Watu Tisa wafariki dunia, 44 wajeruhiwa ajali ya basi na lori Morogoro

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Watu tisa wamefariki dunia papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Hai kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba shehena ya sukari katika eneo la Lugono Melala, barabara kuu ya Morogoro–Iringa.

Ajali hiyo imetokea wakati magari hayo mawili yalipogongana kwa nguvu, na kusababisha maafa hayo makubwa.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk Daniel Nkungu, ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Alhamisi Juni 12, 2025 na hospitali imepokea miili ya marehemu tisa.

Ameeleza kuwa kati ya miili hiyo, mitano ni ya wanaume na minne ni ya wanawake.

Aidha, Dk Nkungu amesema hospitali hiyo imepokea majeruhi 44, ambapo kati yao watu wazima ni 37 na watoto ni saba.

Dk Nkungu amebainisha kuwa majeruhi wengi wamepata mivunjiko na wanaendelea kupatiwa matibabu ya haraka chini ya uangalizi wa karibu wa wataalamu wa afya.

Amesema kuwa miili minne kati ya tisa tayari imetambuliwa na ndugu wa marehemu, ambapo utambuzi huo umewezekana kupitia vitambulisho walivyokuwa navyo marehemu hao.

Dk Nkungu amesema miili mingine bado haijatambuliwa na imehifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, ikisubiri utambuzi na taratibu zaidi kutoka kwa familia husika.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema kwamba atatoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari muda si mrefu, kuhusu chanzo cha ajali hiyo na hatua zinazochukuliwa.

Screenshot 2025-06-12 112306.png
 
Duuh hatari!
 
Tanzania inafuatiwa na Congo kwa ajali,kila siku ajali,mbona inchi za wenzetu kama Marekani,Canada,China,Uingereza na kwingineko kuna magari mengi lakini hatusikiagi ajali?
 
Ajali zipo ila sio sana,hawazitangazi ili uwaone wapo safi kila idara

Wazungu siku zote wanapambania kujenga taswira yao ionekane ni nzuri
 
Wameripoti Mwananchi Communication
1749719755854.jpg
 
Poleni wana Moro,poleni ndugu wa Marehemu,poleni Majeruhi wote.Wapumzike kwa amani Marehemu wote.
 
Tanzania inafuatiwa na Congo kwa ajali,kila siku ajali,mbona inchi za wenzetu kama Marekani,Canada,China,Uingereza na kwingineko kuna magari mengi lakini hatusikiagi ajali?
Acha uongo uongo wewe,Tanzania haipo ata kwenye nchi 10 zinazoriport ajali nyingi Kwa mwaka Africa..
Kwanini mnapenda kuipa ubaya ubaya nchi yenu
 
Dah, Miscalculation hizo za road. Ukigongana hizi gari za mizigo kishindo chake si mchezo.
 
Mkiambiwa bara bara iongezwe Upana ile hamtaki , bara bara ya Morogoro Road iringa road Dodoma road Zina magari mengi sana zinapaswa kuongezwa Upana ,
 
Tatizo ni madereva kutofuata sheria za barabarani .Gari zikigongana uso kwa uso mara nyingi ni mwendo wa kasi na ku overtake sehemu zisizoruhusiwa kufanya hivyo na ulevi.
 
Ajali zipo ila sio sana,hawazitangazi ili uwaone wapo safi kila idara

Wazungu siku zote wanapambania kujenga taswira yao ionekane ni nzuri
UONGO MTUPU!
NIMEKAA HIZO NCHI,AJALI ZIPO KIDOGO SANAAAAA.

HATA MIEZI 6 INAPITA BILA AJALI.

WATU WANAFATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI,NYIE KILA KITU HAMTAKI KUTUMIA AKILI,HALAFU MNASEMA WAO HAWATANGAZI AJALI ZAO.

WAKATI MNAISHI NCHI YA KUTOKUJALI KILA KITU.

FATILIA CHANZO CHA AJALI UONE KAMA SIO UZEMBE AU KUTOKUJALI.
 
Tatizo ni madereva kutofuata sheria za barabarani .Gari zikigongana uso kwa uso mara nyingi ni mwendo wa kasi na ku overtake sehemu zisizoruhusiwa kufanya hivyo na ulevi.
Kuna wakati Wana sinzia pia safari ya Masafa marefu inachosha so laiti kama bara bara ingekuwa ni Pana na imefanywa kuwa ya njia moja tu Kwa magari yapitayo upande mmoja Kisha katikati wanaweka barrier pasingekuwa na hayo matukio
 
Back
Top Bottom