Watu Muhimu katika Historia ya Nchi yetu

Wakuu zangu,
Nitarudia tena ktk maombi yangu. Nataka kujifunza kwa yale watu hawa waliyafanya kwani majina tu ni ule msemo wa Simple minds yaani tunajadili WATU badala ya Events na Issues..
Nachoomba wakuu zangu ni kuzungumzia zaidi events na issue ambazo zinaambatanisha majina ya watu hawa.

Namshukuru sana mchangiaji mmoja (jina silikumbuki) alitupa majina na matukio (hasa zile harakati za kinamama ambazo dhahir inaonyesha wazi kuwa harakati za Uhuru zilianza toka miaka ya 40..
Nimeona majina mengi sana hapa lakini sijaona michango yao..na bila sjhaka hii inatokana na kwamba sisi sote ni kizazi kipya tumesimuliwa tu majina ya watu (wanachama) walioshiriki wakati wa Uhuru... na kibaya zaidi ni kwamba hatuna kumbukumbu zozote...

Mkuu GT na Julius, hao wazee wa Pwani nawajua wengi wao kwa majina yao lakini walifanya nini ndicho muhimu zaidi kwangu/kwetu kwani kuwa mwanachama wa jumuiya ya Wiislaam haiwezi kuwa sababu ya kuutafuta Uhuru... Walikuwemo ktk kundi kama vile mimi mwanachama wa Bacelona kuwa uwanjani siku Bacelona anachukua ushindi..Mtasema Mkandara alikuwepo lakini has nothing kabisa na Ushindi wa Bacelona..Kam nilicheza watu watauliza alicheza position gani?.. hapo ndipo mjadala hunoga.. na sii hizi habari za uanachama wa Jumuiya.

Pia kuwepo asilimia 50 ya WaBrazil au Spanish hakuwezi kuwa sababu ya ushindi mzima wa Bacelona..ni mchango wao na nguvu ya pamoja (wahusika kwa uwezo wao na sio imani zao ndiko kumeleta ushindi..sasa tukianza kusema Waislaam wako wangapi Bacelona na sijui wakristu kweli hii inaingia akilini jamani?..Wakuu zangu tuwe wapana kidogo ktk mtazamo wa mambo haya..

Jamani kama mnakumbuka majuzi tu Obama alikuwa Ghana na akatembezwa hadi ktk ktk lile jumba la watumwa...
Amini usiamini, jumba hilo leo hii ni kivutio kikubwa sana cha Watalii nchini Ghana. Toka Obama ameondoka ni zaidi ya watalii 100,000 wameitembelea Ghana na hasa sehemu hizo (wengi wao wakitokea Marekani)..ni record ya nchi hiyo...
Hivyo kuna vitu vya historia ambavyo sisi tumechukulia mzaha na uvivu wa kufikiri tumeviuza au kubomoa historia kwa sababu mswahili hapendi kukumbushiwa machungu.. hata Hospital kutembelea wagonjwa ni mwiko acha mbali makaburi..

Nitazidi kusisitiza tuondokane na Udini, haitusaidii kitu wala haiwezi kupindisha historia kwa sababu AbdulWahid Sykes alikuwa Muislaam, mbona hatusemi alikuwa Msouth (Mzulu)hivyo makabala yetu tulikuwa tumelala..

Navyofahamu mimi, Aboul Wahid na kundi lake wote walipigania Uhuru sii kwa sababu zinazotokana na dini yao ama imani ya dini ila Uzalendo kwa nchi yake..Na uthibitisho mkubwa ni kuwa mpinzani wake mkubwa alikuwa baba yake mwenyewe (khreist) ambaye alitaka chama kile cha kiislaam kibakie chama cha dini kisijiingize ktk maswala ya siasa..Abdul Wahid na Mwapachu wakampindua mzee wa watu na wafuasi wake wote tena wakiwa waislaam...Kikaundwa chama cha siasa.. hivyo matukio haya ni muhimu kuyaweka ktk record pia..kwani wapo waislaam waliopinga mtazamo wa AbdoulWahid kama walivyopinga Wakristu na wapo wakristu walioungana naye...

Wakuu zangu tusiwe kama Wakenya (simple minded people) kila siku hawa jamaa zangu mazungumzo yao ni Ujaluo na Ukikuyu.. hata huku majuu wamegawanyika kiasi hunda vyama vyao kutokana na kabila zao..Hata Harusi au msiba wa Jaluo, Mkikuyu hawezi kwenda na kinyume...imefikia kiasi kwamba hata ku date baina ya makabila haya mawili ni kufuru tena basi huku huku nje majuu...Na Obama ndiye kazidisha kabisa wigo la mgawanyiko wao..Ujinga wote huu unatokana na kwamba Jaluo akidai yeye kasoma na Mkikuyu akidai yeye ndiye kaleta Uhuru..So what?.. Haya tazama WaEthiopia na Eretrea..Wahutu na Watusi, wote yale yale na ndio maana tunaitwa NDIVYO TULIVYO! -huyu akidasi kasoma huyu kaleta Uhuru... Hovyooooo!

