Davis Abely Nziku
Member
- Jun 3, 2022
- 13
- 13
WATU NI MTAJI
Mtaji ni Fedha ambayo ni lazima uwe nayo katika mwanzo wa biashara yoyote ile. Mtaji ndio msingi mkuu wa biashara yoyote ile ili iweze kukua na kufikia malengo na matamanio ya mfanyabiashara. Natumaini ushawahi kusikia mtu/watu wakisema kuwa Sina Mtaji ndio maana sijafanya Biashara yoyote. La hasha watu wengi tumekalili mtaji ni Fedha tu Lakini mtaji mkuu katika biashara yoyote ile ni WATU.
WATU
Watu ni Nani, watu ni mimi wewe, sisi, wale na wao, Mtaji wa watu ndio kila kitu katika msingi wa biashara yoyote ile, maana hata kama ukiwa hauna mtaji wa Fedha utaweza kuwakopa watu au wakaweza kukusaidia. Ndio maana siku hizi Kuna msemo unasema "ISHI NA WATU VIZURI" kama utashindwa kuishi na watu vizur basi hata uwe na Mtaji Fedha wa mamilioni na mabilioni basi hautaweza kufika popote vilevile ukiwa na mtaji watu hata kama huna Fedha Unaweza kuwatumia Hao watu vizuri na ukaweza kufikia ndoto zako.
Katika Mtaji watu ni lazima uwe makini Sana katika kuwagawa Hao watu maana ukikosea kuwaweka katika makundi Yao basi Mtaji watu kwako utakuwa hauna maana ni lazima uzingatie mtu wa jikoni ni lazima akae jikon na sio Sebuleni au Chumbani na mtu wa kukaa getini akae Getini na mtu wa kupita awe wakupita sio wewe mtu wa kupita unataka umpeleke hadi Chumbani kwako hapo utakuwa unatumia vibaya mtaji watu.
Kuna watu pia wanamtaji wa Fedha lakini hawana watu na Kuna watu hawana mtaji Fedha wala mtaji watu sasa naomba unisikilize kwa umakini Sana namna ya kuwa na watu sahihi katika mzunguko wako ili Hao watu waweze kuwa mtaji wako
1.Jiweke katika mazingira Safi na watu Safi kama unataka kuwekeza katika mpila basi ni lazima ukubali kukaaa karibu na makocha, wachezaji wawekezaji katika mpira na sio wewe unataka uwekeze katika mpila ila unazungukwa na watu wanaomiliki Bar, Restaurant, lodge au wapika mihogo hapo utakuwa unajikosea wewe mwenyewe kuzungukwa na watu sahihi.
2. Ondokana na makundi mabaya, kama wewe ulikuwa ni mtu wa Starehe Sana au mtu wa pombe basi ni lazima ukae mbali na Hao marafiki zako walevi ili uweze kufikia ndoto zako maana Hao watu wako wakaribu wanaweza kukuvuta ili usifikie malengo yako hivyo basi Ondoka haraka iwezekanavyo katika Hao watu wabaya
3.Ambatana na watu sahihi kokote uendako lazima utambue ni lazima uambatane na watu sahihi maana watu husema "KAA NA WARIDI UNUKIE" hivyo basi ili kuwa na mzunguko wa watu sahihi ni lazima ukae na watu sahihi kwako katika jambo Fulani unalolitaka
4. Kaa karib na Watu wenye Elimu ya Juu ukikaa karibu na wasomi lazima na wewe wakubadilishe kifikra kimtazamo na hata katika utendaji wa mambo yako utakuwa unayaendesha kisomi somi kuliko ukikaa na wajinga wenzako na wewe utaishia kuwa mjinga mjinga tu
5.Toka katika eneo la faraja (Get out of comfort zone) huwezi kubadilika kama kila siku utakuwa unakaaa katika comfort zone na pia kama hubadilishi mazingira basi huwezi kufanikiwa na hautaweza kuwa na mtaji watu Wa maana.
6.Kubali kujifunza kwa watu wengine, hata kama huyo mtu anaekufundisha hakujui au hata humjui ila lazima uwe mwepesi katika kukubali kujifunza hata kama uwe umemzidi maarifa.
