Uncle Rukus
JF-Expert Member
- Jun 16, 2010
- 2,415
- 398
Taarifa ambazo zimethibitishwa na kamanda wa polisi mkoa Simon Sirro,
zinadai jeshi hilo linawashikilia watu sita ikiwa ni pamoja na mjumbe
wa kamati ya siasa wa CCM Mkoa Ellen Bogohe wakidaiwa kuhusika na
kupanga njama za kumuua aliyekuwa mbunge wa Busega Dk. Raphael
Chegeni. Inadaiwa mpango wa uaji ulikuwa umeandaliwa na mbunge mmoja
wa CCM kanda ya ziwa. Naendelea kufuatilia zaidi isipokuwa kamanda
Sirro amesema jeshi lake litatoa taarifa kwa vyombo vya habari kesho.
Jamani mimi naona MZEE NDESAMBURO alitoa laana kali sana juu ya chama cha magamba!tumuombe aibatilishe nini?
Hee mbona makubwa!! Wenyewe kwa wenyewe wanaanza kuuana tena? Tuelezee yanayojiri mkuu
Jaribu kueleza kilicho andikwa kwenye gazeti kwa ufupi. Wengine hatupo Tanzania au sehemu ambayo unaweza kupata gazeti hilo. Habari uliyotoa hajitoshelezi. Kama unalo hilo gazeti jaribu kuweka ufupisho wa hiyo habari.
Katika hali isiyo ya kawaida kundi la watu wakiongozwa na wana ccm walio kwenye kamati kuu za chama mkoani mwanza wamekamatwa hotelini wakijipanga jinsi ya kumuuua dk chegen,mtu aliepangwa kummaliza mh chegeni ambae aliukosa ubunge anaitwa kamanda chakaza kutoka kahama ambae aliwasili tar 12 kwa ajili ya kusubiri kikao walichokaa tar 13 kujua anapata ngapi baada ya shuguli..polisi wamekiri kutonywa mchezo huo mchafu na kusema wana vielelezo vyote tangu wanaitana toka kahama na mpaka siku aliekuja na ndege ya precission mwanza akitokea dar na million 10 kwa ajili ya mgao...
Loh chama amna huruma nyie yaani mmekosesha ubunge bado mwataka kummaliza siasa weee huna maana kabisa unataka kuondoa uhai wa mtu loh!!kweli chama cha majambazi
Rais kikwete moto umeanza unauweza???
Kwa habari zaidi
nunua tanzania daima