Wakuu zangu kumbukerni kwamba hata mapinduzi ya Marekani walipigana wao kwa wao.. Yankee against Loyalist. Sisi hata hatukufikia kumwaga damu baina yetu ingekuwa hivyo kweli leo hii tungekuwa tukizungumza hapa. Na ilikuwaje Marekani hiyo hiyo leo hii hatusikii majina ya watu waliokuwa wamechukua upande wa Muingereza kama ni wasaliti au kusikia states za juu North zikidai kwamba wao ndio waliouleta Uhuru na sio WaSouth..badala yake tunaambiwa majina ya watu na michango waliyoitoa ktk hata sinema zikatengenezwa kulingana na matendo yao na siii majina yao..

Nitasema tena kinachofanyika hapa JF ni simple minds.. jamani tunazungumza sana about OTHER PEOPLE badala ya EVENTS au ISSUES..na ndio maana kila siku nasema haramu ni kitemdo tulaani UFISADI hayo majina yatakuja tu lakini tunapojadili na kulaani sana WATU, huo Ufisadi huonekana kama sii adui yetu mkubwa bali baadhi ya watu fulani..

Mkandara umeprove kuwa hu keep track na posts zilizopo humu za hii thread uliyoianzisha mwenyewe

Umetaka majina ya watu muhimu umepewa...na si hivyo tuu tumekupa mpaka events za Kariakoo ya miaka ile na chimbuko la kuwepo kwa wamanyema wengi kule na contribution yaomkwenye kuanzisha vyama vya kupinga ukoloni....Umetaka events zingine niejaribu kukuelezea kuhusus SAIDI TEWA na ule mkutano uliofanyika pale Anatoglo wa kumchagua Nyerere lakini hayo yoote umejaribu kuyaignore..kwa sababu husomi posts zilizomo humu...kwa kuthibitisha hilo sidhanikama unamjua Mwafrika wa kwanza Tanzania kuanzisha gazeti...yes nilishamtaja huko nyuma lakini kwa sababu husomi posts basi umeingia kwenye malalamiko yako ya siku zote ya udini udini...kama sikosoei hata jina la hilo gazeti lenyewe utakuwa hulijui japo nilishakutajia na nikaelezea hizo events unazozitaka wewe kwa kirefu zilizopelekea kuanzishwa kwa gazeti hilo...lakini hilo si tatizo kwani nalo laweza ongelewa tuuu hata kama lawaudhi watu...

Kuhusu udini mimisikuelewi unataka kusema nini hasa...kila mmoja atakupa events kwa jinsi anavyoona sawa kwake..kama kuna mtu anaona anaweza kukuelezea events kutokana na michezo au vyama vya ushirika uwanja ni wake...unajua unakuwa kama vile wale wazungu wabaguzi kule USA ambao hawataki kukubali au ukweli kuwa AFRICAN AMERICANS fought in the civil war na mchango wao ulikuwa ni mkubwa kuliko ambavyo baadhi ya wazungu wanataka kukubali...watu wakisema ohhh nyie mko obsessed with blacks na racism!!! isnt this the same thing hapa?

Kama kuna mtu ana historia jinsi wakristo na vyama vyao walivyopingana na wakoloni wakiingereza then ailete hakatazwi mtu humu

Kama hupendi kusikia waislam wakihusishwa na harakati za mwanzo za ukombozi wa nchi hii then i'm sorry my friend kuwa huwezi ku pick and hose historia ipi ambayo unayoitaka umetaka historia utaletewa historia..umetaka majina na events utaletewa vyote hivyo
 
Wakuu zangu ningependa sana kujua kwa nini nchi yetu haikuweka record za kumbukumbu ya watu muhimu ktk Historia ya nchi yetu. Watu ambao leo hii wangeitwa mashujaa wa kweli..Watu ambao sisi wengine hatuwajui wala tusingewajua kama sii kuulizia kwa watu..

Mbali na majina tunayoyafamu sote nimepewa majina haya kuwa hawa watu walikuwa muhimu sana ktk mchango wa kupatikana kwa Uhuru wetu..

Kwanza kuna Mzee Tambaza wa Magomeni Mikumi ambaye shule ya Tambaza imepewa jina lake, na Pili kuna Mzee Sheikh Amri Abeid naye wa Magomeni Mikumi ambaye pia uwanja wa mpira wa Arusha ulipewa jina lake.. Huyu mimi nilifikiria jina hilo limetokana na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Amri Abeid Karume, kumbe huyu ni mtu mwingine kabisa..

Je, kuna majina mengine muhimu tuyafahamu? Na zaidi ya yote Upi mchango wao ktk Uhuru na maendeleo ya nchi yetu..

Inasikitisha sana kuona viongozi bora wa nchi hii wanateuliwa kutokana na elimu au umaarufu wao badala ya michango ya watu hao ktk kutuletea mafanikio..wanapoondoka huondoka na kila mazuri yao..

kwa kadri falsafa ya historia ya vitu au watu maarufu inavyojieleza, umaarufu wa mtu kuingia katika historia ya kukumbukwa ni lazima kufanya jambo ambalo aghalabu watu wengi hawakulifahamu bado ama hawakupata ujasiri wa kulifanya. Ni nani katika historia ya mtu mweupe unayemjua wewe ambaye hajakuwa na mchango katika jamii yake na akawa na historia hadi leo? Linkoln, Newton, Plato, socrates, Darwin, Galileo, etc... wote walifanya jambo fulani. Nyerere alikuwa pia tofauti. huwezi ukaniambia kuwa hao wazee waliokuwa wakicheza bao na kusema eti walimfundisha nyerere kuvaa suruali ndio wakumbukwe kiivyo. hata hivyo ukisoma historia ya uhuru na TANU hao wazee utawakuta. tatizo la wabongo si wasomaji wa maandishi. hao wazee waliachieve nini hadi tuwakumbuke kwa staili hiyo?
 
