Watu tunalia na vifurushi vya NHIF Mtibeli amegundua bima ya elfu 40 , naipataje wadau ?

Watu tunalia na vifurushi vya NHIF Mtibeli amegundua bima ya elfu 40 , naipataje wadau ?

Yaani bima 40k wewe jamaa umetuona watoto humu JF kila mtu si angekata

Mimi siongei kwa kumfurahisha yoyote naongea mambo kwa uhalisia wake.

Hiyo Bima ipo na inafanya Kazi na watu wananufaika.

Ingia Google andika CHF
Ukiipata nenda Kituo chochote cha afya kakate.

Baada ya wiki MBILI nenda katibiwe
 
Asilimia kubwa hiyo bima ya afu 40 haina huduma za maana mkuu tena wakati mwingine hata paracetamol utaelezwa ukajinunulie hebu fatilia
 
Ndugu yangu nasema haya kwa mema tu na kukuelewesha kuna watu wana hali ni mbaya na ngumu kuliko unavyofikiria tenga muda tu pita pita mitaani Mtibeli utalia nakuambia

Hao watu mbona pesa za waganga wa kienyeji wanazo lakini zingine Hawana?

Mimi na ushahidi ya watu wengi wenye maisha duni Kabisa lakini wakiagizwa Laki Moja na waganga wanazipata.

Unataka tudekezane?
 
Ndugu yangu nasema haya kwa mema tu na kukuelewesha kuna watu wana hali ni mbaya na ngumu kuliko unavyofikiria tenga muda tu pita pita mitaani Mtibeli utalia nakuambia
Nakuunga mkono mkuu, sisi wengine tunafanya shughuli zetu vijiji tunaona hali halisi. Unataklmani uwasaidie lakini unajikuta huna uwezo. Kuna watu wanaishi maisha magumu sana hapa duniani.
 
Upo Mkoa gani ili Twende kwa vitendo na ushahidi?
Hapo uliposema tu nipo mkoa gani nishakuelewa sana mkuu

Ungeuliza umefanya uchunguzi mikoa gani ningejua na wewe umetembea tembea ila kuuliza mkoa gani maana yale wewe mwenyewe umefanya utafiti kupitia mkoa mmoja tu uliopoa,

Nakueleza tena tembea ujionee utalia
 
Nimeona member mmoja anajiita Robert Heriel Mtibeli anaungana na RC chalamila na kusema kuna bima ya Elfu 40 ina cover mpaka uzazi , Ultrasound,X ray ...etc

Naipataje mnaoijua ?
Usijaribu kukata hiyo bima ya chf unatibiwa Zahanati ndogo tu hospital za rufaa hawazipokei! Mi shuhuda mdg wangu alilazwa na vipimo vyote kuanzia utrasound tulilipia
 
Back
Top Bottom