Watu tisa waliozaliwa na viungo vya ziada na kuishangaza dunia

Watu tisa waliozaliwa na viungo vya ziada na kuishangaza dunia

Ana makusudio yake kufanya hivyo maana yeye ni mjuzi zaidi ndio maana kuna weupe na weusi ,wafupi na warefu.
Sijakataa kama inawezekana ana makusudio yake.

Tatizo linakuja mtu anakwambia "ana makusudio yake" halafu hawezi kuyaelezea hayo makusudio ni yapi.

Kusema hivyo si kutoa jibu, ni kukubali kwamba hujui jibu unaungaunga habari tu.

Sasa kwa nini Mungu kaweka weusi na weupe na hali hiyo ikasababisha ubaguzi wa rangi kama alikuwa na uwezo wa kuumba duniaisiyowezekana kuwa na ubaguzi wa rangi?
 
Sijakataa kama inawezekana ana makusudio yake.

Tatizo linakuja mtu anakwambia "ana makusudio yake" halafu hawezi kuyaelezea hayo makusudio ni yapi.

Kusemahivyo si kutoa jibu, ni kukubali kwamba hujui jibu unaungaunga habari tu.

Sasa kwa nini Mungu kaweka weusi na weupe na hali hiyo ikasababisha ubaguzi wa rangi kama alikuwa na uwezo wa kuumba duniaisiyowezekana kuwa na ubaguzi wa rangi?
Kila kitu kinatokea kwa sababu maalumu , halafu ukae ukijua hapa duniani siyo makazi yetu ,hapa duniani ni njia tu .
 
Hao hawajaumbwa na Mungu, kama wameumbwa na Mungu basi sisi wengine katupunja.

Sasa Mungu gani anapunja wengine na kupendelea wengine?
Hapa umebifikirisha maana yule bwana mdogo George Lipert kapewa miguu mitatu kana stuli wakati sisi mamilioni tuna miguu miwili
 
Kila kitu kinatokea kwa sababu maalumu , halafu ukae ukijua hapa duniani siyo makazi yetu ,hapa duniani ni njia tu .
Kauli hizo zina matatizo mengi sana.

1. Mtu anaposema kila kitu kinatokea kwa sababu maalum, halafu hawezi kuzielezea hizo sababu maalum ni zipi, hii katika kanuni za kuchambua mambo tunaiita weakness ya "Deus ex Machina". Unamaliza mjadala kwa kumshusha Mungu wa kuchongwa asiye na maelezo ya kutosha.Yani ni kama Rambo kazungukwa na jeshi la watu 1,000, unaona kabisa hapa hawezi kutoka, halafu eti linashuka bonge la radi linaua wale maadui wote 1,000 halafu Rambo peke yake anapeta.

Hapo kama movie unaweza kupotezea ukasema hili movie tu.

Lakini kama mtu anakuelezea hii fact lazima uone unauziwa mbuzi kwenye gunia.

2. Hapa duniani si makazi yetu, tunapita tu, hii ni argument weak sana.

Kwa sababu gani? Mimi kama baba, nikikodi nyumba ufukweni New Jersey Beach huko nikae na wanangu kwa wiki tatu napunga upepo wa baharii, hapo nitakapokodi si kwangu, ni "vacation stay" tu, napita.

Lakinihilo halina maana eti kwa sababu napita tu ndio pawe pachafu, niruhusu maji yamwagike kila pahali, watu wapate magonjwa niachie tu, watu wapigane risasi wauane, niseme hapa si makazi yetu tunapita tu, wakati uwezo wa kupafanya hapo tunapopita na nyumbani tunakoenda kote kuwe pazuri kabisa.

Huyo Mungu aliyeumba ulimwengu huu akafanya mabaya yawepo tu, wakati aliweza kufanya mabaya yasiwepo, alifanya hivyo kwa sababu kuondoa mabaya kunatumia umeme na yeye aliogopa kumaliza LUKU yake?

Kwa nini hakuumba hapa pakiwa hapawezekani kufanyika mabaya na huko tunakoenda kusiwezekane kufanyika mabaya pia?

Na unaweza kuthibitisha kwamba huko mnakosema tunakwenda nyumbani kupo kweli na si hadithi tu?