By the way mambo hayakuwa DAR pekeyake kwani kila kona kulikuwa na mwamko na of course huko kusini ndiko kwenyewe kwani chama cha TAA mjini Lindi ilikuwa chini ya uongozi wa mzee Suleiman Masudi Mnonji aliyekuwa Rais na Katibu wake alikuwa Mohamed Waziri.

huyu jamaa Mnonji alikuwa fundi cherahani na Waziri alikuwa mchoraji wa ramani za nyumba(yaani alikuwa SHARIFF wa enzi hizo...ninaposema Shariff MASATU nadhani unanipata hapo) ni vizuri kumfahamisha huyu MKANDARA kuwa TAA ilichelewa kuanza mjini Lindi. TAA ilianzishwa Lindi mwaka 1953 wakati uongozi wa TAA mjini Dar es Salaam si tu ulikuwa unaigeuza TAA kuwa chama cha siasa bali ulikuwa ukifanya mipango kumpeleka mjumbe wake Umoja wa Mataifa kudai uhuru. Masudi Mnonji alikuwa na uzoefu wa kutosha katika siasa....wenyeji wa kusini wataweza kuthibitisha hilo kwani alikuwa mmoja kati ya vigogo wakubwa huko Lindi

Baada ya Vita Kuu ya Pili alikuwa amejaribu kuanzisha vyama vya wafanyakazi katika mashamba mbalimbali ya mkonge kule kusini mwa Tanganyika na si hivyo tuuu vilevile aliwakusanya wapishi na madobi mjini Lindi waanzishe umoja wao.... Ilikuwa kupitia juhudi zake binafsi TAA ijapokuwa ilichelewa, ilikuja kuanzishwa mjini Lindi na Mnonji alijitolea nyumba yake katika mtaa wa Makonde (nasikia MAFISADI wameubadilisha jina huu mtaa ) kama ofisi ya chama. Mnonji kwa kutambua umuhimu wa kuwa na uongozi ulioelimika vizuri, alimleta mtu mmoja anaitwa Nangwanda Sijaona kutoka Nachingwea aje aishauri TAA jinsi ya kufanya mambo kwa utaalamu.

Wakati huo mjini Lindi kulikuwa na chama cha wafanyakazi bandarini Dockworkers' Union chini ya uongozi wa Mussa Athumani Lukundu, chama ambacho kwa kiasi chake kilianzisha vuguvugu la siasa za vyama vya wafanyakazi.... Ingawa vyama hivi viwili, yaani TAA na Dockworkers' Union vilikuwepo katika mji mmoja, siasa za hiki chama cha pili cha wafanyakazi bandarini hazikupitia TAA kama ilivyokuwa mjini Dar es Salaam....na unaambiwa hili kwa kiasi fulani ilidhoofisha mwamamko wa siasa kwa wananchi....mind you Jimbo la Kusini lilikuwa katika usingizi mzito wakati sehemu nyingine Tanganyika zilikuwa zikipiga hatua kwenda mbele zikiandaa vita dhidi ya utawala wa kikoloni.....na chanzo cha usingizi huu mzito huko kusini ulikuwa na asili yake katika historia ya Tanganyika.

SASA MKANDARA NGOJA TUKURUDISHE NYUMA KIDOGO....

Kama ulisoma elimu ya Msingi utakumbuka tulifundishwa kuhusu Vita vya Maji Maji ambavyo vilipoanza kusini ya Tanganyika mwaka 1905 kwa nia ya kuwafukuza Wajerumani kutoka Tanganyika, zile sehemu zenye Wakristo wengi zilikataa kujiunga na vita na badala yake wakajiunga na majeshi ya Wajerumani na kupigana bega kwa bega na dhidi ya wazalendo.(Of course kuna wengine ambao hawajui hata maana ya vita vya maji maji watakuja kupinga hili)

Hii ilitokana na sababu ya kuwa uasi dhidi ya dhulma wa Wajerumani ulianza katika maeneo yenye Waislamu wengi na vita vikachukua sura ya vita vya Kiislamu dhidi ya Wazungu ambao dini yao ni Ukristo na kwa kuwa wamishonari walikuwa washirika wa wakoloni, walichukuliwa kama maadui na hivyo ikawa vituo vyao vinashambuliwa na wapiganaji wa Maji Maji. Kutokana mashambulizi haya, Wakristo walivichukua Vita Vya Maji Maji kama vita dhidi ya Ukristo. na hii inawezekana kuwa sababu kubwa watawala hawapendi tujue sana kuhusu vita vya maji maji.....Harakati za Maji Maji zilishindwa na Wajerumani walifanya fisadi kubwa dhidi ya wananchi na viongozi wao. In the end jambo hili liliacha kovu kubwa katika fikra za wananchi na kwa upande wa Wakristo ambao walinusurika na ghadhabu ya Wajerumani, wengi wao wakajiweka mbali na aina yoyote ya kupinga ukoloni.

Kufuatia historia hii Waafrika waliokuwa kusini ya Tanganyika sasa wakiwa chini ya utawala wa Waingereza na kuwa chini ya himaya ya wamishonari walipupazwa kiasi kiasi kwamba waliogopa siasa.

