samora10
JF-Expert Member
- Jul 21, 2010
- 7,602
- 4,811
Njama za mauaji CCM
DK. CHEGENI ANUSURIKA KUUAWA KWA RISASI
na Sitta Tumma, Mwanza
KATIKA hali ya kushtusha, kundi la mtandao wa watu sita akiwemo mjumbe wa Kamati Kuu ya Siasa (CCM), mkoani Mwanza, wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kula njama na kutaka kumuua kwa kumpiga risasi aliyekuwa mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega wilayani Magu mkoani hapa, Dk. Raphael Masunga Chegeni (CCM).
Watuhumiwa wa mtandao huo wa mauaji, walikamatwa Aprili 13 mwaka huu mkoani Mwanza, wakiwa katika harakati maalumu za kumuwinda kumuua Dk. Chegeni, ambaye katika Uchaguzi Mkuu uliopita 2010 alishindwa kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho tawala, na sababu kuu inayodaiwa kutaka kumuua mbunge huyo wa zamani wa Busega ni uhasama wa masuala ya kisiasa.
Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima jana jijini Mwanza zinaeleza kwamba mtandao huo wa kutaka kumuua kwa kumpiga risasi Dk. Chegeni uliandaliwa tangu wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana na anayedaiwa kuhusika na mpango huo ni mwanasiasa mmoja ambaye pia ni kiongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (jina tunalo).
Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo pia zimethibitishwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, zimewataja waliokamatwa na polisi kwa tuhuma hizo kuwa ni Dismas Zacharia Kamani (mratibu wa mauaji), Erasto Casmil (alitafuta wauaji), Queen Joseph Bogohe (alitumika utoaji wa fedha kwa wauaji), Ellen Bogohe, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya siasa CCM mkoani Mwanza, na diwani wa zamani wa Viti Maalumu Kata ya Kisesa, wilayani Magu mkoani hapa.
Wengine wanaodaiwa kuhusika kwenye mtandao huo wa kutaka kumuua Dk. Chegeni ambao wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mwanza, walitajwa kuwa ni Hamis Masoud mkazi wa Furahisha jijini hapa na Richard Kamugisha mkazi wa Mwanza.
Mbali na watuhumiwa hao wanaodaiwa kukamatwa, mtumishi mmoja wa serikali katika kitengo nyeti (jina na kitengo chake tumevihifadhi), kwa sasa, naye ametajwa kuwemo kwenye mtandao na hujuma hizo za kutaka kumuua Dk. Chegeni, lakini mtumishi huyo bado hajakamatwa na polisi.
Ni kweli tukio la kutaka kuuawa Dk. Chegeni lipo, na baadhi ya wanamtandao huo wa mauaji wamekamatwa na wako ndani kwa sasa!
Kati ya hao waliokamatwa, yupo mmoja wao presha ilimpanda baada ya kubanwa maswali mazito na polisi na hasa alipoona mawasiliano yake yote ya kupanga mikakati ya mauaji yapo mikononi mwa polisi, kilisema chanzo kimoja ambacho hakikutaka kutajwa jina lake kwa sababu si msemaji wa polisi.
Habari zinaeleza kwamba siku ya Aprili 13 mwaka huu, baadhi ya wanamtandao hao wa walizulu jijini Mwanza kwa lengo la kukamilisha taratibu zote za mauaji, ikiwa ni pamoja na kukodi mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Kamanda Chakaza kutoka wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya kumchakaza Dk. Chegeni kwa risasi.
Inadaiwa kwamba mhusika wa mtandao huo aliahidi kuupatia mtandao wake huo sh milioni 9 na kati ya fedha hizo sh milioni 4 zilikuwa kwenye utaratibu wa kupelekwa jijini Mwanza kwa ajili ya kutimiza azma hiyo ya mauaji, huku baadhi ya fedha zikidaiwa kutumwa kwa njia ya simu ya kiganjani.
Kulingana na tukio hilo, taarifa zinadai kwamba siku hiyo watuhumiwa hao wa kupanga mauaji walifika jijini Mwanza wakiwa wamepewa sh milioni 1.2 na kwamba baadaye polisi walipata taarifa juu ya mkakati huo kisha kuanza kuweka mtego ambapo ulifanikiwa kuwakamata watu hao.
Baada ya kufika Mwanza, polisi walipata taarifa na kuweka mtego ambao ulifanikiwa kunasa mawasiliano yote ya mikakati ya kumuua Dk. Chegeni kwa kutumia bunduki na rissi za moto...baada ya hapo polisi walifanikiwa kuwazingira na kuwakamata wakiwa kwenye hoteli maeneo ya mtaa wa Rufiji, kilisema chanzo kingine huku kikisema: Siasa ni mchezo mchafu na mbaya sana.
Uchunguzi wa Tanzania Daima unaonesha kwamba watuhumiwa hao wote kwa ujumla huenda leo Jumanne watapandishwa mahakamani kwenda kujibu tuhuma zinazowakabili na kwamba mtuhumiwa namba moja (jina linahifadhiwa), wa kupanga mtandao huo wa kutaka kumuua Dk. Chegeni ambaye hivi sasa anajihusisha na masuala ya biashara, bado anatafutwa na polisi na muda wowote akikamatwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yake.
Alipoulizwa jana ofisini kwake iwapo ni kweli tukio hilo lipo na watuhumiwa wamekamatwa, kamanda wa polisi mkoani Mwanza na kamishna mwandamizi wa polisi nchini, Simon Nyakoro Sirro, alisema kwa kifupi: Tumewakamata, lakini kesho (leo) nitawapeni taarifa zote, kuna vitu fulani bado nakamilisha.
Hata hivyo Tanzania Daima ilipomtafuta Dk. Chegeni ili kuelezea tukio hilo la kutaka kuuawa kwake, hakuweza kupatikana mara moja, licha ya kupata taarifa kwamba alikuwa katika hali ya hofu zaidi.
Matukio ya namna hii yakiwemo ya badhi ya wanasiasa mkoani Mwanza kumwagiwa tindikali mwilini si geni, kwani matukio kadhaa ya mauaji ya wanasiasa, kumwagiwa tindikali mwilini yalishawahi kutokea mkoani hapa, ikiwa sababu kuu ni uhasama wa kisiasa.
Kati ya mwaka 1995 aliyekuwa mbunge wa Mwanza mjini kipindi hicho, marehemu Saidi Shomali, alimwagiwa tindikali usoni na watu waliosadikiwa kuwa ni mahasimu wake wakubwa wa masuala ya kisiasa, mwaka 1994 aliyekuwa diwani wa Kata ya Kitangiri jijini Mwanza, Sylvester Lubala naye alipata maswahibu kama hayo.
Lakini matukio kama hayo, yaliendelea kuukumba mkoa wa Mwanza ambapo mwaka jana 2010 aliyekuwa meya wa jiji la Mwanza na diwani wa Isamilo, Leonald Bandiho Bihondo (CCM), alikamatwa na kufikishwa mahakamani hadi sasa kwa tuhuma za kula njama na kumuua kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili Katibu wa CCM Kata ya Isamilo, Bahati Stephano kwa kile kinachodaiwa kuwa na uhasama dhidi yao wa masuala ya kisiasa.
source ;tanzania daima