Watu Pori - Nafsi ya Mtu

Watu Pori - Nafsi ya Mtu

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
images-59.jpg
WATU PORI - NAFSI YA MTU.

Watu pori a.k.a washamba a.k.a washamba a.k.a washamba /nyani wapya msitu wa zamani beat mjerumani mambo yote kwa Bonnie/

Verse ..1 ( mc koba)

Sikiliza haya ninayo kueleza leo na kesho usije kuyapuuza / kwenye mizizi ya Dhambi wivu ndio Unaongoza / kwa upande wa Mema upendo ndio wa kwanza/

Tena kabla ya kutenda nakuomba ufikiri kwanza/ kwani ukienda papara utakuja kuteleza / na kuaza kui laumu nafsi baada ya kuumiza / na ukaja kufeli ulilopanga kutimiza/ kama Sanaa ni Sanaa " ni Sanaa" we fanya kweli sasa wacha kushangaa/ kama uja kubalika usianze kuleta visa uzindi kuwajibika/ na uachake kabisa..!! We pana kushoto usiloliweza lione ka Gari la moto/ Mc kaa tayari kupokea changamoto/ ni Mc koba napenda mabadiriko/ Daruni nishatazama 🎤 mic kasema "sio lazima wote tuimbe" shtuka wacha uzembe/ mkulima shika jembe..!! / ulimwengu wa leo mi nakushangaa unaongopa "ukwimwi" huku una angaika Aaah/ ..

Unachekesha una amini Wazungu wakati Mungu unakataa Eeeh / Ewe mwana Elimu shika pen ujinga Sumu / uliza waliochezea hiyo nafasi ya muhimu / walichokipata nini..? Zaidi ya kusota na kuzuga mitaani Eeeh/...

Chorus ( mc koba)

Sogea karibu nikuambie Eeeh/
Nitakayonena uyasikie Eeeh/
Watu wananishangaza mie Eeh/
Nafsi zao hasieleweki eeeh/
Mkanye mjinga akuchukie Eeh/
Mipango yako hakuharibie Eeh/
Na sauti inanichosha mie Eeeh/

Eeeh eeeh eeh...!!

Verse 2..( Dogo ditto)

Inanichanganya kuona mnyonge anatukanwa / hata kile kidogo alicho nacho ana nyang'anywa..Aah..!! / ni nafsi ya mtu kwa vile imekosa Imani / basi ni chuki moyoni kila siku hakuna Amani " hakuna amani"/ namshangaa....! moyoni ana furaha kwenye Bar / Mambo yaki haribika kwenye ibada ana haha " ana haha./ ni mtu mzima ukimuona utamuita Babu/ anaona Aibu nyumbani ni Tabu tu / maisha yake ni kama adhabu akienda Bar miguu juu / mbona ana jenga chuki sababu yule kapata/ wakati sehemu ya ibada ana kesi kaiba sadaka/ si unge fanya kazi ujitume brother unge zinyaka .... si ungefanya kazi ujitume uenda ungezipata / ni siku gani..? Muda gani..? Na nchi gani..? Wamekuambia uangushwa kama majani/ kifkra upo hoi bini Taabani bila kutafuta uzipate kakuambia nani..?/ fanya kazi ...........usinichekeshe unapenda ....!! staff uta ombaje kazi mchori wakati unaongopa wafu..

Chorus ( mc koba)

Sogea karibu nikuambie Eeeh/
Nitakayonena uyasikie Eeeh/
Watu wananishangaza mie Eeh/
Nafsi zao hasieleweki eeeh/
Mkanye mjinga akuchukie Eeh/
Mipango yako hakuharibie Eeh/
Na sauti inanichosha mie Eeeh/

Verse..3 ( mc koba & ballet)

Ni nafsi ya mtu imekosa Imani/iwe dunia na hata mbinguni/ binadamu wa leo afadhiliki/ mpe kila kitu mpe atakushiti..

Maana wema unapozidi mauti/
Wana lengana kwa bunduki na manati/
Wana rongana kwa uchawi wa saniki nafsi zao zimejaa chuki binafsi/..

Verse..4 ( afande sele)

Mwingine...Mwingine...siku nyingine....mtu mwingine....
Anakuja kwako anashida ameshindwa Tena mikono Nyuma / amekonda "amekonda" una mtazama kwa huruma na kukwepa lawama/ unasema loooh..!! Lazima nimpige Tafu kwa moyo mkuchufu/ tena bila kujali skendo zake za uharifu / na uchafu wa mwili na Tabia unakua nae unaishi nae kama wife for life kumbe ni knife 🔪/ ana kusifu machoni moyoni ana kusanifu/ ana beef Aiseeh...!! ni mbwa mwitu anae winda kuliko chatu/ ndio nafsi yake / hata U mpe kila kitu sasa basi/ kama wasipo rudi wanao kwenda mbele za haki / ndivyo kilicho pinda kime pinda akinyoosheki/ basi nawaambia naku Abia asie shiba kwenye sinia/ hato shiba kwenye kijiko/ na tena nawaambia utafundishwa na Dunia kama ujafunzwa na mama Yako/ shauri yako Simba mzee....

Chorus..( Mc koba)

Sogea karibu nikuambie Eeeh../
Nitakayo nena uyasikie Eeeh./
Watu wana nishangaza mie Eeeh./
Nafsi zao hasielewiki Eeeh./
Mkanye mjinga akuchukie Eeeh./
Mipango yako hakuharibie Eeeh/
Na sauti inanichosha mie Eeeh /

Eeeh Eeeh Eeeh ..

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
 
Back
Top Bottom