Baada ya Waafrika kushindwa vita kwa silaha kali za Wazungu sasa Kanisa likaona ndani ya fadhaa ile fursa yao kutawala sehemu hiyo kwa kutoa vishawishi kama vile shule na hospitali. Kwa hiyo Wamishionari na Waingereza walionekana kama mabwana wema wenye kuwajali raia zao kinyume na serikali katili na ya kidhalimu ya Wajerumani.

MKANDARA upo au umelala?
 
Hii ilitokana na sababu ya kuwa uasi dhidi ya dhulma wa Wajerumani ulianza katika maeneo yenye Waislamu wengi na vita vikachukua sura ya vita vya Kiislamu dhidi ya Wazungu ambao dini yao ni Ukristo na kwa kuwa wamishonari walikuwa washirika wa wakoloni, walichukuliwa kama maadui na hivyo ikawa vituo vyao vinashambuliwa na wapiganaji wa Maji Maji. Kutokana mashambulizi haya, Wakristo walivichukua Vita Vya Maji Maji kama vita dhidi ya Ukristo. na hii inawezekana kuwa sababu kubwa watawala hawapendi tujue sana kuhusu vita vya maji maji.

Na hapa tunampata mtu mwingine muhimu, kiongozi wa Vita vya Maji Maji, Shehe Alhaji Kinjekitile Ngwao. Na Maji yaliyotumika ni Maji yenye baraka ya Zam Zam kutoka Maka. Lakini wakifundisha mashuleni wanasema maji ya uganga!
 
Swadakta kabisa maalim wangu...ni vizuri tukamfahamisha bwana mkandara na kundi lake kuwa vuguvugu la siasa kama ilivyokuwa Vita vya Maji Maji, lilianza katika maeneo ya Waislam kufuatia mfumo ule ule kama ilivyokuwa katika upinzani wa ukoloni wa Wajerumani...vile vile ni muhimu kusisitiza kuwa Wakristo katika Jimbo la Kusini waliiona TANU kama walivyoviona Vita Vya Maji Maji, kama harakati nyingine za Waislam zilizokuwa zikija tena kwa mara ya pili kuvuruga amani na utulivu.(na of course kama unavyoona humu JF wanavyo lalama kuhusu mahakama ya kadhi italeta vurugu na kuvunja amani...as if hiyo amani ilikuwepo)

Vile vile nadhani ni muhimu kuwaelimisha hawa watoto kuwa mtu wa kwanza kuutanabaisha uongozi wa TAA mjini Lindi juu ya mageuzi yaliyokuwa yakitokea Tanganyika na kuanzishwa kwa chama kipya cha siasa mjini Dar es Salaam alikuwa anaitwa Abdallah Juma Makopa, kijana kutoka Tanga akifanya kazi ya ukarani Posta ya Lindi. Makopa aliwaendea Mnonji na Waziri na kuwajulisha kuhusu kuanzishwa kwa TANUmjini Dar es Salaam na aliwashauri waanzishe TANU pale Lindi. Jambo hilo lilipingwa moja kwa moja na Mnonji, Waziri, Said Nassoro, Abdallah Mhuji na wanachama wengine wa TAA.

Chama cha Waafrika ambacho kilianzishwa siku nyingi mjini Lindi na kwa hakika ndicho kilikuwa chama cha pekee kushughulikia maslahi ya Waafrika sehemu za kusini kilikuwa African Welfrare Association ambacho mlezi wake alikuwa John Nevi, Mjaluo kutoka Kenya na katibu wake alikuwa Casian Njunde, Mngoni wa Songea. Makopa aliposhindwa kukishawishi kile kikundi cha wazee wa TAA ndipo alipowaendea Yusufu Chembera na Rashid Salum Mpunga

wenyeji wa Lindi ambao ni members wa JF wanaweza kuja kuleta nyeti zaidi....
 
Hizi historia zingekuwa zina ambatanishwa picha ingekuwa bora zaidi mie kuna jamaa yangu yupo Iringa ameniahidi kunitafutia picha za wana harakti wa TANU mkoani humo zama za kudai Uhuru.Waanzilishi wa TANU mkoani Iringa,ni:Hussein bin Issa,Omari Arubati,Abdallah Mabruki,Ibrahim Makongwa,Ahmed Wanguvu
 
maneno yako mazima kabisa mmee huko Iringa ninakuja tar-tiiibu
Vile vile si vibaya kukumbusha kuwa serikali ya kikoloni iliweza kudhibiti habari, ikitoa habari zile ambazo ilifikiria muhimu kwa maslahi yake yenyewe na hivyo zinafaa kusomwa na raia. Idara ya Maendeleo ya Jamii ilikuwa ikichapisha magazeti ya Kiswahili - Mambo Leo, Tazama, Mwangaza na Baragumu.

Wamishonari walikuwa wakichapisha Kiongozi na Lengo, magazeti haya yakimilikiwa na Wakatoliki na Walutheri. Madhehebu ya Ahmadiyya ilikuwa na gazeti lao - Mapenzi ya Mungu lakini gazeti hili halikuwa maarufu na nakala chache sana ndizo zilizokuwa zikiuzwa. Kwa kuwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni ndiyo wengi Tanganyika, watu walijiepusha na gazeti hilo wakiliona kama kama chombo cha kufru.

Wakati magazeti ya serikali yakijishughulisha zaidi na kampeni za kufuta ujinga kwa kuchapisha porojo na visa kuwahimiza watu kusoma, Wamishionari walijikita zaidi katika kueneza Biblia na propaganda za kupinga Ukomunisti. Kwa kushirikiana katika nyanja ya vyombo vya habari serikali na Wamishonari waliweza kuyalinda maslahi yao kwa pamoja.

