiyo Miungu isiyokuwa na ushahidi wa kuwepo zaidi ya hadithi za Abunuwasi, Dunia hii siyo magonjwa, njaa, vita, wala mabalaa yamewahi kuisha. Kama hiyo Miungu ingekuwepo kusingekuwa na haya yote in the first place.

Watu wanaoomba wanaamini wakifanya hivyo wanaweza kuushawishi ulimwengu kuwa upande wao. Wanadhani wao kuwa karibu na Mungu (their imaginary friend) wanakuwa watu wakipekee sana hivyo wanastahili kuwa first priority kwa kila wanachokiomba. Ndiyo maana wengine wanalia, wanafunga na kuomba ili tu wasikilizwe wao kwanza badala ya wengine.

"God's plan" "God's plan for me" hivi huyo Mungu kama tayari ana mpango na wewe kwanini sasa inabidi umuombe tena, yeye si atimize kulingana na mpango alionao juu yako?

Kuna Miungu zaidi ya 3,000 lakini kila mtu anaamini wa kwake ndiyo wa kweli. 😂
Ni haki zao za kikatiba na kibinadamu kuamini Mungu wanayemtaka mkuu. Na wewe pia ni haki yako ya kikatiba na kibinadamu kujieleza ulivyojieleza hivi.

Mimi siamini Mungu lakini nakubali katika haki za watu kuamini katika Mungu wanayemtaka.

Haki ya kuamini Mungu unayemtaka na haki ya kutoamini Mungu ni haki moja ile ile, hizi ni pande mbili za haki moja ile ile.

Sina tatizo na watu wanaoamini Mungu katika muktadha wa kiimani, nina tatizo na watu wanaosema Mungu yupo kama fact.

In fact, hata kama Mungu hayupo, kama watu wanapata faraja katika imani ya Mungu, na hawajaniletea imani yao kwangu, watu hao wanastahili kupewa faragha yao ya imani na kuachwa wapate faraja ya imani hiyo, hata kama ni ya uongo.

Ila pia, watu wa imani wakiiweka imani yao sehemu za mitandao ya kijamii, public square, wanajiondolea faragha ya imani na kujianika wakosolewe kimantiki nje ya muktadha wa imani.
 
Back
Top Bottom