Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kujipatia zaidi ya millioni 81 kwa njia ya udanganyifu kwa vijana zaidi ya 80 waliokusanywa kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Akitoa taarifa kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Benjamini Kuzaga, amesema Watuhumiwa hao wamekamatwa mapema hii leo katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambapo walikuwa wakijipatia fedha kwa kuwarubuni vijana kuwa watawapatia ajira kwenye kampuni ijulikanayo kwa jina la Q NET na Global Alliance kwa kuwatoza 40,000 hadi milioni tano ili wawapatie ajira katika kampuni hizo
Amesema watuhumiwa waliokamatwa ni William Hamis, mkazi wa Mwambene, Tyson Lubida, mkazi wa Shewa, Onesmo Hildepbonce, mkazi wa Isyesye, Charles Masanja, mkazi wa Iwambi, Chemka Mwanyanga, mkazi wa Iwambi, na Gracia Ephraim, mkazi wa Isyesye Jijini Mbeya na Ezekiel Mgogo, mkazi wa Igunga mkoani Tabora, waliokuwa na vijana kwenye nyumba zilizopo maeneo ya Iwambi, Shewa, Isyesye na Iyunga Jijini Mbeya.
Video:
https://www.facebook.com/
View: https://www.facebook.com/share/v/1KxPnNXspj/