Ningependa kumkumbusha huyu MKANDARA kuwa japo anajifanya hasomi lakini si vibaya kumwambia kuwa RAMADHANI MASHADO PLANTAN ndiye alivunja ukiritimba huu baina ya serikali na Wamishionari. Akifuata nyayo za Erika Fiah, Mwafrika wa kwanza kuchapisha gazeti katika Tanganyika, Mashado alianzisha gazeti lake Zuhra.
 
Wakuu zangu,
Nitarudia tena ktk maombi yangu. Nataka kujifunza kwa yale watu hawa waliyafanya kwani majina tu ni ule msemo wa Simple minds yaani tunajadili WATU badala ya Events na Issues..
Nachoomba wakuu zangu ni kuzungumzia zaidi events na issue ambazo zinaambatanisha majina ya watu hawa.
Namshukuru sana mchangiaji mmoja (jina silikumbuki) alitupa majina na matukio (hasa zile harakati za kinamama ambazo dhahir inaonyesha wazi kuwa harakati za Uhuru zilianza toka miaka ya 40..
Nimeona majina mengi sana hapa lakini sijaona michango yao..na bila sjhaka hii inatokana na kwamba sisi sote ni kizazi kipya tumesimuliwa tu majina ya watu (wanachama) walioshiriki wakati wa Uhuru... na kibaya zaidi ni kwamba hatuna kumbukumbu zozote...

Mkuu GT na Julius, hao wazee wa Pwani nawajua wengi wao kwa majina yao lakini walifanya nini ndicho muhimu zaidi kwangu/kwetu kwani kuwa mwanachama wa jumuiya ya Wiislaam haiwezi kuwa sababu ya kuutafuta Uhuru... Walikuwemo ktk kundi kama vile mimi mwanachama wa Bacelona kuwa uwanjani siku Bacelona anachukua ushindi..Mtasema Mkandara alikuwepo lakini has nothing kabisa na Ushindi wa Bacelona..Kam nilicheza watu watauliza alicheza position gani?.. hapo ndipo mjadala hunoga.. na sii hizi habari za uanachama wa Jumuiya.

Pia kuwepo asilimia 50 ya WaBrazil au Spanish hakuwezi kuwa sababu ya ushindi mzima wa Bacelona..ni mchango wao na nguvu ya pamoja (wahusika kwa uwezo wao na sio imani zao ndiko kumeleta ushindi..sasa tukianza kusema Waislaam wako wangapi Bacelona na sijui wakristu kweli hii inaingia akilini jamani?..Wakuu zangu tuwe wapana kidogo ktk mtazamo wa mambo haya..

Jamani kama mnakumbuka majuzi tu Obama alikuwa Ghana na akatembezwa hadi ktk ktk lile jumba la watumwa...
Amini usiamini, jumba hilo leo hii ni kivutio kikubwa sana cha Watalii nchini Ghana. Toka Obama ameondoka ni zaidi ya watalii 100,000 wameitembelea Ghana na hasa sehemu hizo (wengi wao wakitokea Marekani)..ni record ya nchi hiyo...
Hivyo kuna vitu vya historia ambavyo sisi tumechukulia mzaha na uvivu wa kufikiri tumeviuza au kubomoa historia kwa sababu mswahili hapendi kukumbushiwa machungu.. hata Hospital kutembelea wagonjwa ni mwiko acha mbali makaburi..

Nitazidi kusisitiza tuondokane na Udini, haitusaidii kitu wala haiwezi kupindisha historia kwa sababu AbdulWahid Sykes alikuwa Muislaam, mbona hatusemi alikuwa Msouth (Mzulu)hivyo makabala yetu tulikuwa tumelala..
Navyofahamu mimi, Aboul Wahid na kundi lake wote walipigania Uhuru sii kwa sababu zinazotokana na dini yao ama imani ya dini ila Uzalendo kwa nchi yake..Na uthibitisho mkubwa ni kuwa mpinzani wake mkubwa alikuwa baba yake mwenyewe (khreist) ambaye alitaka chama kile cha kiislaam kibakie chama cha dini kisijiingize ktk maswala ya siasa..Abdul Wahid na Mwapachu wakampindua mzee wa watu na wafuasi wake wote tena wakiwa waislaam...Kikaundwa chama cha siasa.. hivyo matukio haya ni muhimu kuyaweka ktk record pia..kwani wapo waislaam waliopinga mtazamo wa AbdoulWahid kama walivyopinga Wakristu na wapo wakristu walioungana naye...

Wakuu zangu tusiwe kama Wakenya (simple minded people) kila siku hawa jamaa zangu mazungumzo yao ni Ujaluo na Ukikuyu.. hata huku majuu wamegawanyika kiasi hunda vyama vyao kutokana na kabila zao..Hata Harusi au msiba wa Jaluo, Mkikuyu hawezi kwenda na kinyume...imefikia kiasi kwamba hata ku date baina ya makabila haya mawili ni kufuru tena basi huku huku nje majuu...Na Obama ndiye kazidisha kabisa wigo la mgawanyiko wao..Ujinga wote huu unatokana na kwamba Jaluo akidai yeye kasoma na Mkikuyu akidai yeye ndiye kaleta Uhuru..So what?.. Haya tazama WaEthiopia na Eretrea..Wahutu na Watusi, wote yale yale na ndio maana tunaitwa NDIVYO TULIVYO! -huyu akidasi kasoma huyu kaleta Uhuru... Hovyooooo!

