Watu na hisia

Watu na hisia

Black listed

Senior Member
Joined
Apr 6, 2023
Posts
181
Reaction score
260
Kila mwanadamu anaongozwa na hisia na akili katika kuendesha maisha yake hapa duniani. Wanyama pia huongozwa na hisia katika harakati za kujitafutia mawindo au kumkimbia adui yao (predators).

Kabla ya jambo lolote kufanyika, hisia kupitia viungo vya fahamu (sensory organs) kama vile macho, masikio, ngozi, pua, nywele, nk, huzalisha tamaa au kukata tamaa (impulse) juu ya jambo fulani na kutuma ujumbe akilini ili jambo hilo lifanyike au la.

Katika hali ya kawaida, akili inatakiwa kuiongoza hisia (mind should be dominant over emotions), na siyo hisia kuiongoza akili. Ikitokea kinyume chake, basi muhusika atakuwa katika hali (maisha) ya ubabaishaji. Kuendelea kwake kimaisha kutategemea bahati tu aliyo nayo na siyo uwezo wa akili yake. Watu hao wapo.

Watu wanaoongozwa na hisia (emotion is dominant over the mind), huamua kufanya jambo fulani bila tafakari ya kina, kuona kama ana uwezo wa rasilimali kama fedha, muda, nguvukazi zinazohitajika kukamilisha jambo hilo. Matokeo yake jambo hilo (au kazi hiyo) huishia njiani na rasilimali zilizotumika hupotea.

Kwa mfano, utakuta mtu ameona mwenzake anajenga jengo la ghorofa, bila ya kufanya tathmini ya uwezo alio nao, na yeye anaiga kujenga jengo la ghorofa. Ujenzi unafikia nusu, hela imekata na hana uwezo wa kupata hela nyingine. Atawaambia watu, nimesimamisha ujenzi kidogo, nitaendelea siku chache zijazo, kumbe ndio nitolee.

Matokeo yake, jengo linakaa miaka na miaka bila kuendelezwa. Jengo linapigwa mvua mpaka linanabadilika rangi na kuwa jeusi tii na kusababisha kero, maana lipo katikati ya nyumba za watu. Hii yote imesababishwa na kupenda zaidi sifa (mashindano) kulikoongozwa na hisia na sio akili. Angeongozwa na akili, angeegemea uwezo alio nao, na kisha kujenga nyumba ya uwezo wake na ingeisha na kuwa na manufaa kwake. Usimuige tembo kun........makubwa, utapasuka msamba!

Wengine hupenda kutoa misaada ili tu ajenge jina (apate umaarufu). Utakuta mtu uwezo wa kuihudumia familia yake tu ni shida, lakini akisikia mahalj fulani panahitajika msaada, yupo radhi hata kukopa akatoe msaada ili aonekane. Na mara nyingi atajitahidi kutafuta fulsa kwenye watu wengi, ndipo atoe msaada wake. Hizi zote ni sifa za watu wanaoongozwa na hisia na sio akili!

Kuna makundi matatu katika mtazamo wa uwiano kati ya akili na hisia. Kundi la kwanza ni hili nililoongelea hapo juu (hisia zinatawala akili), na sifa zake ni kama nilivyokwishazielezea hapo juu. Lakini sifa nyingine ya watu hawa, ikitokea yuko katika mkusanyiko wa watu na likaongelewa jambo la kuchekesha, watu hawa hucheka sana, maana wanatawaliwa na hisia zaidi. Tukumbuke tunacheka baada ya kuhisi na akili kutafsiri jambo husika, sasa hisia ikizidi ndipo akili inashindwa kuidhibiti (control) akili na mtu atacheka sana. Sifa nyingine, ni wale wanaoongea peke yao. Mtu kuongea peke yake, zile ni hisia (emotions).

Kundi la pili ni wale wenye uwiano sawa wa akili na hisia. Sifa ya watu hawa ni kwamba akitamani kufanya jambo fulani, atalifikiria namna ya kulifanya mpaka kukamilika, na ataanza kulifanya. Huyu hata kama alianzisha kujenga jengo la ghorofa, atajitahidi kwa kadiri iwezekanavyo, hata kwa kutumia njia zisizo halali ili kutimiza lengo lake, maana alikwishaona mapema namna ya kupata rasilimali pindi akikwama, na wakati huohuo ana shauku ya kupata kile alichokusudia. Watu wa aina hii hupenda burdani kwa wastani, na ikitokea jambo la kuchekesha, wanacheka kwa kadiri.

Kundi la mwisho (la tatu), ni wale wenye akili inayozidi hisia. Hawa hutumia zaidi akili kuliko hisia. Watu wa aina hii wakitamani kufanya jambo linalohitaji rasilimali, hulichambua jambo hilo kwa kina kabla ya kuanza utekelezaji. Gharama zote zinapigiwa hesabu na kupata mustakabali mzima wa jambo husika. Akiridhika na mahesabu yake, ndipo huanza utekelezaji. Watu hawa wakianza project fulani, mara nyingi hufanikiwa. Hii inatokana na plan na mikakati waliyoipanga kabla ya kuanza jambo lenyewe.

Kwa upande wa burdani, watu hawa hawapendelei sana burdani, muda mwingi wanapenda kutafakari namna ya kufanya jambo jipya. Wakijichanganya na watu, mara nyingi hawapendi kuongea, na likitokea jambo la kuchekesha, wao hucheka kidogo sana. Wakati nyinyi wengine mnacheka hadi kutoa machozi, yeye anafunua mdomo kidogo tu na kisha kufumba, hapo ameshamaliza kucheka. Baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa watu wa aina hii hawana bandama ndio maana wanashindwa kucheka. Hiyo sio kweli, ukweli ni kwamba watu hawa wana uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.

Tujitathmini kila mtu kwa wakati wake yuko katika kundi gani!
 
Nitacheka sana panapochekesha sana Yani....[emoji1][emoji1]kwenye kulia nitalia sana na pa kukaa kimya nitakaa kimya....maisha ni mafupi sana
 
N kosa kubwa kuongozwa na hisia katka ufanya maisha,tunafaa kujifunza namna ya kuthibit hisia zetu

Kanuni elekezi n hii

TAFAKARI,TATHMINI,CHUKUA HATUA
 
Back
Top Bottom