Yafuatayo ni madhara ya Kuchagua watu Vibaya
1.Kukatishwa Tamaa, kama utakuwa na marafiki ambao hawana Imani juu yako au wale ambao hawajafanikiwa ni rahis Sana kukatishwa Tamaa hivyo unalazimika kuwa makini Sana katika kuchagua marafiki ambao watakutia moyo kila wakati hata ukiwa katika Hali ngumu kiasi Gani wao watakupa moyo na kukusaidia kukuta katika shida hiyoo.
2.Kupatwa na msongo Wa mawazo kama utakuwa na marafiki au watu ambao sio sahihi katika mtaji wako ni rahisi kukupatia msongo Wa mawazo kiurahisi Sana maana sikuzote tunajua kuwa Rafiki mbaya hapendi wewe ufanikiwe hivyo atafanya lolote lile ili akufelishe hivyo inakupasa uwe makini Sana katika kutafuta mtaji watu ili usije jutia.
3.Kutofikia Malengo Ukiwa na watu au marafiki ambao hawana future juu ya maisha Yao nirahisi pia kukufanya wewe usiwe na future hivyo kuishia kukata tamaaa na kutokufikia malengo yako yoyote Yale katika maisha yako na mwisho wa siku unaiahia kuwa maaikini tu.
4.Kujihisi mwenye Gundu/Mkosi au mtu asiye na Bahati, pindi unapopitia katika wakati mgumu wa maisha yako kama utakosa watu wakukupatia msaada utajiona kama ni mtu mwenye Gundu na Mkosi hiyo yote itatokana na kuchagua watu vibaya.
5.Kutokujiamin, Ndugu yangu katika uchaguzi wa watu wako wa karibu ni lazima ujue kuchagua watu wenye Imani Zaid kubwa Zaid yako na kama utachagua watu wenye Imani ndogo kuliko yako basi lazima utakata tamaa na ikishakuwa hivyo ni lazima ukose kujiamin katika maisha yako yote.
Nimeanza na madhara yakuchagua watu(marafiki) wabaya katika mzunguko wa maisha yako ya kila siku ili uweze kuzingatia Zaid na sasa tunamalizia na faida za kuchagua watu sahihi katika maisha yako ili uweze kuwafanya mtaji wako, Kwanza Ukizungukwa na watu sahihi katika maisha yako itakufanya ujiamini kwa kiwango kikubwa Sana na ili ufanikiwe basi unahitaji kujiamin na kuwa na Imani, ni rahisi Sana kufikia ndoto zako ambazo unazo maana watu ulionao ndio watakaokupatia mbinu zenye uhakika wa matokeo mazuri na kukufanya ufikie ndoto zako pia Itakusaidia kuokoa muda pindi unapokuwa katika changamoto Fulani maana watu wako wakaribu watakusaidia.
Faida za kuchagua watu sahihi katika mzunguko wa maisha yako ya kila siku ni nyingi kuliko kawaida hivyo inakupasa kuwa makini Sana katika uchaguzi wa MTAJI WATU ili uweze kutimiza ndoto zako zote na Malengo yako.
Lakini Katika hayo yote usisahau kwamba katika Mtaji watu mtaji wa kwanza kabisa ni wewe mwenyewe kabla ya watu wengine kuongezeka katika mzunguko wako Mtaji wewe ndio Kitu cha msingi Zaid ya chochote kitu maana hata ukiwa umezungukwa na watu sahihi katika mzunguko wako kama wewe mwenyewe hujajiweka Sawa basi hakuna faida yoyote ya Hao wengine kwanza ni lazima ujiamini, uwe na Imani ujitume katika ufanyaji kazi wako ukubali kubadilika pindi unapoambiwa umekosea usiwe mbishi na wala usiwe mjuaji pindi unaloshauliwa na pia usichoke kujifunza na mwisho usiwe mtu wa kukata Tamaa wala usiwe mtu wa kujiamin.
Hivyoo basi mtaji watu unaanzia kwako wewe mwenyewe kabla hata hujatafuta watu wengine katika kujazilizia mtaji wako. Hivyo basi mtaji Mkubwa katika biashara yoyote ile ni Watu maana wahenga wanasema WATU NI
MTAJI.
Mimi ni Davis Abely Nziku DNA (23)
Contact :0755386540
:0628488781
Mkazi wa Kigamboni Mjimwema

Upvote
7