Watu watatu wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori, bajaj na pikipiki, iliyotokea leo, Novemba 3, 2026, majira ya saa tatu asubuhi eneo la Magomeni Kanisani, Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Mkoani Mtwara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Issa Suleiman amesema Jeshi la Polisi linamshikilia Dereva wa lori hilo, Ibrahim Hajibu (32), Mkazi wa Mtwara Mikindani, kwa madai ya kuendesha kwa uzembe na bila kujali.