Wakuu zangu kumbukerni kwamba hata mapinduzi ya Marekani walipigana wao kwa wao.. Yankee against Loyalist. Sisi hata hatukufikia kumwaga damu baina yetu ingekuwa hivyo kweli leo hii tungekuwa tukizungumza hapa. Na ilikuwaje Marekani hiyo hiyo leo hii hatusikii majina ya watu waliokuwa wamechukua upande wa Muingereza kama ni wasaliti au kusikia states za juu North zikidai kwamba wao ndio waliouleta Uhuru na sio WaSouth..badala yake tunaambiwa majina ya watu na michango waliyoitoa ktk hata sinema zikatengenezwa kulingana na matendo yao na siii majina yao..

Nitasema tena kinachofanyika hapa JF ni simple minds.. jamani tunazungumza sana about OTHER PEOPLE badala ya EVENTS au ISSUES..na ndio maana kila siku nasema haramu ni kitemdo tulaani UFISADI hayo majina yatakuja tu lakini tunapojadili na kulaani sana WATU, huo Ufisadi huonekana kama sii adui yetu mkubwa bali baadhi ya watu fulani..

Mkandara:
Kuna vitu ni lazima tukubali kwanza, kabla ya kuendelea mbele na mjadala. Tanganyika kama taifa, lilijengwa na wakoloni. Na ndani ya taifa hili kulikuwa na mataifa kamili yenye identity zake za kikabila. Na wale ambao hawakuwa na identity za kikabila walikuwa na identity za kidini au kiukazi. Hivyo watu kwa kutumia identity zao walianza harakati zamani kupigania uhuru au haki zao.

Hivyo basi kutokana na identities zetu, ni lazima tukubali kabisa harakati za mwanzo zilikuwa sio za kitaifa. Hata ukienda Kenya, Nigeria na nchi zote za kiAfrika, harakati za mwanzo zilikuwa hazikuenea taifa zima.

Hivyo katika mjadala kama huu kuna machaguo mawili tu. Chaguo la kwanza ni kutaja watu mashuhuri kuanzia July 7, 1954. Maana kuanzia hapa ma-super wenye kueleweka nchi nzima walianza kuonekana. Tatizo la chaguo hili ni kuwa historia yetu itakuwa fupi sana.

Chaguo la pili ni kutaja watu mashuhuri kabla ya July 7, 1954. Hapa historia yetu itakuwa tajiri sana. Lakini ni lazima tukubali udini, ukabila na mambo mengine.

Mimi si mchagga lakini events zilizowafanya wao kuanzisha vyama vya ushirika ninatoa Inspirations. Tunawalaumu wachagga kuwa ni wabaguzi, lakini juhudi zao za mwanzo za kujenga shule na mahospitali ndio msingi wa maendeleo yao. Na hayo yalifanyika kwa sababu walikuwepo viongozi imara kama Marealle.

Wapare walikuwa na juhudi zao kama wapare. Lakini mpare yoyote akitoa mchango wake ataonekana kuwa ana ukabila fulani. Mijini walikuwa na harakati zao. Lakini ukitaja majina, udini utaoneka.
Nina uhakika kuwa kulikuwepo na events za kuanzisha TAA, ambazo ni muhimu kwa watanzania kuzijua.

Simplest ya mind inayokuja hapa wakati mwingine inakuja kwa sababu kuna watu hawajuhi mchango wa sehemu aliyotoka katika harakati za kupigania haki toka ukoloni uingie.
 
Hapana. Sijakubali Nyerere ni muuaji... Sijui nani aliyemwua Babu yako. Lakini nina hakika hakuwa Nyerere.

Jasusi, ww kataa, lakini historia haifutiki kuwa watu wafuatao na wengine wengi tu, walipotea katika mazingira ya kutatanisha na mpaka leo hawajuulikani walipo, kukamatwa kwao, kuwekwa kwao kizuizini na taarifa zao kufutika kote huku kulijuulikana na Mwalimu Nyerere, wengine walizuiliwa katika "torture chamber" za Oysterbay na Kigoto, Mwanza na baadhi yao kabla ya kuuwawa,Nyerere aliwatembelea walipokuwa wamezuiliwa, na kuwa mtu wa mwisho kuwaona wakiwa hai. Baadhi yao ni hawa hapa:

Abdulaziz Twala, Saleh
Sadala Akida, Jimmy Ringo, Amour Zahour, Hemed Said, M Makame Hatibu, Idrissa Majura, Seif A. Nassor, Aboud
Nadhif, Khamis Masoud, Jaha Ubwa, Mdungi Usi.