Kuna mtu anaweza kuthibitisha hilo?
 
Last edited:
Hapa umebifikirisha maana yule bwana mdogo George Lipert kapewa miguu mitatu kana stuli wakati sisi mamilioni tuna miguu miwili
Kwahiyo kama unaamini Mungu yupo, hapo itabidi uulize, Mungu ana ubaguzi kuwapa wengine miguu mitatu na wengine miwili?
 
2/Maria De Nazare
ca548e744faebda2167efc548198da45.jpg
7358fafc025296b80d935d62018af1f7.jpg

Huyu binti amezaliwa miaka 24 iliyopita na bado anadunda tu
Alizaliwa na vichwa viwili vinavyofanya kazi vizuri kabisa yaani kama aina fulani ile ya mnyama mwenye vichwa viwili sijui mnawita dragon
Wazazi wakaamua kumpa jina linalofanana na manaye Yesu Maria wa Nazareth ila usilitaje bure jina la Bikira Maria hivyo huyu anaitwa tu Maria De Nazare badala ya Nazareth
Huyu ni binti wa Kibrazil kiuhalisia ni mapacha walioungana yaani chini ni mtu mmoja ila juu ndo vichwa viwili au tuseme tu mtu mwenye vichwa viwili

Tofauti kabisa na wale akina Maria na Consolata huyu ni mtu mmoja kuanzia chini shingoni hadi miguuni ila ana vichwa viwili ndio maana anahesabika ni mtu mmoja tu
dunia ina maajabu
 
Kwahiyo kama unaamini Mungu yupo, hapo itabidi uulize, Mungu ana ubaguzi kuwapa wengine miguu mitatu na wengine miwili?
Naomba niweke wazi
Mimi sijui kama Mungu yupo au hayupo yaani sipo upande wowote
 
Naomba niweke wazi
Mimi sijui kama Mungu yupo au hayupo yaani sipo upande wowote
Umesiamama pazuri sana.

Profesa Yuval Noah Harari ameelezea vizuri sana katika vitabu vyake "Sapiens: A Brief History of Humankind" na "Homo Deus: A Brief History of Tomorrow" kuhusu dhana nzima ya kuamini kuwepo Mungu kuwa ni jitihada za watu kuziba pengo la ujuzi, kwamba pale ambapo hatujui jibu, watu tuko tayari sana kuziba pengohilo kwa kusema habari za Mungu, halafu tukija kujua, tunamsukuma huyo Mungu kwenye jambo lingine ambalo hatulijui.

Kifupi ni kwamba, watu tunakuwa wagumu sana kusema "sijui jibu, ngoja nitafute jibu".

Kwa hiyo, nikisikia mtu anasema hajui, nafurahi sana.

Kwa maana, ukisema hujui na kutafuta jibu lakweli kwa juhudi, utalipata.

Lakini ukiw ahujui na kusema unajua jibu, jibu ni "kazi ya Mungu", hutakaa upate jibu la kweli.
 
Mungu huwa hakosei kuumba ?
Mimi sijui na lengo langu siyo kumkosoa Mungu wala kumuhoji bali kuzungumzia kuhusu binadamu waliozaliwa na viungo vya ziada na kuishangaza dunia

Kawaida mtu ana meno 32,miguu miwili,pua moja,mikono miwili,moyo mmoja n.k ila hawa watu viungo vyao vimepitiliza idadi



9/Hazel Jones
d8b33b5dda7df285bc613bea06273108.jpg
2f24682c0af169ea6426dd0363eb50f4.jpg

Demu Huyu alizaliwa na uke pea mbili
Huyu alisumbuliwa na ugonjwa wa kushangaza wakati anakaribia kuvunja ungo na akajikuta anapata hedhi mfululizo kama mvua za masika zinazosumbua wakazi wa mabondeni
Anatokea huko High Wycombe nchini Uingereza
Tatizo lake linajulikana kama Uterus Didelphys yaani pia ana vyumba viwili vya uzazi

Alipoambiwa na daktati kwamba ana uke na vyumba vya uzazi pea mbili akamjibu anajisikia fahari japo atahitaji mtu antoe bikra kote kote (sizungumzii tundu la nyuma......mi simo nasema simo !!<
hahaaaa
 
Back
Top Bottom