Watu Unaokaa Nao Wanaweza Kubadilisha Umri Wako Kiakili

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Kuna kitu cha ajabu sana kuhusu maisha watu unaoishi nao wanaweza kabisa kubadilisha namna unavyojiona hata bila wewe kugundua. Ukiwa karibu sana na watu wa umri mkubwa, baada ya muda unaanza kujikuta unatabia za kikubwa automatically. Unaanza kuongea kwa utulivu, kufikiria maisha kwa seriousness, hata vitu vya kijinga vinaanza kukuudhi. Unaweza ukaanza hata kushauri watu mambo ya maisha kana kwamba una miaka 47 na viwanja vitatu huko Kigamboni.

Lakini sasa jaribu kuhamia kuishi sana na wadogo zako. Mwanzo utaanza tu kawaida “ah ni familia tu”. Kumbe hapo ndipo safari inaanza. Leo mnacheza PlayStation pamoja, kesho mnagombania pad, wiki inayofuata mnaanza kutupiana maneno ya kitoto hadi unasahau kabisa wewe ni mkubwa wao. Baada ya muda wanakuona sawa na wao kabisa. Hakuna tena ile heshima ya kaka mkubwa. Wanakuambia we tulia bana

Na tatizo kubwa zaidi si wao kukudharau, tatizo ni wewe mwenyewe kuanza kujisahau. Unaanza kujilinganisha nao. Wao wakinunua sneaker mpya unajisikia pressure pia. Wao wakikesha TikTok hadi saa nane usiku na wewe unajikuta upo pale mnacheka memes badala ya kuwaza maisha yako. Taratibu unaingia kwenye age bracket yao kiakili bila hata kutambua.

Ndiyo maana mazingira yana nguvu sana kwenye personality ya mtu. Ukiwa na watu wanaokufanya ujione responsible, na wewe unakuwa responsible. Ukiwa na watu wanaokufanya ujione mtoto mwenzao, baada ya muda utaanza kuishi kama mtoto mwenzao kabisa. Mwisho unajikuta una miaka 30 lakini bado mnagombania remote ya TV na watoto wa form two. AU UNA MIAKA 38 BADO UNATAFUTA GIRLFRIEND Na una mpenzi instagram na facebook yuko mwanza we uko songea..
 
Mtoa Uzi kafanya research ya kutosha .....andiko lake liko sahihi 98.99/%
 
Chai.

Basi baba au mama wa familia ambaye muda mwingi ana shinda nyumbani na watoto wake basi naye angekuwa na akili kama za watoto wake.
 
Back
Top Bottom