Swadakta kabisa maalim wangu...ni vizuri tukamfahamisha bwana mkandara na kundi lake kuwa vuguvugu la siasa kama ilivyokuwa Vita vya Maji Maji, lilianza katika maeneo ya Waislam kufuatia mfumo ule ule kama ilivyokuwa katika upinzani wa ukoloni wa Wajerumani...vile vile ni muhimu kusisitiza kuwa Wakristo katika Jimbo la Kusini waliiona TANU kama walivyoviona Vita Vya Maji Maji, kama harakati nyingine za Waislam zilizokuwa zikija tena kwa mara ya pili kuvuruga amani na utulivu.(na of course kama unavyoona humu JF wanavyo lalama kuhusu mahakama ya kadhi italeta vurugu na kuvunja amani...as if hiyo amani ilikuwepo)

Vile vile nadhani ni muhimu kuwaelimisha hawa watoto kuwa mtu wa kwanza kuutanabaisha uongozi wa TAA mjini Lindi juu ya mageuzi yaliyokuwa yakitokea Tanganyika na kuanzishwa kwa chama kipya cha siasa mjini Dar es Salaam alikuwa anaitwa Abdallah Juma Makopa, kijana kutoka Tanga akifanya kazi ya ukarani Posta ya Lindi. Makopa aliwaendea Mnonji na Waziri na kuwajulisha kuhusu kuanzishwa kwa TANUmjini Dar es Salaam na aliwashauri waanzishe TANU pale Lindi. Jambo hilo lilipingwa moja kwa moja na Mnonji, Waziri, Said Nassoro, Abdallah Mhuji na wanachama wengine wa TAA.

Chama cha Waafrika ambacho kilianzishwa siku nyingi mjini Lindi na kwa hakika ndicho kilikuwa chama cha pekee kushughulikia maslahi ya Waafrika sehemu za kusini kilikuwa African Welfrare Association ambacho mlezi wake alikuwa John Nevi, Mjaluo kutoka Kenya na katibu wake alikuwa Casian Njunde, Mngoni wa Songea. Makopa aliposhindwa kukishawishi kile kikundi cha wazee wa TAA ndipo alipowaendea Yusufu Chembera na Rashid Salum Mpunga

wenyeji wa Lindi ambao ni members wa JF wanaweza kuja kuleta nyeti zaidi....

Nikiwaambia kuwa Game Theory ni bonge la fundamentalist wa kiislam mnasema kuwa namuonea. Mnaona maandishi yake? Ukichukulia kuwa GT ndiye mwakilishi wa Kikwete kiaina hapa JF, usishangae kuwa haya mambo ya udini ni mbinu ya serikali ya Kikwete kuwavuruga watanzania
 
Naam kwa kuendelea tuuu ni kuwa bwan Ramadhani Mashado alizaliwa mwaka 1900 huko Lourenco Marquis (sasa Maputo) na alikuja Tanganyika akiwa mtoto mdogo mwaka 1905 wakati nchi ipo katika vita vya Maji Maji dhidi ya Wajerumani.....waka 1924 alirudi Msumbiji na alisafiri kwenda Lisbon kwa pasi ya Kireno. Wale waliomfahamu wanasema kwa kiwango cha miaka ya 1950, Mashado Plantan alikuwa mtu mjuzi wa mambo. Alikuwa miongoni mwa wanachama wa mwanzoni wa African Association ilipoanzishwa mwaka 1929 na miongoni mwa wanchama wa awali kujiunga na TANU pale ilipoasisiwa mwaka 1954.

Unlike akina media owners tulionao sikuhizi gazeti laZUHRA lilikuwa na masimamowa kuwazindua na kuwashirikisha Waafrika kupambana na ukoloni pamoja na ubeberuna katika editorial zaje zake nyingi, Mashado alimwonyesha Mwingereza kama mgeni ambae baada ya kukaribishwa sasa anambughudhi mwenyeji wake.... Lakini gazeti hilo halikuwa likithaminiwa na wasomi ambao walilidharau na kuliona kama gazeti la Kiswahili tu, lisilokuwa na ujuzi wowote, lililokusudiwa hasa msomaji wa chini asiye na elimu na asiyejua kusoma Kiingereza.

Mashado, kwa kupitia safu za Zuhra, alikuwa ndiye msemaji wa African Association na kupitia tahariri zake alitangaza na kudhihirisha msimamo wa chama.

Una la zaidi?
 
Na baadaye akaenda Iran na Saudi Arabia kujifunza zaidi.
 
Mwalimu wangu mmoja aliniambia kwa kimombo" HISTORY IS MADE. IT DOES NOT HAVE TO BE WRITTEN".

Nimeanza mchango wangu huu hivi kwa vile inaonekana kwamba wanaJF wengi wanalalamika kwamba michango ya Waislamu ktk historia yetu haikutambulika. Hiyo sio kweli. Pia kuna impression kwamba serikali ya kimla ya Mwalimu Julius Nyerere haikuwaathiri Wakristo au kwamba Nyerere alikuwa anawapendelea Wakristo. Kuna dhana pia kwamba historia yetu, kama taifa, imekuwa ni monopoly ya watu wa pwani. Sio kweli pia.

John Rupia,Msukuma, alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa TANU ilipoanza. Japhet Kirilo wa Meru aliyekwenda UNO kupetition juu ya ardhi ya Wameru, ametajwa. Lakini Thomas Lenana Marealle, aliyekuwa New York wakati Julius Nyerere akihitubia UNO hajatajwa. Uchangiaji wa mtu unaweza kuwa negative. Lakini historia ni lazima iseme.

Sasa nami niongeze majina ambayo najua yanastahili kuwekwa ktk kumbukumbu zetu.: Bibi Titi Mohamed kiongozi wa wakina mama, Mama Sofia Kawawa aliyekuwa Mwenyekiti wa kinamama na Lucy Lameck. Machifu Adam Sapi Mkwawa, Humbi Ziota na David Kidaha Makwaiya na mdogo wake Hussein waliotiwa kizuizini na Nyerere.

