Watu tisa waliozaliwa na viungo vya ziada na kuishangaza dunia

Bitoz

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2015
Posts
30,823
Reaction score
126,553
Mungu huwa hakosei kuumba ?
Mimi sijui na lengo langu siyo kumkosoa Mungu wala kumuhoji bali kuzungumzia kuhusu binadamu waliozaliwa na viungo vya ziada na kuishangaza dunia

Kawaida mtu ana meno 32,miguu miwili,pua moja,mikono miwili,moyo mmoja n.k ila hawa watu viungo vyao vimepitiliza idadi



9/Hazel Jones

Demu Huyu alizaliwa na uke pea mbili
Huyu alisumbuliwa na ugonjwa wa kushangaza wakati anakaribia kuvunja ungo na akajikuta anapata hedhi mfululizo kama mvua za masika zinazosumbua wakazi wa mabondeni
Anatokea huko High Wycombe nchini Uingereza
Tatizo lake linajulikana kama Uterus Didelphys yaani pia ana vyumba viwili vya uzazi

Alipoambiwa na daktati kwamba ana uke na vyumba vya uzazi pea mbili akamjibu anajisikia fahari japo atahitaji mtu antoe bikra kote kote (sizungumzii tundu la nyuma......mi simo nasema simo !!<
 
8/George Lippert

Huyu bwana mdogo George jamani kapendelewa sana na muumba !!
Alizaliwa mwaka 1844
Alizaliwa akiwa na miguu mitatu na mioyo miwili lakini ilipofika siku ya kufa haikufua dafu mioyo yote injini zilisimama na nshua akavuta kama wengine tu wenye moyo mmoja!!
Huyu jamaa hakujua kama ana mioyo miwili tena inayopiga kazi sawasawa hadi mwaka 1906 alipoenda hospitali na daktari kumtonya ana moyo wa ziada
Miguu yake yote mitatu ilikuwa mizima na jamaa ukimchokoza utakula mateke zaidi ya shukrani ya punda.....Huyu ndo bwana Lippert

Miguuni jumla alikuwa na vidole 16
Hadi leo jamaa rekodi zake bado ni funika bovu labda zivunjwe na wanyama wengine ila siyo binadamu

..........................................................................


Huyu demu alizaluwa akiwa na miguu minne lakini bado kaachwa mbali na bwana Lipert sababu Lipert alikuwa pia na mioyo miwili
 
[emoji23] [emoji23] style ya uhadithiaji, ipo tununu!!
 
7/Alfie Clamp

Karibia kila aliyesoma Biology japo Form Two anaelewa maana ya DNA
Huyu dogo alizaliwa mwaka 2010 akiwa na Extra strand DNA tuseme ana DNA zaidi ya pea mbili
Alizaliwa akiwa kipofu(mlemavu wa macho), pia alikuwa na ulemavu mwingine kibao hivyo kuwalazimu madaktari wamfanyie uchunguzi uliopitiliza
Mwisho wa siku wakambamba dogo ana DNA ya kushangaza ambayo haipatikani popote pale duniani (angalia picha)
Hayo ndo maajabu ya dogo Alfie
.................................................................

.Nyongeza by Lyon Lee

Ni kweli na nadra sana kumkuta mtu kuwa na DNA ya haina hii ila japo hii ni evidence tosha kuwa mutation inatokea na ikitokea kuna impacts kubwa kama hizo ...ila hii wataalamu wanaiterm kama advanced mutations. .
Kiukweli binadamu wa kawaida huwa na DNA ambayo ni double strand ...na tunajua DNA ni kitu muhimu katika maisha ya binadamu. ..na ndo hii DNA inayozalisha RNA ambayo ni single strand ....hapa usije sema RNA inaweza kuwa na double strand ....haiweziiii

Zile base sugar zinazopair kutengeneza double strand ikitokea katika hali ambayo siyo ta kawaida mfano Hoogsteenn Base sugar ukipenda H ikabind na sugar base tulizozizoeaa ...mfano natumia herufi kidogo na nisiwachoshe ...T lazima ikutane na C ...ikitokea kamailivotokea kwa dogo H ikajipendekeza na mechanism ikakubar bhasi H*DNA tunaipata ambayo ni triple strand.
Asante mdau
 
6/Deepak Pastwan

Huyu ni dogo kutoka familia maskini huko nchini India
Alizaliwa mwaka 2010 akiwa na miguu ya ziada "iliyoota" kifuani
Dogo alizaliwa akiwa na miguu 8 yaani dogo kifuani ana miguu kama matawi ya miti
Wazazi wake hawakuifurahia hali hiyo hivyo kuomba iondolewe maaba mtoto wao alikuwa anadhihakiwa kitaani kuitwa mti unaotembea ila hawakuwa na pesa hivyo hospitali ikawaonea huruma kutokana na umaskini uliowakithiri hivyo kumfanyia upasuaji bure na ukafanikiwa kuiondoa na sasa hivi ana hali ya kawaida tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…