Chifu mwingine ni Petro Itosi Marealle (mwananchi anayeonekana amevalia suti ya kisasa) ktk picha ya kuchanganya udongo wa Tanganyika na wa Zanzibar kuashiria Muungano tarehe 26 Aprili, 1964. Wengine ni Erasto Mbwana Mang'enya, John N. Maruma, Abdieli Shangali, Harun Lugusha wa Tabora walikuwa Legco kabla ya Uhuru.

Kundi la kina Tewa Said Tewa walikuwepo Solomon Eliufoo (Waziri wa Elimu, baadaye wa Afya). Waziri wengine walikuwa Asanterabi Z. Nsilo-Swai, Clement George Kahama, Saidi Maswanya, Bhoke Munanka na Amir Jamal. Jacob Namfua naye alikuwa Msaidizi wa Waziri wa Fedha hapo mwanzo.

WanaJF wanaotaka majina zaidi ya walioshiriki harakati za uhuru wasome Hansard pale Ofisi ya Bunge katika miaka ya 1958/1961.
 
Last edited:
safi sana mzee KILASARA

lakini usisahau kuwa Mkandara alikuwa anataka na events yaani narrative ya matukio na sie tumeona why not give a bro what he wants?

all in all post yako ni nzuri isipokuwa kuna walakini kidogo na ni difference ambayo sidhani ni muhimu kuipoint out maana post yako imekamilika

safi sana mzee na tungependa kuona michango yako zaidi humu
 
Mwalimu wangu mmoja aliniambia kwa kimombo" HISTORY IS MADE. IT DOES NOT HAVE TO BE WRITTEN".

Nimeanza mchango wangu huu hivi kwa vile inaonekana kwamba wanaJF wengi wanalalamika kwamba michango ya Waislamu ktk historia yetu haikutambulika. Hiyo sio kweli. Pia kuna impression kwamba serikali ya kimla ya Mwalimu Julius Nyerere haikuwaathiri Wakristo au kwamba Nyerere alikuwa anawapendelea Wakristo. Kuna dhana pia kwamba historia yetu, kama taifa, imekuwa ni monopoly ya watu wa pwani. Sio kweli pia.

John Rupia,Msukuma, alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa TANU ilipoanza. Japhet Kirilo wa Meru aliyekwenda UNO kupetition juu ya ardhi ya Wameru, ametajwa. Lakini Thomas Lenana Marealle, aliyekuwa New York wakati Julius Nyerere akihitubia UNO hajatajwa. Uchangiaji wa mtu unaweza kuwa negative. Lakini historia ni lazima iseme.

Sasa nami niongeze majina ambayo najua yanastahili kuwekwa ktk kumbukumbu zetu.: Bibi Titi Mohamed kiongozi wa wakina mama, Mama Sofia Kawawa aliyekuwa Mwenyekiti wa kinamama na Lucy Lameck. Machifu Adam Sapi Mkwawa, Humbi Ziota na David Kidaha Makwaiya na mdogo wake Hussein waliotiwa kizuizini na Nyerere.

Chifu mwingine ni Petro Itosi Marealle (mwananchi anayeonekana amevalia suti ya kisasa) ktk picha ya kuchanganya udongo wa Tanganyika na wa Zanzibar kuashiria Muungano tarehe 26 Aprili, 1964. Wengine ni Erasto Mbwana Mang'enya, John N. Maruma, Abdieli Shangali, Harun Lugusha wa Tabora walikuwa Legco kabla ya Uhuru.

Kundi la kina Tewa Said Tewa walikuwepo Solomon Eliufoo (Waziri wa Elimu, baadaye wa Afya). Waziri wengine walikuwa Asanterabi Z. Nsilo-Swai, Clement George Kahama, Saidi Maswanya, Bhoke Munanka na Amir Jamal. Jacob Namfua naye alikuwa Msaidizi wa Waziri wa Fedha hapo mwanzo.

WanaJF wanaotaka majina zaidi ya walioshiriki harakati za uhuru wasome Hansard pale Ofisi ya Bunge katika miaka ya 1958/1961.

Kilasara:

Asante kwa mchango wako wa kutia moyo. Kwa bahati nimekaa katika nchi za ki-communist au kijamaa. Matatizo ya nchi za ki-communist au kijamaa usipoamini itikadi yao unaondoka kwenye historia.

Na mara nyingi katika nchi ki-communist au kijamaa, historia inaanza pale itikadi zao inapoanza. Kwetu Tanzania, baada ya ujamaa kupamba moto, wale wote wasioweza kuimba kijamaa walifutwa kwenye historia wawe waKristo au waIslam.

Katika vitabu vya shule kwa sisi tuliosoma miaka ya baadaye, ilikuwa ni rahisi kumsoma Seti Benjamini au Dr. Kleuu, kuliko kuwasoma watu uliotaja hapo juu. Kuna baadhi ya viongozi wa mgogoro wa Arumeru, wanafahamika zaidi Kenya kuliko Tanzania.
 
Hata katika nchi za kibepari, usipoimba kile mafisadi wa kibepari wanachotaka, unafutwa kwenye historia.

Anza na Kenya au hata baba ya ubepari - Marekani
 
Bro:

Tumia basi angalau ubunifu. Sio kuja na kujaribu kupinduapindua posti za watu.

Watu wengine mliopata uraia wa Tanzania kwa makaratasi ya ukimbizi mnaonekana tu.
 
Back
Top Bottom